Mvua kutoka Thailand: Lowassa ajitetea bungeni

Mvua kutoka Thailand: Lowassa ajitetea bungeni

Kichwa cha habari hakiendani kabisa na content
 
Leo Jenister Mhagama amempa nafasi Lowasa atoe ufafanuzi baada ya upotoshaji.
Nimejiuliza je angekua Tundu Lisu angepewa nafasi?

huyo tundu lissu anayetibiwa mirembe ameingiaje ktk maelezo ya lukuvi kuhusu mvua na ni wapi lowasa amejitetea? Mleta mada una malaria sugu kapime damu haraka
 
Hizi mvua zingekuwa zanunuliwa, uarabuni kungekuwa ever green mwaka mzima.

Amin amin nawaambieni, Lowasa anaweza kumiuzeni (wa) any time.

Mijitu imekaa kama ng'ombe anapelekwa machinjioni.
 
Swala la msingi hapa je kuna utaalamu huo wa kuleta mvua kwa njia za kisayansi jibu rahisi kabisa ni NDIO haya mengine yote ni siasa za kwetu ila technology inaruhusu kabisa

Nakumbuka vizuri. Waziri Mkuu (Lowasa wakati huo), aliagiza tuingie mkataba na shirika la Thailand lije lifanye cloud seeding ili kujaza Bwawa la Mtera. Lilikuwa limepungua sana na kuathiri uzalishaji wa umeme.

Tulijadili sana hili swala humu mtandaoni. Tulikubaliana kwamba ilikuwa absolutely not cost effective.

Mtu anayedhani unaweza kujaza Bwawa la Mtera kwa kukodisha ndege zifanye cloud seeding hafai kuwa kiongozi. Ni mbumbumbu mno.
 
Mvua zingekuwa zanunuliwa, Misri isingeuabudu mto Nile.
 
Huyu mama Huviza ana matatizo kweli. Tangu siku ile alipochemka kwenye mapori tengefu (ya Wizara ya Maliasili na Utalii) akisema ni maeneo oevu yaliyo chini ya Wizara ya Mazingira, nilimchoka kabisa. Hajui kabisa tofauti ya maeneo tengefu na maeneo oevu. Huyu ndiye anayeongoza wizara!! Kazi kweli kweli.

Ndo mawaziri wetu hao,bora angebaki na kazi yake ya Dean pale DuCe,vigezo gani sijui
 
Huyu mama Huviza ana matatizo kweli. Tangu siku ile alipochemka kwenye mapori tengefu (ya Wizara ya Maliasili na Utalii) akisema ni maeneo oevu yaliyo chini ya Wizara ya Mazingira, nilimchoka kabisa. Hajui kabisa tofauti ya maeneo tengefu na maeneo oevu. Huyu ndiye anayeongoza wizara!! Kazi kweli kweli.

Nafikiri tatizo sio la waziri pekee yake.....ni tatizo la wataalamu wa wizara husika pia....! Ni vizuri hawa mawaziri wawe wanapewa briefing za mambo ya kitaalamu ya wizara wanazoongoza...!

Nilihudhuria siku moja cocktail nyumbani kwa balozi wa nchi fulani pamoja na huyu mama nilishangaa jinsi alivyokuwa anaropoka vitu bila kujua kuwa anaongea pumba......!
 
Huyu mama Huviza ana matatizo kweli. Tangu siku ile alipochemka kwenye mapori tengefu (ya Wizara ya Maliasili na Utalii) akisema ni maeneo oevu yaliyo chini ya Wizara ya Mazingira, nilimchoka kabisa. Hajui kabisa tofauti ya maeneo tengefu na maeneo oevu. Huyu ndiye anayeongoza wizara!! Kazi kweli kweli.

MKuu, huyo ni Dr. kama Jk
 
... Hajui kabisa tofauti ya maeneo tengefu na maeneo oevu. ...

Kiswahili hakina mpangilio .. yaani hovyo kabisa! Ni wazi kinamilikiwa na watu wachache waliojitwika jukumu la kuamua maneno gani yatumike (badala ya kuacha lugha ikue yenyewe). . Wengi tunapata shida ya kujua maneno (terms/terminologies) yanayoibuliwa kila kukicha bila mpangilio ... Hapa kiingereza kingetumika wengi (pamoja na huyo waziri) tungeelewa tu.
 
