Mwajiri muzuia wafanyakazi kuingia na mabegi ya mgongoni kazini

Mar 29, 2015
95
41
Kwa heshima na taadhima msaada misheria hii ipoje? Sababu kila abebae begi mgongoni anakuwa na Sababu zake binafsi. Eidha ziwe nzuri ama mbaya. Je, kisheria mwajiri anamamlaka ya kuzuia mabegi?

Natanguliza shukrani.
 
anayo mamlaka .....kazini unaenda na mabegi ya nini kwani hapo ofcini ni chuoni au kituo cha usafiri......
 
Mimi napewaga laptop na bag lake, kwahiyo nilikuwa naenda na bag lao vitu vyangu vyote naweka humo. Ila wengi hawazuii labda akuhisi kwamba unaweza chomoa cable ukatia mfukoni, au ukachukua chochote ukatia kwa ki bag. Kuna kampuni zingine huingii na ki bag mfano kiwanda cha nguo cha 21 Centure Textiles moro, wao bag zako anaziacha kwa askari getini ukimaliza mda wa kazi wakati wa kutoka unachukua...maana wanahisi usije ukachukua kitenge ukatia kwenye bag lako. Wengi hapo awali walikuwa wanafanya hivyo...kwahiyo utazoe tu kwenda bila bag
 
hapo kuna dalili za udokozi ndo maana ameonelea kuzuia mabegi kuingianayo kazini...
 
Asanteni sana wakuu. Kila mtu ana haki ya kutoa mchango wake kutokana na kikomo chake kiuwelewa. Nikipata msaada kisheria ambayo inatoa mamlaka ya moja kwa moja nadhani tutajifunza wengi zaidi.

Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom