Mwakilishi Nancy Pelosi achaguliwa tena Spika wa Bunge la Marekani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
perosi.jpg

Mwakilishi Nancy Pelosi alichaguliwa tena kuwa spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Jumapili kwa kipindi chake cha nne, akiwa na wingi uliopungua wa wawakilishi wa chama cha demokrat na changamoto zilizo mbele.

Mdemokrat huyo kutoka Jimbo la California alipata kura zilizohitajika kupata ushindi Jumapili alasiri, na huku Wademokrat wawili wakipigia kura wagombea wengine na wengine watatu wakipiga kura ya kusema walikuwapo. (bila kuunga mkono wala kukataa).

Wademokrat wanashikilia wingi wa baraza la wawakilishi kwa idadi ndogo katika Baraza jipya la 117, wakiwamo wademokrat 222 na Warepublican wapatao 211. Wawakilishi wengine wachache hawakuweza kupiga kura kwa sababu walikuwa wameambukizwa virusi vya korona au walikuwa na shida zingine za kiafya.

Kwa mara ya kwanza tangu Mei, Wabunge walipaswa kuwapo kwenye upigaji kura kura badala ya kutumia mfumo wa mtandao uliowekwa katikati ya janga hili. Kura hiyo ilidumu kwa saa kadhaa wakati wabunge waliletwa ndani ya ukumbi katika vikundi vidogo vidogo ili kuepusha idadi kubwa ya wajumbe katika ukumbi.

Bunge jipya linakabiliwa na changamoto kadhaa, kati yake kulishinda janga la corona ambalo hadi sasa limegharimu maisha ya wamarekani zaidi ya 350,000 na kufufua uchumi wa nchi.

Pelosi mwenye umri wa miaka 80 ameonyesha kuwa baada ya kipindi hiki cha miaka miwili hatagombea muhula mwingine kama Spika wa Bunge, kulingana na makubaliano yaliyofanywa na Wanademokrat mnamo mwaka 2018 ambapo walimtaka asigombee uspika wakati huo.
 
Mama ana miaka 80 yupo fiti anaunguruma atishiki ana maamuzi yasiyopingika kwa wamarekan walio wengi ni mfano wa kuigwa
 
Moja ya vitu vinavyonifanya nimshangae huku kwetu Bibi wa miaka 80 nguvu Hana kabisa
Ndugu yangu wenzetu wanakula vizuri na wanapata matibabu kwa uhakika. Sisi huku lishe ni taabu hata kwa mwenye fedha maana utakuta ana fedha lakini akasumbuliwa na ulaibu wa pombe hivyo, hufanya afya iwe ovyo, au achoke mapema.
 
Back
Top Bottom