Mwacheni Mh Rais afanye kazi

Mwacheni Mh Rais afanye kazi

Moja ya kazi zake ni kuilinda na kuitetea Katiba. Ni nani kamwambia avunje Ibara ya 3 ya Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea? Hauwezi kusema aachwe afanye kazi huku akivunja Katiba.
 
Awaache na wanasiasa wafanye kazi zao. Asiwachagulie watu kazi za kufanya kwamba mwanasiasa abaki yeye peke yake. Amekubali kazi ya kisiasa aukubali mziki wake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
maajabu haya ya Tanzania aya. ... kwa kisingizio cha tufanye kazi... mwenyekiti wa ccm anazuia upinzani usifanye mikutano wakati yeye akifanya mikutano kwa gia ya kuwa ni raisi??. .. nadhani washauri wa ccm sasa wamezeeka na kwa kipangere tu cha sympathy... ukawa inavuna popularity ya bure kabisa .. it's possible only in Tanzania. Uganda na Rwanda
 
Ww utakua ni mwanafunzi wa special plogram kule dodoma kwa akili zako unadhani kuandamana kwenda ikulu pekee ndo kunaweza kusababisha kusumbua popote Rais ni watanzania nzima popote mtakapo andamana kukapeleakea watu kutofanya kaz zao ipasavyo ni shida ndo mana nasema tumwache afanye kaz

nadhani wewe unafikilia kama mtoto wa chekechekea. ivi ule umati katika mkutano wa magu pale ndo shambani au pahala pa kufanyia kazi??? ukiargue uwe na base na si kusukumwa na ushabiki pia buku mbili mnazopewa pale lumumba na magu ameahidi kuufuta umoja huo tafuta kazi ya kufanya ndugu
 
Moja ya kazi zake ni kuilinda na kuitetea Katiba. Ni nani kamwambia avunje Ibara ya 3 ya Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea? Hauwezi kusema aachwe afanye kazi huku akivunja Katiba.
Mkuu iyo ibara ya 3 ushaisoma au unaisikia inasema ivi `Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokua na dini yenye kufata mfumo wa vyama vingi vya siasa` kwan mh Rais kufuta mfumo wa vyama vingi au kuzuia demokrasia siasa za matukio ndizo zimezuiwa siasa zisizokua na tija kwa watanzania tunataka siasa zenye faida sio zile za kumtembeza fisadi anayestairi kuwa Kisutu sasa ivi akijibu mashtaka
 
Ww utakua ni mwanafunzi wa special plogram kule dodoma kwa akili zako unadhani kuandamana kwenda ikulu pekee ndo kunaweza kusababisha kusumbua popote Rais ni watanzania nzima popote mtakapo andamana kukapeleakea watu kutofanya kaz zao ipasavyo ni shida ndo mana nasema tumwache afanye kaz

Du..kumbe hatuwezi kujadiliana kama watu wazima bila kuanza kutukanana? Basi haina shida..tuendelee...we endelea kunirushia matusi...mie wala sitakujibu kwa matusi.

Rais hajasema "waacheni watanzania wafanye kazi"..alisema "niacheni nifanye kazi". Lakini basi hebu tuchukulie hicho ulicho andika ndio alichomaanisha rais (kitu ambacho huwezi thibitisha. Je..UKAWA kwenye tamko lao wamemlazimisha mtu yoyote kuacha kufanya kazi zake na kuandama? Si ni hiari ya yoyote anayetaka kufanya hivyo? Je..anayelazimisha hapa si ni Rais ambaye anawanyima watanzania haki yao ya kikatiba ya kuandama?
 
Weeee nae hivi mtu akikusema vyovyote anavyojua yeye wewe inakuzuia vipi kufanya jambo lolote ambalo ulikokusudia kulifanya ambalo halivunji sheria acheni ubabe mwingi ambao hauna maana maringiringi yako palepale MUNGU hakosei mtaweweseka sana!
 
