Mwaka mmoja wa Rais Samia: TIC yaweka rekodi ya kusajili miradi ya uwekezaji na biashara 266

Sasa tuamini lipi. Kipindi Cha mtu yule tuliambiwa kila mkoa ulianzisha viwanda Mia. Leo hii ndani ya mwaka Kuna miradi 266.
Asking for a friend. 'hivyo viwanda na hiyo miradi iko Zambia au Tanzania hii hii, mbona havionekani',?
 
Na wewe ulimuamini yule? Kwani wewe huko mkoani kwako huoni kwamba mambo yako moto? Huoni ujenzi unavyokimbia huko kitaa?
 
Nawasalimu kwa jina la JMT.

Mama anaendelea kuweka rekodi kwenye Kila sekta.Sekta ya viwanda, biashara na uwekezaji nayo imeshuhudia mapinduzi makubwa.

Kwa mwaka mmja tuu wa mama madarakani Tanzania Investment Center TIC imeweka rekodi ya kusajili zaidi ya miradi ya uwekezaji na biashara 266.Hii haijawahi fikiwa toka JK atoke madarakani.

Ikumbukwe TIC inasajili miradi mikubwa mikubwa ya mamilioni.Hii manake ni fursa zaidi,ajira zaidi na uchumi kufunguka zaidi.

Ikumbukwe kwa miaka 6 iliyopita TIC walikuwa wanapiga miayo tuu ofisini hakuna Kazi wala uwekezaji mpya kiasi kwamba nao wakajikuta wamekuwa waimba pambio za kusifu na kuabudu.

Hii ndio maana halisi ya Kufungua uchumi. Kazi iendelee 👇

------
WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, amesema miradi 266 imesajiliwa katika Kituo cha Uwekezaji (TIC) kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema hayo jana wakati wa hafla ya kukabidhi kiwanja namba moja kitalu B eneo la Kwala, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa mwekezaji wa kampuni ya Sino Tan (Kibaha Industrial Park Ltd) kwa ajili ya Kongani ya viwanda.

Akizungumzia mradi huo mkubwa wa kimkakati kwa Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara, alimpongeza Rais kwa kuhakikisha Tanzania inakuwa eneo salama la uwekezaji na mahali pa kuvutia wageni.

Alisema mradi huo ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne, utaanza kwa miaka miwili ya awali na mingine baadaye na ujenzi wake unatarajia kugharimu zaidi ya Dola za Kimarekani 150 ambazo zitawekezwa katika upatikanaji wa ardhi, miundombinu, ujenzi wa viwanda na vifaa vinavyohitajika.

Alisema manufaa ya uwekezaji wa mradi huo ni uhakika wa soko la malighafi, mikataba iliyosainiwa na kampuni ya Sino Tan inayomilikiwa na wawekezaji kutoka China ni mwanzo wa mradi mkubwa utakaoleta manufaa mapana kwa taifa kwa kuwa viwanda vya kuchakata mazao vitajengwa na Watanzania watanufaika na soko.

Manufaa mengine ni ajira za moja kwa moja 100,000, pia wananchi wanatakiwa kutumia fursa ya kujifunza lugha ya Kichina na Watanzania wanatakiwa kutumia fursa hiyo ili wapate kuwa wakarimani ndani na nje ya Tanzania.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Prof. Godius Kayarara, alisema upatikanaji wa ardhi ni jambo kubwa kuliko kitu chochote ndiyo maana sheria zinabadilishwa ili ardhi ipatikane haraka na mradi ufanyike kwa haraka.

Alisema mradi huo utakuwa na viwanda 200 vya kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwamo pikipiki.

Mwakilishi wa Sino Tan Kibaha Jansen Huang, alisema mradi ukikamilika watahitaji huduma ya polisi kwa ajili ya usalama na baadhi ya nchi zenye miradi yake ya uwekezaji ni Nigeria, Ethiopia na Uganda na wana marafiki wengi na kuitaja Tanzania kuwa na sera nzuri kuhusu uwekezaji.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, alisema wanamshukuru Rais kwa kufanya jitihada za kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini na kwenye mkoa kwa kutafuta wawekezaji na kuboresha maisha.

Kunenge alisema mkoa una viwanda 1,453 vikiwamo vikubwa 87.

Chanzo: Nipashe
🤔
 
Namba hazidanganyi👇

Screenshot_20220512-130134.png

Screenshot_20220513-104418.png

Screenshot_20220513-104556.png

Screenshot_20220513-104822.png
 
Endelea kusubiria kuonyeshwa fursa
Kama wewe unavyoendelea kuambiwa na TIC figures wakati mtaani hakuna kinachoonekana 😁😁 wanasiasa waacheni, kujifagilia ndo zao ndo maana unaona Shaka anawahimiza wakuu wa wilaya na mikoa watoe promo kwa maza. 😂
 
Endelea kusubiria kukiona mtaani

20220423_125737.jpg
 
Sasa tuamini lipi. Kipindi Cha mtu yule tuliambiwa kila mkoa ulianzisha viwanda Mia. Leo hii ndani ya mwaka Kuna miradi 266.
Asking for a friend. 'hivyo viwanda na hiyo miradi iko Zambia au Tanzania hii hii, mbona havionekani',?
Si Waziri alisema wakati ule hata ukiwa na Charahani 2 ni kiwanda na wewe ni Mwekezaji
 
Endelea kusubiria kukiona mtaani

View attachment 2227914
Mazungumzo na wezi. 😁😁 kwani watanzania hawana hizo hela za kuweka viwanda vikubwa vya sukari, mafuta n.k? Ni kujipendekeza tu hata kwa vitu wanavyoviweza watanzania, kaa na matajiri wa kitanzania waambie changamoto za bidhaa tunazoziagiza nje kwa wingi wao wazalishe ili watanzania tuneemeke zaidi kabla ya kuita hao. Hao waje kwenye vtu ambavyo watanzania hawawez 😁😁
 
Na wewe kaibe..Kazi inaendelea 👇

Screenshot_20220517-123025.png

Screenshot_20220517-123113.png
 
Back
Top Bottom