Mchochezi
JF-Expert Member
- Feb 29, 2012
- 10,416
- 6,578
Jamani,
Kadri ninavyofahamu mimi kuhusu historia ya Tanzania, ambayo sisi vijana wengi siku hizi tunaipuuuza, MWAISELA na SEWA HAJI, walikuwa ni madaktari bingwa wa mwanzo wenye asili ya Kiafrika nchini mwetu. Hospitali ya kwanza kubwa katika Tanzania, ilikuwa inaitwa kwa jina la Sewa Haji, ambayo ilikuwepo kabla ya uhuru katika eneo kati ya Kituo cha sasa cha Kati cha Polisi na Ofisi ya Kituo Kikuu cha Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam. Baadaye wakati uhuru unapatikana, Sewa Haji, ikahamishiwa pale ambako sasa ni Muhimbili, lakini wakati huo ilikuwa inajulikana kuwa Princes Margaret Hospital, kwa heshima ya Malkia wa Uingereza wakati huo. Ndiyo maana Wodi moja muhimu Muhimbili, inaitwa Sewa Haji. Hospitali nyingine kubwa ni ile ambayo sasa ni Ocean Road, lakini ilikuwa inaitwa European Hospital, kwa ajili ya Wazungu tu!
TAMBAZA, alikuwa kiongozi wa Kizaramo, aliyeitwa Jumbe Tambaza. Jumbe kilikuwa ni cheo ambacho baadhi ya Waafrika walipewa tangu utawala wa Kijerumani nchini. Yeye ndiye aliyekuwa anamiliki eneo lote la kuanzia Ikulu hadi Muhimbili (Upanga Mashariki na Magharibi). Ndiyo maana shule ya H.H. The Agakhan iliyokuwa inamilikiwa na Waislamu wa Dhehebu la Ismailia, ikataifishwa na kuitwa jina la Tambaza. Jumbe Tambaza aliyagawa maeneo hayo bure kwa ajili ya maendeleo na hakuwa na uchoyo na uroho ulioletwa na Wazungu wa kuhodhi na kulangua ardhi! Yeye mwenyewe akabaki na kieneo kidogo kwenye msikiti uliopo Barabara ya Umoja wa Mataifa na eneo ambalo sasa linatumika kuvizika vitoto vichanga vilivyofia Muhimbili!
KIBASILA ni Chifu wa Kizaramo, ambaye alinyongwa na Wajerumani kutokana na msimamo wake wa kukaidi kutawaliwa na Wazungu hao! Alinyongwa kwa kamba kwenye mti wa mwembe katika eneo ambalo sasa kinajengwa Kituo cha Mabasi yaendayo kasi, (Kamata, karibu na duka kubwa la Shoprite, barabara ya Nyerere). Tusisahau historia hii muhimu! Kwa kuisahau ndiyo maana hatujiamini na sasa tunatawaliwa tena kiuchumi na hawa Wazungu!
Bwassa
interesting....