Mwaka 2022 ni uchaguzi wa ndani wa CCM

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
792
1,007
Je, watanzania tuna msimamo gani na mtazamo gani juu ya chama tawala?

Tunatarajia nini kwa hali iliyopo kuhusu uhalali wa chama hiki kuendelea kuongoza taifa letu?

Mwalimu Nyerere mwaka 1962 aliacha uongozi wa serikali kwa msaidizi wake (Kawawa), akajitoa serikalini na kubaki chamani tu ili afanye kazi ya kukiimarisha chama cha TANU, ha alifanya hivyo kwa sababu alisema serikali imara inatokana na chama imara, baada ya kuifanya kazi hiyo alirudi tena kupokea madaraka yake serikalini na kuendelea kuliongoza taifa, hii ndio ishara ya kweli ya mtu mzalendo wa kweli kwa taifa lake.

Je, leo chama cha mapinduzi kina uhalali kiasi gani wa kuendelea kuiongoza serikali katika hali ya mvurugano wake unaoongezeka kila kukicha, je tufuate maneno ya baba wa taifa kuwa chama dhaifu huleta serikali dhaifu?

Je, muda uliopo utakitosha chama hiki kurudisha uhalali wake mwaka 2022 kwa kujiimarisha ndani kwa ndani ama kitakutana na anguko lake jingine.
 
Kabla ya kuamua nani ashike madaraka CCM au Chama chochote cha upinzani tunataka katiba mpya kwanza.

Hatuna shida na CCM, wala CDM, ACT au CUF kushika madaraka ya nchi.

Tunahitaji katiba mpya ili tuweze kumwajibisha atakayekuwa amepewa mamlaka ya kuongoza pindi anapoenda kinyume na matakwa ya wananchi kama muongozo wa katiba yao ulivyo.
 
Kabla ya kuamua nani ashike madaraka CCM au Chama chochote cha upinzani tunataka katiba mpya kwanza.

Hatuna shida na CCM, wala CDM, ACT au CUF kushika madaraka ya nchi,

Tunahitaji katiba mpya ili tuweze kumwajibisha atakayekuwa amepewa mamlaka ya kuongoza pindi anapoenda kinyume na matakwa ya wananchi kama muongozo wa katiba yao ulivyo.
Ugumu unakuja kuwa pale tunapolitamka jambo la katiba mpya bado wanaotuwakilisha ndio wanaotusemea juu ya jambo hilo pia, nao ni CCM karibia wote.

Naona bila ya kuanza na chama kwanza hakutakuwa na katiba mpya wala ukombozi mwingine wowote tunaoutarajia kama wananchi.
 
Ugumu unakuja kuwa pale tunapolitamka jambo la katiba mpya bado wanaotuwakilisha ndio wanaotusemea juu ya jambo hilo pia, nao ni ccm karibia wote.

Na bila katiba mpya huwezi kuanza na CCM kwanza!!

Katiba mpya ndo kila kitu kwa sasa hv, usitegemee chochote bila hivyo, labda kuwe vuguvugu la kuwaondoa madarakani kwa nguvu!!
 
Ugumu unakuja kuwa pale tunapolitamka jambo la katiba mpya bado wanaotuwakilisha ndio wanaotusemea juu ya jambo hilo pia, nao ni ccm karibia wote.
Naona bila ya kuanza na chama kwanza hakutakuwa na katiba mpya wala ukombozi mwingine wowote tunaoutarajia kama wananchi.
Mkuu tukiziweka itikadi zetu ya kivyama tukashikana pamoja kwenye mapambano ya kudai KATIBA MPYA, tutafanikiwa. Hawana uwezo wakutuzuia. Wanachokifanya hivi sasa ni Ku attack individual.
 
Nakubaliana na ww kwa hili, tukifanikiwa kupata mass awareness, basi the rest itakuwa ni history.
 
Hii nchi inahtaj mabadiliko ya kifikra
Je, watanzania tuna msimamo gani na mtazamo gani juu ya chama tawala?

Tunatarajia nini kwa hali iliyopo kuhusu uhalali wa chama hiki kuendelea kuongoza taifa letu?

Mwalimu Nyerere mwaka 1962 aliacha uongozi wa serikali kwa msaidizi wake (Kawawa), akajitoa serikalini na kubaki chamani tu ili afanye kazi ya kukiimarisha chama cha TANU, ha alifanya hivyo kwa sababu alisema serikali imara inatokana na chama imara, baada ya kuifanya kazi hiyo alirudi tena kupokea madaraka yake serikalini na kuendelea kuliongoza taifa, hii ndio ishara ya kweli ya mtu mzalendo wa kweli kwa taifa lake.

Je, leo chama cha mapinduzi kina uhalali kiasi gani wa kuendelea kuiongoza serikali katika hali ya mvurugano wake unaoongezeka kila kukicha, je tufuate maneno ya baba wa taifa kuwa chama dhaifu huleta serikali dhaifu?

Je, muda uliopo utakitosha chama hiki kurudisha uhalali wake mwaka 2022 kwa kujiimarisha ndani kwa ndani ama kitakutana na anguko lake jingine.
 
Pengine kweli CCM imechoka kukaa madarakani, au labda viongozi wake wamejisahau, lakini embu tafakari, kwa hali ya sasa ya siasa nchini, ni chama gani kinaweza kuchukua nafasi ya kuongoza dola? Hii nchi ina vyama ambavyo hata baraza la mawaziri haviwezi kuunda kwanza havina wananchama wa kutosha pia, wachache waliopo hawana uwezo wa kusimama kwenye nafasi hizo. Hivyo badala ya kukesha kuikosoa CCM, pengine nguvu zielekezwe kwenye kujenga mbadala wa CCM
 
CCM
FB_IMG_15805053448797833.jpg
 
Tunaomba vigezo ulivyotumia kutambua hakuna chama kinaweza kuongoza dola isipokuwa CCM.

Pia tunaomba vigezo ulivyotumia kutambua vyama visivyoweza kuunda baraza la mawaziri, uchache wa wanachama, na kukosa kwao uwezo wa kusimama kwenye nafasi za uongozi.

Nakusubiri!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom