Mwaka wa kwanza,Kituko cha kwanza... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka wa kwanza,Kituko cha kwanza...

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by VUTA-NKUVUTE, Oct 1, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Ni kituo cha Mabasi ya Mikoani Ubungo. Naingia kukata tiketi ya Arusha. Nimeshaipata. Sasa wakati natoka nje,nawakuta madereva wa taksi na bajaji wanawazonga vijana wawili:mmoja msichana,mmoja mvulana. Nikasogea kuona na kusikia. Walikuwa wanazongwa ili wapande kwenye ima bajaji au taksi ili wapelekwe UDSM kwakuwa ndio wamefika kama wanafunzi wa mwaka wa kwanza.

  Kwa uzalendo wangu kama mwana-UD wa zamani nikaingilia kati na kuinunua kesi. Nikawasogeza pembeni wanafunzi wale. Wakaniarifu mengi. Kubwa ni kwamba wanataka kufika UDSM. Wamebeba unga,mchele,maharage,mafuta ya kupikia na mafuta ya taa. Wa kike amebeba na sufuria na baadhi ya vyombo vya chakula. Si mchezo!

  Sasa kituko: wakaniarifu kuwa wao ni ndugu wanaotokea Bukoba. Wakasema kuwa wameambiwa nyumbani kuwa wakae chumba kimoja ili kupunguza gharama. Wahakikishe inakuwa hivyo. Ni lazima. Itawezekanaje ikiwa UDSM kuna hosteli za kike na za kiume? Mwisho mwishoni,nikawachukua garini mwangu hadi UDSM. Nimewashusha stendi ya Utawala.Nikawauliza:mnahitaji msaada wowote mwingine? Wakajibu:'hapana kaka.Hapa tumeshafika.Asante sana'. Kazi ipo...
   
 2. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Naona umekutana na kina nshomile! Haya bwana. Ukimtafuta baada ya wiki tatu atakukana kabisa kwamba hajawahi kutana nawe.
   
 3. Bee hive

  Bee hive Senior Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mi nilifikiri haya mambo kwa miaka hii yameisha, kumbe bado yapo!, kuna haja ya wageni wa maeneo mbali mbali nchini kupata taharifa ya mahala uendapo mapema, vinginevyo utaingia kwenye mitego ya matapeli.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  dah isee......

  Nimependa kuona kuna watu wachache wenye moyo kama wako, maana miaka hii mambo yalivyoharibika watu wanaogopa kusaidia mtu wasomjua
   
 5. Mzee wa kurekebisha

  Mzee wa kurekebisha Senior Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Nahisi wewe ni mtani wao, sijui watani wa wahaya ni kina nani!
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  hawa nadhani kila mtu nchi hii ni mtani wao.
   
 7. Mzee wa kurekebisha

  Mzee wa kurekebisha Senior Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Inapendeza sana, nilikuwa nawaogopa kesho nitaanza. Na wewe ni wao nini?
   
 8. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Mkuu. Saa nyingine uoga huleta madhara
   
 9. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Hapana Mkuu. Mimi ni mgoni,no Mngoni...
   
 10. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Duuuuuh! Hiyo kweli vuta nikuvute........ Wameambiwa wakae chumba kimoja....... Akili za mbayu wayu changanya na zako.... Otherwise, labda huko walikotoka walikua wanaishi chumba kimoja pia! Watakua wanamaanisha wanachotaka fanya..... Ila kwa mm waishi chumba kimoja hata km hostels wangewaruhusu haiwezi ingia akilini..... Yaani wao hawataki kbs kupigwa EXILE kbs?
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  waha, wakurya, wajaruo...............
   
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  Ulisachi mabegi yao ama?

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 13. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  KWIKWIWIWIWWWIIWI umenimekumbusha mbali.
   
 14. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  sasa ungewaambia kabisa chuoni hawaruhusu kupika.
   
 15. matwi

  matwi JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  aisee hawakua na nsenene kweli.ungewapiga picha kabisa then unaomba contacts zao baada ya mwezi unawatafuta
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hahahaaah!! Me sio mmoja wao.
   
 17. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hahahaaaaaa!
   
 18. Githeri

  Githeri JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 820
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ongezea na wakerewe, wazanaki, waikizu.....
   
 19. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Vitu vyote nilivyoviitaja vilikuwa live Mkuu...
   
 20. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wakurya
   
Loading...