Mwakalebela ashinda tena,Takukuru Waumbuka ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakalebela ashinda tena,Takukuru Waumbuka !

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutunga M, May 26, 2011.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Chanzo blog ya Francis Godwin,Iringa

  MAHAKAMA ya hakimu makazi mkoa wa Iringa kwa mara ya pili imemwachia huru aliyekuwa mshindi wa kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Frederick Mwakalebela na mkewe Celina baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu katika shitaka lililofunguliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa.


  Mwakalebela na mkewe walifikishwa kwa mara ya pili mahakamani hapo na Takukuru baada ya kushinda kesi hiyo kwa mara ya kwanza miezi miwili iliyopita kabla ya Takukuru mkoa wa Iringa kuifungua upya kesi hiyo ya kuwakamata kwa mara ya pili watuhumiwa hao.  Hakimu wa mahakama hiyo Mary Senapee alisema kuwa mahakama hiyo inawaachia huru watuhumiwa hao kutokana na kutokuwa na kesi ya kujibu katika shitaka hilo la rushwa lililofunguliwa na Takukuru na kuitaka Takukuru kama haijaridhika kukata rufaa.  Mwakalebela na mkewe walifikishwa mahakamani hapo na Takukuru kwa kosa la kutoa rushwa ya shilingi 100,000 kinyume na sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15(1)(b) kinachokwenda sambamba na sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka mwaka 2010 kifungu namba 21 (1) (a) na kifungu cha 24(8).  Takukuru kupitia mwendesha mashtaka wake Imani Mizizi ilidai kuwa Juni 20, mwaka jana mshitakiwa Mwakalebela alidaiwa kutoa hongo ya sh. 100,000 kwa mwenyekiti wa kijiji cha Mkoga ,Hamis Luhanga ili awagawie wajumbe wa CCM 30 ambao waliitwa kwenye kikao hicho cha kujipanga kushinda kura za maoni CCM huku akitambua wazi kufanya hivyo ni kosa .


  Hata hivyo kesi hiyo ambayo ilionyesha kuwa na mvuto zaidi kwa wakazi wa mkoa wa Iringa ambao walifika mahakamani hapo kutaka kujua hatma ya kesi hiyo ,imekuwa ni kesi ya aina yake na kupelelea ndugu kutoka kwa shangwe zaidi katika mahakama hiyo kutokana na TAKUKURU kuendelea kubwagwa mahakamani .  Mwandishi wa habari hizi alishuhudia ndugu na marafiki wa karibu wa Mwakalebela wakiondoka mahakamani hapo kwa furaha kubwa huku wakimpongeza Mwakalebela na mkewe kwa kushinda katika kesi hiyo tena.  Katika kesi hiyo Mwakalebela na mkewe Celina walikuwa wakitetewa na wakili wa Basil Mkwata ambaye aliwasilisha pingimizi la awali la kisheria ukiomba kesi hiyo iondolewe mahakamani kutokana na mapungufu ya kisheria yaliofanywa na upande wa mashitaka kabla ya Takukuru kuendelea kungÂ’angÂ’ania kuendelea na kesi hiyo ​
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Duh!
  Asee!
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Rutunga

  Sahihisha heading ya thread : BREAING NEWS.. Although hii pia ilishakuwa posted hapa JF kama NEWS!
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  no sense, Takakuru inaangaika na dagaaa ikiacha mapapa yakidunda
   
 5. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hivi alikuwa na kesi? haya ni mamichezo ya wanasiasa wanamaliza tu stationary za mahakama.
   
 6. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kulikuwa hakuna kipya kwani tangu mwanzoni alikubali kuvunja makundi na kumuunga mkono aliyepitiswa na kina Magamba. Angelikuwa alikataa, angekiona cha moto, leo angekuwa ananyea debe. Kwa ujumla ukipata jibu la Swali kwanini hakuna yeyote aliyekamatwa kwa makosa ya rushwa baada ya mchakato wa kura za maoni ccm, wakati kura zilikuwa nje nje, basi utapata jibu kuwa hizi kesi zitakuwa na maana tu ya kuwakomoa wale waliokwenda nje na ccm baada ya kuenguliwa na kukataa kuwaunga mkono.
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Ushahidi wa bongo bwana................tunayo kazi.....
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Habari ndiyo hiyo
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Acha kupoteza muda kufuatilia hizi kesi, hakuna kesi hata moja ambapo mgombea wa ccm aliyekamtwa anatoa rushwa na takukuru atayefungwa kwani hii ilikuwa set up tu ya takukuru lakini hamna lolote kwani takukuru ni taasisi yao wao ndio wanaicontrol. kesi hii ya uchaguzi ya iringa mjini mwakalebela hawezi kushinda endapo takukuru isingekubali kutumiwa kwani mwakalebela alikamatwa live na mkewe wakigawa rushwa mkutanoni na video zipo, mama sitta alikamatwa usiku wa manane akigawa rushwa tena mtego uliowekwa na takukuru wenyewe mpaka leo kimya jiulize why? na yule mama aliyekuwa mkuu wa wilaya kule moshi alikamatwa hotelini amejifungia na watu akiwagawia bahasha zenye pesa ndani lakini mpaka leo hii kimya. wahusika wote hawa rais akiwa ziarani mikoani mwao utawaona waki chat na rais. in my opinion takukuru should have been abolished longtime to save taxpayers money to be spent on failed institution like Takukuru.
   
 10. oba

  oba JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ukweli unapopita uongo hujitenga, Takukuru na ccm yao wameumbuka!
   
 11. s

  sativa saligogo Senior Member

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhhhhhm! A case of better devil you know................???????????:mod:
   
 12. s

  sitakuwafisadi Member

  #12
  May 26, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbuzi nimbuzi hawezi kuwa simba!!!!!!!
  Membe alisema, 'pesa hiyo ya FIDIA YA RADA KUTOKA( BAE )sio ya watanzania, ni ya tanzania.!!!'...........................Usually
  when people are sad they don't do anything they just CRY over their
  condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)
  .
   
 13. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mtoto kaa hapa nikirudi nitakuletea pipi, umesikia. Haya baki!
  Hizi kesi zinasikika kama uongo huo wa wazazi kwa watoto wao.
  Wazazi ni serikari inayoongoza ya magamba, na watoto ni watanzania wenye taabu na shida nyingi, wakiahidiwa kila uchao na ahadi ambazo serikari ina uhakika 100% haitazitekeleza ng'o.
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwani takukuru ni kitu gani, na inafanya nini, mbona immempeleka huyo mahakamani, hivi na yenyewe inaweza kumpakazia mtu? na yenyewe inakula rushuwa, nisaidieni wana JF.:smow:
   
 15. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  TAKUKURU inakula rushwa kama kawa. Hatua ya kuwabambikia watu kesi wakati wa uchaguzi ilikuwa ni sehemu ya rushwa ambazo TAKUKURU ilivuta ili kuwaharibia wengine na kuwaacha wengine wapete
   
 16. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kwani hiyo ilikuwa kesi? hilo lilikuwa zengwe tu amekubali yaishe magamba baana

  Pukudu@ Ilkiding'a, Arusha
   
 17. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  TAKUKURU inakula rushwa kama kawa. Hatua ya kuwabambikia watu kesi wakati wa uchaguzi ilikuwa ni sehemu ya rushwa ambazo TAKUKURU ilivuta ili kuwaharibia wengine na kuwaacha wengine wapete
   
 18. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  TAKUKURU inakula rushwa kama kawa. Hatua ya kuwabambikia watu kesi wakati wa uchaguzi ilikuwa ni sehemu ya rushwa ambazo TAKUKURU ilivuta ili kuwaharibia wengine na kuwaacha wengine wapete
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  May 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kesi ya rushwa ya uchaguzi wa kura za maoni ilikuwa set up ya ccm kwa ajili ya kupata watu wao waliowataka kushinda.
  kwenye uchaguzi mkuu uliopita rushwa zilikuwa zinatolewa hadharani lakini takukuru hawakutaka kukamata mtu yeyote.
  Mfano ilikuwa uchaguzi wa jimbo la Arusha, Batilda Buriani alikuwa anagawa fedha kwenye baa moja ... Garden, taarifa ilitolewa kwa takukuru saa 11 jioni ili wawahi pale, matokeo yake wao walifika pale saa 2 usiku, wakasema hakukuwa na dalili yoyote ya rushwa.

   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  May 26, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kazi ni Kwako
   
Loading...