Mvutano Wa Ethiopia na Somalia Washika Kasi Huku Vikosi Vya Usalama Vya Ethiopia ViKimzuia Rais wa Somalia Kuingia Kwenye Mkutano wa AU

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,044
49,727
Hali ya Wasiwasi na mvutano kati ya Ethiopia na Somalia imezidi kuchukua sura Mpya baada ya Vikosi vya Usalama Vya Ethiopia kuharibu kumzuia Rais wa Somalia Mahmoud Hassan kuingia kwenye Mkutano Mkuu wa Viongozi wa Nchi na Serikali unaendelea Mjini Addis Ababa.(AU Summit).

Hali hii inafuatia Ethiopia kutaka kumiliki Ardhi ya Somalia Kupitia Jimbo lililojitenga la Somaliland ambapo Somalia imepinga vikali na Kuendesha kampeni kubwa ya Kidiplomasia na Msaada wa kijeshi Ili kumpambania Ardhi yake isinyakuliwe.

View: https://twitter.com/Kenyans/status/1758886030189453809?t=uCNX_OmbfLugPWk2lkMu9A&s=19

My Take
AU ihamishe Makao Makuu yake kuja Arusha Tanzania Kwa sababu Ethiopia imepoyeza uhalali wa kuwa Makao Makuu Kwa kuingilia uhuru wa Nchi nyingine na kuwa kinara wa migogoro.

View: https://twitter.com/africaupdates/status/1759112514707620180?t=_X-rQoJ7GJakYCiTx_b-Hg&s=19
 
Somalia awe mpole kwani Ethiopia kamzidi mno,ajikite kupambana na alshabaab!

Siungi mkono Ethiopia kunyakua kinguvu ardhi ya jiran yake
 
Somalia awe mpole kwani Ethiopia kamzidi mno,ajikite kupambana na alshabaab!

Siungi mkono Ethiopia kunyakua kinguvu ardhi ya jiran yake
Kwani lazima Somalia apigane conventional war?

Wasomali wana marafiki thabiti wa kuwapa silaha ila front wataenda wenyewe na hiyo roho ya paka Ethiopia hawmuwezi.
 
Somalia awe mpole kwani Ethiopia kamzidi mno,ajikite kupambana na alshabaab!

Siungi mkono Ethiopia kunyakua kinguvu ardhi ya jiran yake
somaliland wanajitegemea tangu awali na hawashei historia moja na hawa wa somalia , Serikali kuu ya Somalia ni dhaifu sana na imegubikwa na rushwa ndio maana Somaliland wanataka jitenga , Somaliland wanataka tambulika ndio maana wamewapa bandari hao Ethiopia kama bibi yenu alivyotaka fanya kwa waarabu , so Somalia wamalize matatizo yao kwanza kisha ndo wawafikirie hao Somaliland
 
Hata Zanzibar inajitegemea lakini Kwa nini haitambuliki Kimataifa kama Nchi huru?

Ukijua sababu basi utaelewa Kwa kesi ya Somaliland na Somalia.

Eritrea imemshinda huyo Ethiopia anataka alete Utapeli Kwa Somalia kisa hawana Nguvu kubwa? Hawezi kufaulu.
 
Back
Top Bottom