Mwaisela, Tambaza, Sewa Haji et al...ni kina nani hawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaisela, Tambaza, Sewa Haji et al...ni kina nani hawa?

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Idimi, Nov 23, 2009.

 1. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Ndugu wanajamvi, katika pita pita yangu nimekutana na majina fulani fulani maarufu ambayo taasisi mbalimbali zimepewa, ambayo kusema kweli sijajua asili ya majina hayo, na nahisi huenda ni ya watu fulani waliokuwa maarufu sana ama viongozi, kama ilivyo kwa Mandela road ama Sam Nujoma road.
  Mfano, ukifika katika hospitali ya taifa pale Muhimbili (MNH) kuna majina kama Mwaisela, Sewa Haji, Kibasila n.k. Hali kadhalika jina la Mwaisela ni jina la bweni katika shule ya Sekondari moja iliyo wilaya ya Mufindi kule Iringa, ambapo pia kuna bweni la Mkwawa katika shule hiyo hiyo. Jina la Tambaza sijajua linatokana na asili gani pia.
  Naomba kuelimishwa asili ya majina haya na mengine mengi pia.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180

  Mkuu nimejaribu kutafuta scanty info za hawa jamaa:
  SEWA HAJI SCHOOL / MWAMBAO SCHOOL
  In 1896 Sewa Haji, an influential businessman, built this three storey interracial school in the heart of Bagamoyo. The school is one of the many social facilities provided by Sewa Haji in the late 1800. The building was expanded in three different stages, and the entrance was moved to the opposite side but the use of the building has not changed since the start. Today parts of the building are not in use because of the poor condition.

  Sewa Haji also built a hospital in the new Govement town south of Bagamoyo,now Dar es salaam.The Hospital however was demolished due to dilapidation.
  The famous Proffessor Koch(discoverer of the TB vaccine) made a point of visiting Sewa Haji in Dar es salaam in 1897 but found out that he had died a short while earlier.
  Tambaza

  Sheikh Jumbe Tambaza , alikuwa mmoja wa wazee maarufu sana jijini Dar es salaam kabla ya Uhuru.
  Kati ya wazee hao ni Aziz Dossa ,Kleist Sykes na wazee wengine ambao walimkaribisha Nyerere Dar es salaam kutoka Pugu alikokuwa mwalimu.
  Sheikh Tambaza anakumbukwa sana kutoka miaka ya 1950's na jina lake lina enziwa kwa Msikiti wa Tambaza pale Upanga na vilevile Shule ya Sekondari Tambaza.

  Mwaisela....naendelea kutafuta mkuu!!!!!
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwaisela tulishamjadili humu kwenye mada ya Tukumbuke Historia yetu. Huyo alikuwa Daktari Mwanaharakati. Pata dondoo hii kutoka kwenye Tasnifu ya Mwanasosholojia:

  As late as 1940s people like Dr. E.F. Mwaisela, when petitioning about the incommensurable remuneration they received, based their arguments on the education status and the life situation expected form them. As a Medial Officer Mwaisela wrote in 1943:

  The general outlook at present as far as my life is concerned, is very gloomy. I have been brought up to such a level in life that I can neither cope with my own people's life, nor that of a civilized man. To get married to a girl of any reasonable standard, for instance, in order that I should maintain that standard of education I enjoyed at school, is literally to commit suicide.

  This frustration, eloquently put by Dr. Mwaisela was part of the issues which fuelled the transition of the assimilated form the position of the co opted to that of rebellion from the 1930s.

  A letter by Dr. E.F. Mwaisela in Mss Brit Emp s. 365, "Papers of the Fabian Colonial Bureau".
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Na Muhimbili ilitokana na nini/nani??
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Na Kibasila je alikuwa nani?

  Nasikia somo la Historia lilifutwa na Waziri Mungai miaka hiyo na vijana wetu wa siku hizi watakuwa na maswali mengi sana ya aina hii.
   
 6. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Sikupata kuona thread hiyo iliyomhusu Mwaisela, hata hivyo nitafurahi sana ukiweka link hapa mahali ili wengi tuelimike. Nitashukuru sana!

  Sure, hata mie nahitaji kujua.

  NB
  Nashukuru sana kwa elimu hii, tafadhali endeleeni kuchimbua na historia ya wanamapinduzi wengine pia kwa faida ya wanajamvi wote. Naamini sio mie pekee ambaye nilikuwa siwajui watu hawa.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..nafikiri eneo ilipojengwa shule, makaburi, mpaka pale kwenye msikiti, ilikuwa ni ardhi ya Mzee Tambaza.
   
 8. s

  shabanimzungu Senior Member

  #8
  Nov 23, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thanks goodness SEWA HAJI AN INDIAN BUSINESSMAN built Muhimbili otherwise we would not even have had that one aswelllllllllllllllllllllllllllll!
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kibasila alikuwa Pazi (chifu) wa Wazaramo maeneo ya Magogoni/Mzizima (kama kuna watu wanaoijua hiyo sehemu). Maeneo ya siku hizi ni Wizara ya Utumishi na Ardhi.
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kina tambaza ndio sie hao
   
 11. C

  Chechenya Member

  #11
  Nov 24, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naomba niweke sawa hapa Bweni la Mwaisela na Mkwawa yapo katika Shule ya sekondari Rungwe mkoani Mbeya na siyo Mufindi.
   
 12. B

  Bwassa Member

  #12
  Nov 24, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Jamani,

  Kadri ninavyofahamu mimi kuhusu historia ya Tanzania, ambayo sisi vijana wengi siku hizi tunaipuuuza, MWAISELA na SEWA HAJI, walikuwa ni madaktari bingwa wa mwanzo wenye asili ya Kiafrika nchini mwetu. Hospitali ya kwanza kubwa katika Tanzania, ilikuwa inaitwa kwa jina la “Sewa Haji”, ambayo ilikuwepo kabla ya uhuru katika eneo kati ya Kituo cha sasa cha Kati cha Polisi na Ofisi ya Kituo Kikuu cha Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam. Baadaye wakati uhuru unapatikana, Sewa Haji, ikahamishiwa pale ambako sasa ni Muhimbili, lakini wakati huo ilikuwa inajulikana kuwa “Princes Margaret Hospital”, kwa heshima ya Malkia wa Uingereza wakati huo. Ndiyo maana Wodi moja muhimu Muhimbili, inaitwa “Sewa Haji”. Hospitali nyingine kubwa ni ile ambayo sasa ni Ocean Road, lakini ilikuwa inaitwa “European Hospital”, kwa ajili ya Wazungu tu!

  TAMBAZA, alikuwa kiongozi wa Kizaramo, aliyeitwa Jumbe Tambaza. Jumbe kilikuwa ni cheo ambacho baadhi ya Waafrika walipewa tangu utawala wa Kijerumani nchini. Yeye ndiye aliyekuwa anamiliki eneo lote la kuanzia Ikulu hadi Muhimbili (Upanga Mashariki na Magharibi). Ndiyo maana shule ya “H.H. The Agakhan” iliyokuwa inamilikiwa na Waislamu wa Dhehebu la Ismailia, ikataifishwa na kuitwa jina la Tambaza. Jumbe Tambaza aliyagawa maeneo hayo bure kwa ajili ya maendeleo na hakuwa na uchoyo na uroho ulioletwa na Wazungu wa kuhodhi na kulangua ardhi! Yeye mwenyewe akabaki na kieneo kidogo kwenye msikiti uliopo Barabara ya Umoja wa Mataifa na eneo ambalo sasa linatumika kuvizika vitoto vichanga vilivyofia Muhimbili!

  KIBASILA ni Chifu wa Kizaramo, ambaye alinyongwa na Wajerumani kutokana na msimamo wake wa kukaidi kutawaliwa na Wazungu hao! Alinyongwa kwa kamba kwenye mti wa mwembe katika eneo ambalo sasa kinajengwa Kituo cha Mabasi yaendayo kasi, (Kamata, karibu na duka kubwa la Shoprite, barabara ya Nyerere). Tusisahau historia hii muhimu! Kwa kuisahau ndiyo maana hatujiamini na sasa tunatawaliwa tena kiuchumi na hawa Wazungu!

  Bwassa
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280

  Sawa, rekodi zako ni sahihi kwa sababu umesoma Rungwe. Na zangu ni sahihi pia kwa sababu nimesoma Malangali Sekondari, mkoa wa Iringa ambako kuna mabweni yenye majina hayo.
  Mambweni yenye majina hayo yapo pia katika shule ya sekondari ya Malangali, iliyo katika kata ya Malangali, wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa. Kwa hiyo hawa celebrities wamekuwa maarufu maeneo yote hayo! Muulize Mwaipopo aliyesoma Malangali, alikuwa analala bweni la Mwaisela! Tupo pamoja hapo?
   
 14. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  naongeza, mzumbe nao wana bweni/kijiji kwa jina la Mkwawa kadhalika Ilboru
   
 15. Companero

  Companero Platinum Member

  #15
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nasikia Malangali naye alikuwa mtu maarufu katika Historia yetu, mwageni data tafadhali!
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du Kiongozi unatisha,
  Naona kumbukumbu zako ziko bado mswano, unakumbuka who was sleeping where hadi leo?
   
 17. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280

  Sure man, mambo ya boarding hayo!
  Huyu jamaa ni best yangu sana na alilala bweni la Mwaisela, mie nilikuwa nalala bweni la Mkwawa. Pia shuleni hapo kuna bweni la Shaaban Robert ambalo amewahi kulala kocha maarufu wa kabumbu Tanzania, Bw. Syllersaid Mziray! Naye alisoma hapo na alikuja kututembelea na kuleta mipira kibao!
   
 18. Companero

  Companero Platinum Member

  #18
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Enhe Mtikila na wale maprofesa wa Sosholojia walilala bweni gani hapo Malangali?
   
 19. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  naomba niongeze hapo kwenye bold, Aziz Dossa au Aziz Ally Dosa kwa kirefu ndiye ambaye jina lake linatumika kule mtoni kwa Aziz Ally. huyu pia ni baba wa Hamza Aziz, IGP wa kwanza wa Tanganyika huru. mzee Hamza Aziz amefariki miaka michache iliyopita.
   
 20. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Tokomile lini?
   
Loading...