Mvua yavunja mechi ya Stand Utd na Kagera Sugar

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,148
2,219
Leo katika mechi YA Ligi Kuu Kati YA Stand United chama la wana! Na Kagera Sugar limeshindwa kumalizka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika Uwanja wa CCM Kambarage hadi Mpira unasimama Stand UTD Ilikuwa inaongoza goli MOJA lililofungwa na Striker machachari Toka Nigeria Chidi Obare .... Kesho asubuhi mechi hiyo itamaliziwa dakika kumi zilizobaki! iwapo matokeo yatabaki hivyo msahau Stand Utd CHAMA la wana!! Kushika daraja

Hii Ni kutoka official Facebook page YA Stand Utd CHAMA la Wana!

Shukrani za dhati sana kwa mashabiki wetu walioko Tanzania nzima na dunia kwa ujumla kwa kuendela kutuombea dua njema kwa mungu, na hasa walioko shinyanga na kanda ya ziwa kwa kujitokeza uwanjani siku ya jana na leo asubuhi katika Mchezo wetu wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Ccm Kambarage shinyanga.

Chama la Wana, Stand United imefainikiwa kulinda bao lake la jana na kuongeza jingine leo asubuhi katika kujihakikishia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar FC.

Baada ya kuichapa Simba SC bao 1-0 Jumapili ya wiki iliyopita, Stand ilipata bao dakika ya 43 jana jioni kwa penalti kupitia kwa mshambuliaji Mnigeria Abasalim Chidiabele ambaye pia ndiye alifunga bao lao la ushindi dhidi ya Simba SC.

Mechi hiyo iliahirishwa dakika ya 80 na refa Hashim Abdallah kutoka Dar es Salaam baada ya kunyesha mvua kubwa ikiambatana na upepo mkali kiasi cha kuwa kiza uwanjani.

Katika kumalizia dakika 10 za mchezo huo leo kuanzia saa 2:30 asubuhi, Stand iliongeza bao la pili dakika ya nne na ya 84 ya mchezo wote kupitia kwa mshambuliaji Abasalim Chidiabele kwa mara nyingine tena baada ya kuwatoka mabeki wa Kagera na kufumua shuti kali lililotinga moja kwa moja nyavuni.
Chidiabele kwa hivi sasa amefikisha magoli 7 katika ligi kuu soka Tanzania Bara VPL.

Mola tuongoze STAND United FC (chama la wana)
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    63.8 KB · Views: 56
Leo katika mechi YA Ligi Kuu Kati YA Stand United chama la wana! Na Kagera Sugar limeshindwa kumalizka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika Uwanja wa CCM Kambarage hadi Mpira unasimama Stand UTD Ilikuwa inaongoza goli MOJA lililofungwa na Striker machachari Toka Nigeria Chidi Obare .... Kesho asubuhi mechi hiyo itamaliziwa dakika kumi zilizobaki! iwapo matokeo yatabaki hivyo msahau Stand Utd CHAMA la wana!! Kushika daraja

Mchezo ukishaahirishwa hurudiwa fresh yaani play de novel, matokeo na matukio yote hufutwa na mechi kuanza upya.
 
Mchezo ukishaahirishwa hurudiwa fresh yaani play de novel, matokeo na matukio yote hufutwa na mechi kuanza upya.

Hii si Mara YA kwanza tulivyoenda Manungu na Mtibwa mchezo uliahirishwa na kesho yake tulianzia dk zilizobaki na goli letu lilihesabiwa Mtibwa ndo akasawazisha
 
Hii si Mara YA kwanza tulivyoenda Manungu na Mtibwa mchezo uliahirishwa na kesho yake tulianzia dk zilizobaki na goli letu lilihesabiwa Mtibwa ndo akasawazisha

Ok Mkuu, ni kweli wameanzia pale walipoishia jana.Thanks to God, chama la wana limeibuka kidedea asubuhi hii. Jana bao moja na leo bao moja, jumla Stand United 2-0 Kagera Sugar.
 
Ok Mkuu, ni kweli wameanzia pale walipoishia jana.Thanks to God, chama la wana limeibuka kidedea asubuhi hii. Jana bao moja na leo bao moja, jumla Stand United 2-0 Kagera Sugar.

Chidi Belle LAZIMA awe mfungaji bora msimu huu!! Point 21 hizo kibindoni
 
Stand Utd wanampumlia mnyama.
Hahaaa Hahaaa ila hii Ligi ngumu tunasubiri mechi za Mbeya tuweke uhakika Mnyama anarudisha CCM Kambarage tarehe 7/4 kucheza na Kagera Sugar wana Nkurukumbi anaacha tena point 3
 
Mchezo ukishaahirishwa hurudiwa fresh yaani play de novel, matokeo na matukio yote hufutwa na mechi kuanza upya.
Usiwe mbishi kama Ngasa, mechi imemaliziwa asubuhi kwa dakika 10, na Chidi ameiongezea Stand United bao la pili. FT Stand United 2 - 0 Kagera Sugar.
 
Hongera stand gangamara kweny ligi msimu ujao uungane na toto africa,african sports kumdharirisha mnyama
 
Waambie waje kuchezea huku. Mvua hakuna.

Stand utd chama la Wana!! Tuna Baraka YA kufatwa na mvua, hata Manungu na Mtibwa mvua ilivunja pambano! Na mechi karibia 4 kuanzia ZA Ligi daraja la kwanza ilikuwa unapiga mvua ya kufa Mtu! Hata tukija huko tunakuja na Baraka zetu za mvua!
 
Usiwe mbishi kama Ngasa, mechi imemaliziwa asubuhi kwa dakika 10, na Chidi ameiongezea Stand United bao la pili. FT Stand United 2 - 0 Kagera Sugar.

Nawe sasa umekua, angalia hapo juu, nimeposti nini. Acha kukurupuka! Umeposti saa 6:18 mchana wakati mimi nimeripoti matokeo hayo saa 3 asubuhi. Kabla ya kulurupuka uwe unasoma posti zote uone kama kuna updates zaidi.
 
Ishu sio kuwahi kuposti matokeo, bali ni mechi kumaliziwa dakika zilizobaki au kuanza upya. Wewe jana ulisema matokeo yangefutwa ianze upya, cha ajabu unakuja kuweka matokeo mwenyewe! Jambo la kukufundisha ni kwamba kila mashindano huwa yana kanuni zake zinazopangwa kabla hata hayajaanza.
 
Stand utd chama la Wana!! Tuna Baraka YA kufatwa na mvua, hata Manungu na Mtibwa mvua ilivunja pambano! Na mechi karibia 4 kuanzia ZA Ligi daraja la kwanza ilikuwa unapiga mvua ya kufa Mtu! Hata tukija huko tunakuja na Baraka zetu za mvua!

wachawi tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom