Habari wanajamii! Nimefuatilia kwa kina mgogoro unaoendelea kati ya Serikali kwa upande mmoja na Madaktari kwa upande mwigine. Ukweli inasikitisha sana kuona kwamba dhani ya uzalendo imetoweka kabisa kwa pande zote mbili zinazokinzana,viongozi wa serikali wamekosa uzalendo na watumishi wa serikali madaktari nao wamekosa uzalendo. Nchi hii ni yetu sote na raia wanahitaji huduma kutoka serikalini sasa kama kuna dhana ya dhati iliyobebwa na uzalendo ndani yake suala hili lisingefikia hapa lilipofika kwani ufumbuzi ungekwishapatikana muda mrefu. Wizara ya Afya na watendaji wake kama kweli wapo makini walipaswa kulitafutia utatuzi suala hili na Madaktari kwa upande wao pamoja na madai yao ya msingi wanapaswa kuwa na subira.
Kwa hiyo kukosekana kwa uzalendo ndo kiini cha matatizo yote haya. Chende chonde viongozi wa serkali na Madaktari tunaomba mtambue uzalendo katika kuwatumikia wananchi (uma wa Watanzania masikini).
Ahsanteni.