Mwafrika na mafanikio (pesa)

Mwafrika na mafanikio (pesa)

Konda wa bodaboda

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
7,981
Reaction score
4,174
Wanajukwaa,

Najaribu kuelezea maisha yetu kama waafrika japo sitaonesha mpangilio mzuri lakini kwa kutumia akili ya kawaida tu unaweza kuelewa nini nimesema.

Hapa nawasilisha kwa namna ya kuuliza kwanini labda wengine mmewahi kujiuliza kama mimi. Nimetumia neno waafrika katika wingi wao ila sisemi ni wote.

Kwanini mtu mweusi akiona pesa akili yake inageuka na kufikiri kinyume. Nimefanya uchunguzi binafsi na kubaini kuwa pesa na mtu mweusi ni paka na panya kwa maana ya kwamba ukiviweka pamoja lazima matokeo yatakuwa hasi.

Kwa mwafrika pesa ndio inatumika kujenga na kubomoa marafiki, ukiwa ma pesa watu watakufuata-fuata na kuonesha kukuheshimu na ukiwa huna watakukimbia na kukudharau.

Kwa mwafrika pesa inamfanya ajitenge na jamii yake aliyoishi hapo kabla na kuachana hata na watu aliokuwa nao mwanzo, ataishi maisha ya kipekee na kwa upande wa pili ataonekana mtu mpya na mwenye heshima kwa watu wengine.

Mwafrika akifanikiwa kupata elimu ya juu anawadharau aliowazidi.Mwafrika akiwa na pesa hata baiskeli haendeshi kwa kuamini kuwa ni usafiri wa watu wa chini/maskini.

Mwafrika akipata pesa anakuwa mnafiki, anaweza kuvaa hata kujiweka local tu ili watu wamuone yuko sawa na wao ila anafanya hivi akijua sio kwa dhati (hapa wanasaikolojia mnaweza kufafanua)

Anaweza kufagia hata barabara ya mtaa, kuchimba mtaro wa maji wakati hapo kabla alikuwa anaona aibu atachekwa!(hapa hata mitazamo ya wanaomtazama inabadilika, kwanini?)

Mwafrika anaweza kumsitiri raia wa kigeni bila kunung'unika ila sio kwa mtu mweusi mwenzake. Mwafrika akiwa na pesa atajenga jumba kuubwa na kuweka vioo hata kama yupo dar(joto) kwanini?

Mwafrika akiwa na pesa atatumia gari kwenda kila sehemu anayotaka hata kama ni mita mia moja kutoka alipo.Hayo juu ni maisha halisi ya waafrika wanaonyanyuka kutoka chini hadi juu.

Linganisha hayo yote na maisha ya wazungu, wachina,waarab,wahindi,wakorea,.nk kwa kuangalia uhusiano wao kwa wao halafu uone tofauti.

Wakati mwingine nawaza kuwa kama sio raia wa kigeni kutembea milimani,mbugani na sehemu nyingine za kutalii mwafrika asingethubutu kufanya hivyo maana angeona ni kupoteza muda na kujitesa tu.

Ila kwa kuwa wazungu wanayafanya hayo nao wanaona ni ujanja.Hata kupanda farasi tusingepanda kwa kudhani kuwa kupanda wanyama ni uzamani.
 
All applies....hii kasumba sio kwa mwafrika tu! Mama wa kihindi anaweza bagua watoto wake wa kuzaa kwa sababu mmoja anazo na mwengine hana.

We acha tu

Na tabia hii ya kubaguana kwa ajili ya hali za maisha ndio inayojenga hali ya kuchukiana hasa kwa wale waliopata mafanikio ila kabla ya hapo walipitia hali kama hizo za kudharauliwa, hivyo kuwafanya kumuona kila mtu anayemfuata ni mchumia tumbo tu.
 
Sio kwa mwafrika tu, hiyo ni kwa wote bwana, achana na nguvu ya pesa kabisa.

Sio kwa wazungu, ndio maana hata wanasiasa wa ulaya na marekani wanaweza kupanda basi au tram moja na raia wa kawaida tofauti na hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom