Mwakibolwa: Tunasubiri amri tuanze mapambano

Mwakibolwa: Tunasubiri amri tuanze mapambano

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,368
Kiongozi wa Majeshi ya Kulinda Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC), Meja Jenerali,James Mwakibolwa amesema kwa sasa wanasubiri amri ya Umoja wa Mataifa waweze kutekeleza majukumu yao Mashariki mwa nchi hiyo.

Majeshi ya kulinda amani ya Tanzania tayari yako kwenye mji wa Goma, Mashariki mwa DRC pamoja yale ya Afrika Kusini. Majeshi ya Malawi bado hayajaingia DRC chini ya mpango huo wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, Monusco.

"Bataliani zote ziko tayari kwa mapambano, tumeshajipanga, zana zote ziko tayari, bado tu silaha ndogondogo...wanajeshi wote wako tayari kuanza kazi. Tunachosubiri ni amri ya UN tuanze kukabiliana na waasi," alisema Mwakibolwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC.

Alisema kuwa pamoja na kwamba waasi wa March 23 (M23) wameanza mashambulizi kukabiliana na majeshi ya Serikali ya DRC, wao hawajaanza kazi kwa kuwa hawajapewa amri kamili ya kupigana pamoja na kunyang'anya silaha.

Mwakibolwa ambaye ni mpiganaji kutoka Tanzania, alisema kuwa wanajeshi wote kutoka Tanzania wako salama na hakuna hata mmoja ambaye ametekwa wala kuumizwa na wanaendelea na mazoezi ya kivita pamoja na wenzao wa Afrika Kusini. Alisema Majeshi ya M23 yanapenda kuzusha mambo kuwateka kisaikolojia wapinzani, lakini wameshafahamu mbinu hizo.

UN imepanga kutumia vikosi vya askari 3,100 Mashariki mwa DRC katika mji wa Goma na vitongoji vyake kwa ajili ya kulinda amani.

Source; Mwananchi

Fagieni wahunu hao wate hadi Rwanda tuunganishe iwe sehemu ya kigoma
 
Kila la Kheri Jenerali.Nayaunga mkono majeshi yetu huko DRC
 
Piga hao halafu mpitie kwa huyu ---- kagame mfagie mnarudi nyumbani.
 
Sasa hii ni taaluma nyingine. Kulinda amani kwa DRC kuna hitaji kuwa na silaha na kupigana? Huku kwa DRC kuko tofauti ya kule kulinda amani kwa Sudani? Naomba anayefahamu anisaidie.

Lakini all in all, ninachokijua, kwa wingu hili, Kagame hawezi kuwa na amani na Tanzania. Kama kweli wingu liko namna hii. Kitisho chochote kwa M23 ni kitisho cha moja kwa moja kwa Kagame na serikali yake. Ili kumaliza mgogoro wa M23 nchini Kongo, UN hawana budi kudhoofisha nguvu zake ambazo ni Paul Kagame wa Rwanda.
 
bado sijaelewa , hivi sisi tumeenda kulinda amani au kupigana ?
 
Msiishie tu kuwakamata na kuua M23 pia hakikisheni mnamkamata Kagame dead or alive

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Vita ni Vita! Vita ya DRC ni ngumu kulingana na historia ya Congo haya yote ni matokeo ya historia ya utawala na Uongozi wao,it needs kujua madai ya waasi na wapi wanapishana na serikali ya kabila,waasi na kabila wanayo nafasi nzuri ya kuumaliza mgogoro huu wa muda mrefu amani haitaletwa na majeshi ya kulinda amani,wasipokaa mezani wakaelewana utaondoa kundi moja la waasi litakuja lingine miaka nenda rudi.
 
bado sijaelewa , hivi sisi tumeenda kulinda amani au kupigana ?
Tumeenda kulinda amani,na ili kulinda amani inabidi tuwanyang'anye silaha,na ili tuwanyang'anye silaha inabidi tuwapige.

Mytake:Tuache siasa!
 
hiki kikosi cha sasa kimeenda kupigana si kulinda amani.... hichi kikosi kimeenda kama peace enforcer not peace keeper!!! kinaruhusiwa kupambana directly kivita nk
 
Nilicheka sana juzi Futui walisema watafanya Rwanda sehemu ya kuanikia dagaa

Usicheke, hicho ndicho kitakacho tokea kama Nduli Kagame Dada, atahatarisha Usalama wetu eti kwasababu tu Tanzania inaunga mkono kwa vitendo, uwepo Amani drc. TUPO CHONJO tunafuatilia mwenendo wao. Hata media fulani kule Uganda iliwahi kutahadhalisha hatari iliyopo kwa Rwanda endapo watatubiipu wazee wa kazi kama walivyo wabiipu Uganda huko huko Congo, miaka michache iliyopita. Walipokuwa wanawaibia Wakongomani. Sasa, sisi sio wao, sisi ni sisi hatupigani vita nusunusu, tunasafisha kabisaa geremsi kwa ajili ya amani ya miaka mingi kwa nchi yetu. Juzi kwenye kumbukumbu ya mashujaa Amiri Jeshi Mkuu KIKWETE alitoboa siri ya Nyerere kumfuata Nduli Amin wa Uganda hadi chumbani kwake, kasema ilikuwa ni kwa ajili ya amani ya muda mrefu. Sembuse haka katarafa ka Rwanda kenye msongamano wa watu.
 
Sasa hii ni taaluma nyingine. Kulinda amani kwa DRC kuna hitaji kuwa na silaha na kupigana? Huku kwa DRC kuko tofauti ya kule kulinda amani kwa Sudani? Naomba anayefahamu anisaidie.

Lakini all in all, ninachokijua, kwa wingu hili, Kagame hawezi kuwa na amani na Tanzania. Kama kweli wingu liko namna hii. Kitisho chochote kwa M23 ni kitisho cha moja kwa moja kwa Kagame na serikali yake. Ili kumaliza mgogoro wa M23 nchini Kongo, UN hawana budi kudhoofisha nguvu zake ambazo ni Paul Kagame wa Rwanda.
nafikiri hawa munusco hawalindi tu amani kama ilivyo sudan, wao wamepewa na ruhusa ya kupigana kabisa kwa silaha nzito kama m23 watahatarisha maisha ya raia, that means wanawalinda raia, ndivyo nilivyokuwa nimesikia. labda kama kuna wengine wanaweza kufafanua. kuhusu comment ya rwanda, ninaunga mkono, lakini upande mwingine ninaamini Tanzania tunatakiwa kuendelea kuwa na amani na urafiki na Rwanda, m23 au congo wasitufarakanishe na Rwanda. sisi ni nchi zilizopakana, tunafanya biashara wote, kuna uhusiano wa karibu mno na hawa member wa east africa community (Rwanda) so tunahitaji kutunza uhusiano wetu na wao.
 
Watu wamepandisha mzuka hapa, utadhani Tanzania iko vitani na Rwanda!!!! Kikwete ameamua kwenda DRC, mwacheni ajaribu kufanya awezalo kuleta amani, lakini watu wasishabikie vita, utadhani mechi ya mpira! Tanzania not at war with Rwanda, period!!!!!!!!!!
Piga hao halafu mpitie kwa huyu ---- kagame mfagie mnarudi nyumbani.
 
nafikiri hawa munusco hawalindi tu amani kama ilivyo sudan, wao wamepewa na ruhusa ya kupigana kabisa kwa silaha nzito kama m23 watahatarisha maisha ya raia, that means wanawalinda raia, ndivyo nilivyokuwa nimesikia. labda kama kuna wengine wanaweza kufafanua. kuhusu comment ya rwanda, ninaunga mkono, lakini upande mwingine ninaamini Tanzania tunatakiwa kuendelea kuwa na amani na urafiki na Rwanda, m23 au congo wasitufarakanishe na Rwanda. sisi ni nchi zilizopakana, tunafanya biashara wote, kuna uhusiano wa karibu mno na hawa member wa east africa community (Rwanda) so tunahitaji kutunza uhusiano wetu na wao.

Kweli kabisa ndugu, kikosi hicho kina uwezo wa kupambana kwa ajili ya kuleta amani. Pia ni ukweli tunaitaji kukaa na majirani zetu kwa amani sana. Ndio maana hizi juhudi za amani Drc hazikuanza juzi, TZ ilijarubu sana hata Kikwete alipokuwa mwenyekiti wa AU aliwashawishi sana bila mafanikio. Haka ka Nduli Kagame kaliweka kigingi!!!!. Sasa TZ ifanyeje!, inyamaze kimya na iendelee kupokea majambazi na siraha haramu za kivita?!!.
 
Vita ni Vita! Vita ya DRC ni ngumu kulingana na historia ya Congo haya yote ni matokeo ya historia ya utawala na Uongozi wao,it needs kujua madai ya waasi na wapi wanapishana na serikali ya kabila,waasi na kabila wanayo nafasi nzuri ya kuumaliza mgogoro huu wa muda mrefu amani haitaletwa na majeshi ya kulinda amani,wasipokaa mezani wakaelewana utaondoa kundi moja la waasi litakuja lingine miaka nenda rudi.

Hawa watu siyo waasi waliozalishwa ndani ya DRC. Hawa ni waasi waliopandikizwa na kupata maelekezo yote kutoka serikali ya Rwanda kwa faida na maslahi ya watusi wa rwanda hususani kagame. NI vizuri kuwatandika hawa hawa M23 KWA vile wasipofanya hivyo watu hawa watazoea na kufanya hata vikundi vingine vya kihuni nchini DRC na kwingineko barani Afrika vipate fundisho kali.
 
Back
Top Bottom