Mvua ya kimbunga kikali kuanza kesho

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa hadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia kesho hadi mwisho wa mwezi huu, itakayosabaishwa na kimbunga kiitwacho Fantala.

Kimbunga hicho kipo katika eneo la Bahari ya Hindi kikienda kwa mwendo wa pole pole na kilikuwa hakijaleta madhara, lakini kwa sasa athari zake zimeanza kuonekana.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema wanatarajia kuanzia kesho hali ya mvua itaendelea kuongezeka katika maeneo ya Ziwa Victoria na maeneo ya Magharibi.

Alisema kutokana na upepo kuvutwa na kimbunga hicho kwenda baharini, eneo kubwa la nchi litakuwa na mvua kubwa hivyo, wananchi wametakiwa kuchukua hadhari “Sasa tuko katika msimu wa mvua za masika, lakini kimbunga hiki kitasababisha ongezeko la mvua, hivyo ni vizuri tahadhari zikachukuliwa,” alisema.

Alisema tatizo kubwa la kimbunga hicho ni mgandamizo mdogo wa hewa unaoweza kuvuta upepo kutoka maeneo mbalimbali kwenda sehemu ambazo kimbunga kipo. Dk Kijazi aliongeza kuwa, kila siku wakati wa kutoa utabiri, watatoa tahadhari ya maeneo yatakayoathirika zaidi hivyo wananchi wanapaswa kuzingatia utabiri wa kila siku.

Alisema vimbunga vimekuwa vikipewa majina na nchi zilizo Ukanda wa Pwani ambayo hupendekeza kwa kufuata mpangilio wa herufi kulingana na msimu unaoanza Novemba mpaka Aprili na hiki ni kimbunga ni cha sita, lakini siyo vyote vyenye madhara kwa nchi.

Alisema vingine havijasikika kutokana na kutokuwa na madhara kwa nchi, lakini Fantala kina madhara ya kusababisha kuongezeka kwa mvua katika maeneo mengi ya nchi.

“Mpaka sasa tupo kwenye msimu wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha na kuna dalili zinazoonesha kimbunga hicho kimeanza kuleta athari lakini kuanzia Jumapili na mvua zitaongezeka zaidi,” alisisitiza.
 
Mhh, utaalamu upi. Unajuaje kama hakukaa mezani na kuandika. We toa shukrani kwa taarifa, kujua kama ni ya kitaalamu au vipi you need evidence!
Ni kweli ili kutoa taarifa kama hii ni lazima uandike na lazima uwe na uwezo wa kitaaluma kusoma ktk satelite mwenendo wa mawingu, mfumo wa upepo mgandamizo wa hewa
 
Ni kweli ili kutoa taarifa kama hii ni lazima uandike na lazima uwe na uwezo wa kitaaluma kusoma ktk satelite mwenendo wa mawingu, mfumo wa upepo mgandamizo wa hewa
NAKUBALIANA NA WEWE, LAKINI KATIKA NCHI KAMA HII AMBAYO KILA KITU KINAWEZEKANA, ONE CAN EASILY COOK DATA (SISEMI WAMECOOK DATA , NO)
 
Mimi binafsi tabiri za mamlaka yetu ya hali ya hewa huwa siiamini mpaka niione mvua kabisa.....
 
Nimeona sasa hivi BBC na al Jazeera pia wamesema kutakuwa na mvua kubwa kuanzia leo na kesho hapa tanzania
 
Na mwenye taarifa zaid kuhusu ile Sayari ya NIBIRU atujulishe tafadhali
Mkuu kwa taarifa za uhakika ni kuwa ile sayari bado ipo njiani....kwa kasi ya ajabu inatarajiwa kuigonga dunia mwishoni mwa mwezi huu......
Kwa hiyo hakuna haja ya kuweka akiba wala kujenga wewe tumbua tu hizo hela kabla ya Nibiru haijahitimisha.....si unajua uko kwa mkuu hela haina kazi.....
 
Mkuu kwa taarifa za uhakika ni kuwa ile sayari bado ipo njiani....kwa kasi ya ajabu inatarajiwa kuigonga dunia mwishoni mwa mwezi huu......
Kwa hiyo hakuna haja ya kuweka akiba wala kujenga wewe tumbua tu hizo hela kabla ya Nibiru haijahitimisha.....si unajua uko kwa mkuu hela haina kazi.....
Hamna kitu mkuu! Ingeshaonekana tena bila darubini siku saba si nying au kama una wasiwasi nitumie hizo hela nikutunzie
 
Hiyo mamlaka ya hali ya hewa ya nchi hii imekuwa kama uganga wa kienyeji.Nishakula hasara sana kwa ajili yao.
 
Back
Top Bottom