Acha ujinga wewe! hakuna siasa zenye tija pale unapoamua kutoiheshimu katiba ya nchi. Hakuna siasa zenye tija pale unapoamua kuwazuia Wabunge wa Upinzani kujadili kile ambacho wanataka kujadili ndani ya Bunge. Hakuna sifa zenye tija pale unapokingia kifua wezi, mafisadi na wapokea rushwa wa Lugumi, UDA, Pride, Escrow, IPTL, Wanunuzi wa boti bovu la bilioni 8. Hakuna siasa zenye faida wala tija pale unapomfukuza kazi Mkurugenzi wa wilaya kwa kusema ukweli mahakamani halafu unaudanganya umma wa Watanzania kwamba umemfukuza kwa sababu ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Mkuu iyo ibara ya 3 ushaisoma au unaisikia inasema ivi `Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokua na dini yenye kufata mfumo wa vyama vingi vya siasa` kwan mh Rais kufuta mfumo wa vyama vingi au kuzuia demokrasia siasa za matukio ndizo zimezuiwa siasa zisizokua na tija kwa watanzania tunataka siasa zenye faida sio zile za kumtembeza fisadi anayestairi kuwa Kisutu sasa ivi akijibu mashtaka
 
1469985425019.jpg
 
Du..kumbe hatuwezi kujadiliana kama watu wazima bila kuanza kutukanana? Basi haina shida..tuendelee...we endelea kunirushia matusi...mie wala sitakujibu kwa matusi.

Rais hajasema "waacheni watanzania wafanye kazi"..alisema "niacheni nifanye kazi". Lakini basi hebu tuchukulie hicho ulicho andika ndio alichomaanisha rais (kitu ambacho huwezi thibitisha. Je..UKAWA kwenye tamko lao wamemlazimisha mtu yoyote kuacha kufanya kazi zake na kuandama? Si ni hiari ya yoyote anayetaka kufanya hivyo? Je..anayelazimisha hapa si ni Rais ambaye anawanyima watanzania haki yao ya kikatiba ya kuandama?
Mkuu nitajie ibara ya katiba inayoruhusu kuandamana
 
Acha ujinga wewe! hakuna siasa zenye tija pale unapoamua kutoiheshimu katiba ya nchi. Hakuna siasa zenye tija pale unapoamua kuwazuia Wabunge wa Upinzani kujadili kile ambacho wanataka kujadili ndani ya Bunge. Hakuna sifa zenye tija pale unapokingia kifua wezi, mafisadi na wapokea rushwa wa Lugumi, UDA, Pride, Escrow, IPTL, Wanunuzi wa boti bovu la bilioni 8. Hakuna siasa zenye faida wala tija pale unapomfukuza kazi Mkurugenzi wa wilaya kwa kusema ukweli mahakamani halafu unaudanganya umma wa Watanzania kwamba umemfukuza kwa sababu ya kutoridhishwa na utendaji wake.
Kwa iyo ni siasa zenye tija kulitembeza fisadi papa nchi nzima
 
Katiba ya 1977 ibara 18 (a) na 20(1)
Mkuu ibara ya 18 (a) inasema kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake. Nionyeshe neno kuandamana apo.
Lakini pia 20(1) inaongelea wa mtu kushirikiana na wengine nionyeshe pia neno kuandamana
 
Mtu akiandama anafanya nini? ana "kutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani" (nukuu kutoka kwenye katiba).

Na isingekua hivyo serikali ingeshaenda mahakamani kuomba mahakama zizuie maandamo...lakini hawajaenda na wala hawataenda maana hiyo ni kesi ambayo watashindwa asubuhi na mapema.
 
Mkuu wana JF wote tukiamua kukutana na kujadili issues mbalimbali tutakua tumeandamana?? Labda nikusaidie tu kwamba uwezi kukutana na neno kuandamana ndani ya katiba na maandamani yoyote lazima yawe lawfull lazima mpate vibali kwenye mamlaka husika. Tena unaongelea swala la serkali kwenda mahakaman kuzuia maandamano hakuna kitu kama icho maandamano yanazuiwa na tahasisi husika kama polisi walivyofanya sasa ukawa ndo inabidi waende mahakaman kupinga kuzuiwa kuandamana naamini utakua umenielewa na ako kacertifcate kako ka sheria
 
1. Katiba haiwezi kutaja kila neno..ingekua hivyo sijui ingekua na page bilioni ngapi. Ibara ya 20(1) inaweza kutekelezwa kwa njia mbali mbali, moja ikiwemo hiyo uliyotaja wewe ya wana JF kukutana na kutoa mawazo yao hadharani (kitu ambacho tunafanya hapa). Lakini pia inaweza kutekelezwa kwa kuandama...na hilo ndilo lengo kuu la kuandama duniani kote. Mara nyingi hapa Tanzania...hizo zinazoitwa fujo zinatokea pale ambapo polisi wanakuja na madefender yao na kuanza kurusha mabomu ya machozi.

