EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,091
Wiki moja tu iliyopita wengi wetu tulikuwa tunaamini uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na landslide victory kwa CCM hasa kwenye nafasi ya Urais
Nachelea kusema hata Rais Magufuli mwenyewe aliamini atashinda kwa kishindo. Lakini tangu Tundu Lissu amerudi, mapokezi aliyoyapata mpaka kwenye tukio la kupitishwa kuwa mgombea Urais kupitia chama chake cha CHADEMA hali ya hewa imebadilika kabisa.
Nimeanza kuona kuanzia mtaani mpaka humu kwenye social media mitizamo imebadilika na kuona sasa uchaguzi sio rahisi tena kama ilivyodhaniwa
Baada ya hotuba ya kukubali kupeperusha bendera ya chama chake, Lissu aliongea mambo ambayo yametengeneza ajenda ambazo kwa kiasi kikubwa zimewashtua pia viongozi wa CCM. Hata ukiangalia press ya leo ya Polepole kuna dalili za kupanic ambazo zimefanya asiwe na ajenda maalum zaidi ya kuruka huku na huku.
Siasa ni mchezo usiotabirika na tukio moja linaweza kubadili mustakabali mzima wa muelekeo.
Na tusubiri tuone.