KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu kwa Rais, wabunge na madiwani. Ni mwaka ambao watanzania wataweka historia juu ya nchi na watanzania watashuhudia mambo yafuatayo: 1) upinzani utapoteza ushawishi kwa wapigakura na kupoteza 80% ya nafasi zao za kiuongozi (2) mgombea urais kwa tiketi ya CCM atapata ushindi wa kihistoria wa kishindo (3) wagombea/mgombea urais wa upinzani kupata aibu ya kihistoria ya kushindwa.
Haya ni majumuisho ya jumla na mtazamo wangu
Tanzania ni yetu sote, tuinjenge pamoja kwa ajili yetu na vizazi vyetu kwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi ya kuchagua na kuamua wa kutuongoza. Binafsi kwa kuona umuhimu wa Tanzania katika kuiletea Tanzania maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kukuza uwekezaji na jaasiriamali, NASIMAMA NA RAIS WANGU NA CCM.
Haya ni majumuisho ya jumla na mtazamo wangu
- Watanzania wanaona umuhimu wa kuwa na rais mzalendo na mwenye kujali masilahi ya umma wa wale anaowaongoza. Na Rais Magufuli ameshakaa akilini na mioyoni mwa watanzania kwa sifa njema ya uzalendo. Watanzania wanahitaji kuwa na kiongozi kama yeye( kama akiamua kupumzika) na hivyo kufanya maamuzi ya kumchagua tena kwa kishindo kikubwa au kumchagua mgombea mwingine wa kutoka CCM. Watanzania wanahitaji kuuenzi uzalendo wa Rais na kuwa pamoja naye kwa kumpigia kura kwa wingi sana. Mzalendo anazawadiwa zawadi ya kura tu.
- CCM itaungwa mkono na watanzania wengi sana na kupelekea kuwachagua wabunge wengi wa CCM na 80% ya wabunge na madiwani wa sasa wa upinzani kupoteza ushawishi majimboni na kupoteza nafasi zao na nafasi zao kuchukuliwa na CCM. Ushahidi ni kupitia chaguzi ndogo za marudio ambapo CCM iliibuka kidedea kwa kura nyingi sana na kishindo hata kwa majimbo yaliyokuwa chini ya upinzani
- Watanzania wameuchoka upinzani na hata sasa wanatamani kufanya maamuzi majimboni na kwenye kata ambayo hawakufanya 2015. Wengi wanajutia ,wananung’unika na kusikitika kushindwa kufanya maamuzi 2015 na wanatamani hata muda huu ungetumika kufanya marekebisho wa yale waliyokosea kipindi. Hii ni dalili mbaya kwa upinzani
- Vijana wengi kuingia kwenye siasa na kupata fursa ndani ya CCM ya kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa nchini yamekuwa ni mafanikio makubwa kwa CCM kuwa na mwanzo mzuri wa kuelekea kupata ushindi mnono wa kihistoria. Vijana ni jeshi la ushindi la CCM litakaloichinja upinzani
- ‘Ajira ni bomu linalosubiri kulipuka’, sasa halitalipuka tena kwa kuwa limeteguliwa na mteguaji makini rais Magufuli. Maelfu kwa maelfu wanaopata ajira katika sekta iliyo rasmi na isiyo rasmi watapata kuichagua CCM kwa wingi kwa mategemeo na matarajio kuwa sera ya Tanzania ya viwanda chini ya CCM ni mkombozi wao wa ajira na kujiajiri katika sekta isiyo rasmi na ile rasmi.
Tanzania ni yetu sote, tuinjenge pamoja kwa ajili yetu na vizazi vyetu kwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi ya kuchagua na kuamua wa kutuongoza. Binafsi kwa kuona umuhimu wa Tanzania katika kuiletea Tanzania maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kukuza uwekezaji na jaasiriamali, NASIMAMA NA RAIS WANGU NA CCM.