2. Kuhusu swala la kutaarifu mamlaka husika (in this case polisi)...uko sahihi. Ila sheria ya vyama vya siasa ibara ya 11 (1) (a) inasema kwamba polisi watataarifiwa (haijasema wataombwa ruhusa) kuhusu mikutano ya kisiasa au maandamano. Hii ni kuwawezesha polisi kutekeleza wajibu wao kwenye ibara ya 11 (1) (b) ya kutoa ulinzi..ambayo ni haki ya vyama vya siasa, wanachama na wafuasi wao (na mtanzania yoyote yule). Sijaona mahali ambapo polisi wamepewa mamlaka ya kuzuia. Ndio maana wanaishia kutangaza "hali ya hatari" ili kuhalalisha msimamo wao...hali ya hatari ambayo ghafla binvuu inatoweka wakati wa mkutano mkuu wa ccm na kurejea mara baada ya mkutano huo kuisha.
 
Habari zenu wanaukawa, wanacmm na watanzania kwa ujumla wasio na vyama kama mimi.

Kumekuwa na mabandiko yasiyo na idadi katika jukwaa letu pendwa hili ya kumpinga na kumkosoa mh Rais mimi nasema tumwache afanye kazi na tumsaport kwan miaka mitano iliyopita kwenye jukwaa hilihili na wachangiaji walewale kwa mabandiko kibao walisema Mh Kikwete Rais wa awamu iliyopita nchi imemshinda na wengine wakafika mbali zaidi wakasema nchi hii inaitaji kuongozwa na mtu mwenye element za kidikteta. Mungu katupa Rais tuliyemtaka sasa kelele za nini. Kwa nin nasema Rais tuliyemtaka;

1. Kuuza majengo ya serkali yaliyopo Dar serikali ikishaamia Dodoma na kujenga majengo ya aina iyo Dom kwa ili mkuu wa nchi apongezwe tatizo ni kuyauza na asijenge ila ana jenge tena ya aina iyo au zaidi yake sasa nyie mnaotaka yasiuzwe mnataka yajae popo au!, eti kuna wengine wanapendekeza yapangishwe ndg zangu serkali haifanyi biashara aisee wana Dar es salaam lazima tuanze kubadil mentality Dar inabaki kua mji wa biashara tu.

2. Tulitaka Rais dikteta Mungu katupatia ambaye ata robo ya dikteta afiki je tungepewa uyo full dikteta si mngeishakimbia nchi. Tungepewa yule full dicteta ambaye ukitaja kidogo kutaka uenyeki wa chama ujue utafte mlango wa kutokea ingekuwaje.

3.Kuzuia siasa miaka kumi iliyopita chini ya Rais wetu kipenzi Mh kikwete mlipewa nafasi ya kutosha mwisho mkataka kuipeleka nchi pabaya kama si uwezo wa yule mzee kisiasa sijui tungekuwa wap mkatuaminisha mafisadi papa leo ndo mnataka kuwapa nchi chini ya chama chenu alafu mnataka kutuletea siasa uchwara wakati wa kaz ebu tupen mda tufanye kazi mtatuletea hao mafisadi papa 2020 ili tuwakatae tena.

Tumwache mh Rais afanye kaz kwani anatekeleza yale aliyotuaidi alisema atadeal na ufisadi sote ni mashahidi. Wateule wake wakizingua hawaamishii sehem nyingine zaidi ya kuwatimua tunaona, elimu bure tunaona, uwajibikaji serikalini tunaona sasa kelele za nini
Wewe nawe una ung'ombe ng'ombe kumbe?!
 
Back
Top Bottom