Mwajiri hajatoa mishahara 5 months now

Mwajiri hajatoa mishahara 5 months now

leyb

Senior Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
111
Reaction score
64
Ndugu ninafanya kazi ofisi moja hivi ninamiezi mitano sijapata mishahara Yangu kisa anasema sales sio nzuri huku naonaa yeye anaimarisha miradi yake mingine. mpaka sasa nadai kiadi cha 9milions. please naomba ushauri njia zipi za kisheria ili nipate hiki kipato changu?
 
kama hujatimiza targets zako kweli ana haki ya kutokukulipa lakin pia inategemea na mkataba wenu ulikuaje
 
Ndugu ninafanya kazi ofisi moja hivi ninamiezi mitano sijapata mishahara Yangu kisa anasema sales sio nzuri huku naonaa yeye anaimarisha miradi yake mingine. mpaka sasa nadai kiadi cha 9milions. please naomba ushauri njia zipi za kisheria ili nipate hiki kipato changu?

9 mil ina maana alitakiwa akulipe 1.8 mil @ month?
:confused2::confused2::confused2::confused2:.... sounds like not realistic!
 
Ww fisadi unaishije miezi 5 bila salar?-joking... Mbane akupe chako upite vile
 
hapa nahitaji kujua sheria inasemaje ili nianze kupambana naye
 
Ndugu ninafanya kazi ofisi moja hivi ninamiezi mitano sijapata mishahara Yangu kisa anasema sales sio nzuri huku naonaa yeye anaimarisha miradi yake mingine. mpaka sasa nadai kiadi cha 9milions. please naomba ushauri njia zipi za kisheria ili nipate hiki kipato changu?

Wew utakuwa kibarua
 
Kuwa na Amani, Kisheria hawezi kukudhulumu, Kama uli devote muda wako na kazi ulifanya hawezi kukuibua hela yako. Nenda Mahakama ya Wilaya ndipo Jurisdiction ya hela yako inapoangukia halafu omba kufungua Shauri la madai, katika Shauri hilo wewe ndo utakuwa Mdai na hiyo Kampuni au Ofisi unayoifanyia ndio watakuwa Wadaiwa na siyo Boss wako, Mwisho wa Shauri Mahakama itatoa hukumu baada ya kusikiliza pande zote mbili na kuridhika na haki yako utaipata. Naomba tu Mungu uwe una Mkataba wa kazi kati yako na Mwajiri wako(Office). Kila la kheri. Lakini kabla hujafanya hivyo jaribu kumuuliza Boss wako physically na ukumbuke hicho kitendo cha kwenda Mahakamani kinaweza kika cost your possition kwenye hiyo office so kuwa na uhakika before ya kuanza chochote.
 
kisheria ndugu yangu unapaswa kwenda ofisi ya kazi mkoa na wao watamuandikia huyo muajiri wako amri ya kumhitaji aje ofisini kwao ili ahojiwe kuhusu kutolipa kwake mshahara. kuhusu kuwa na mkataba halali wa kazi siyo jukumu la muajiriwa kwani anayepaswa kuthibitisha juu ya mahusuiano yote ya kazi baina ya muajiri na muajiriwa ni muajiri na wala siyo muajiriwa, hivyo nenda idara ya kazi na maafisa kazi wa eneo husika watakupatia msaada ili kuweza ktatua suala lako hii ni kwa mujibu wa Sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 ikisomwa pamoja na kanuni zake.
 
Back
Top Bottom