Joshua justine
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 792
- 1,007
Je, watanzania tuna msimamo gani na mtazamo gani juu ya chama tawala?
Tunatarajia nini kwa hali iliyopo kuhusu uhalali wa chama hiki kuendelea kuongoza taifa letu?
Mwalimu Nyerere mwaka 1962 aliacha uongozi wa serikali kwa msaidizi wake (Kawawa), akajitoa serikalini na kubaki chamani tu ili afanye kazi ya kukiimarisha chama cha TANU, ha alifanya hivyo kwa sababu alisema serikali imara inatokana na chama imara, baada ya kuifanya kazi hiyo alirudi tena kupokea madaraka yake serikalini na kuendelea kuliongoza taifa, hii ndio ishara ya kweli ya mtu mzalendo wa kweli kwa taifa lake.
Je, leo chama cha mapinduzi kina uhalali kiasi gani wa kuendelea kuiongoza serikali katika hali ya mvurugano wake unaoongezeka kila kukicha, je tufuate maneno ya baba wa taifa kuwa chama dhaifu huleta serikali dhaifu?
Je, muda uliopo utakitosha chama hiki kurudisha uhalali wake mwaka 2022 kwa kujiimarisha ndani kwa ndani ama kitakutana na anguko lake jingine.