Huyu mama Huviza ana matatizo kweli. Tangu siku ile alipochemka kwenye mapori tengefu (ya Wizara ya Maliasili na Utalii) akisema ni maeneo oevu yaliyo chini ya Wizara ya Mazingira, nilimchoka kabisa. Hajui kabisa tofauti ya maeneo tengefu na maeneo oevu. Huyu ndiye anayeongoza wizara!! Kazi kweli kweli.

Usishangae MKUU. Hao ndio MAGAMBA na PhD za kutungua. Nasikia PhD yake aliipata DSI-SUA kwa "Msaada" wa CHAMA!! Mumewe alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha MAGAMBA. Mkurugenzi wa DSI alikuwa Kada wa Chama na "homeboy" wa Mumewe. Supervisor wake alikuwa Kada wa CHAMA na sasa yuko TAKUKURU. Sasa kwa nini ushangae TENGEFU kuitwa OEVU?
 
Kwa hiyo huyu Waziri wa Mazingira (OMWR) si ni Doctor????!
Ameshindwaje kujua kwamba utaalamu huo upo??
Na kama Waziri amedanganya(kwa maelezo ya Lowassa na Lukuvi) alikuwa akijibu kwa niaba ya Rais au nani??!
Na kama hakuwa akijibu kwa niaba ya Rais, nani amemtuma?
Bunge linachukua hatua gani kwa kudanganya?
Rais anamchukulia hatua gani kwa kumdhalilisha bungeni na kutoa majibu ya uongo?!
CCM bwana!
 
Hii ndio sera ya ccm na usiri wa mikataba
mi nakumbuka mara baada ya lowassa kutoka huko thailand hakumaliza hata wiki.....rais wa thailand akapinduliwa na ndio ukawa mwisho wa habari ya mvua hiyo.....haya mambo ya kusema bajeti haikutosha yanatoka wapi?
 
Mambo mengine ni aibu
tz inashindiwa kupanda miti kutunza mazingira
tupate mvua wanawaza kununua mvua loooh;
au ndo hizo ten percent zinawasumbua.

Umenifurahisha na kunichekesha kweli yaani ni kama tumeshindwa kutumia ardhi yetu kulima chakula kujikinga na njaa na badala yake tunapanga kutafuta ardhi ya kilimo hicho mwezini.
 
Tena eti ndo rais mtarajiwa,
looh, lowasa ni janga la kimataifa.

Umenifurahisha na kunichekesha kweli yaani ni kama tumeshindwa kutumia ardhi yetu kulima chakula kujikinga na njaa na badala yake tunapanga kutafuta ardhi ya kilimo hicho mwezini.
 
Hii habari nafikiri Pasco anaweza kuieleza vizuri.
Lukuvi Majanga. Lowasa majanga mara mia.
 
Dodoma.Suala la mvua za kutengeneza kutoka nchi ya Thailand maarufu kwa jina la ‘Mvua za Lowassa' liliwagonganisha mawaziri wawili wa Serikali bungeni jana. Ubishi mkali ulizuka baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Terezya Huvisa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi waliokuwa wakivutana juu ya ukweli kuhusu teknolojia hiyo.

Wakati Waziri Huvisa akisema kwamba hakuna utaalamu wa aina hiyo, Lukuvi alisimamia kumpinga na kusisitiza kuwa jambo hilo lipo.
Suala la mvua hizo lililetwa nchini na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa mwaka 2007, baada ya kufanya ziara Thailand ambako alivutiwa na utaalamu wa kutengeneza mvua na kuahidi kuuleta nchini.

Kutokana na mvutano wa mawaziri hao, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alipewa dakika moja na Mwenyekiti wa Bunge, Jenister Mhagama kutoa ufafanuzi ambapo aliunga mkono hoja ya Lukuvi. Malumbano hayo yalisababishwa na swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo ambaye alihoji mpango wa kutengeneza mvua ulipoishia kwa kuwa Serikali imekuwa kimya.
"Sasa ni miaka takriban sita au saba tangu Serikali ilipokuja na mpango wa kutengeneza mvua ambao iliuchukua kutoka nchi za wenzetu, mpango huo umefikia wapi?" aliuliza.

Akijibu swali hilo, Waziri Huvisa alisema: "Mimi ni Rais wa Mazingira wa Afrika, nasema hakuna kitu kama hicho, si Marekani wala Malaysia ambao wanaweza kutengeneza mvua, hayo ni mabadiliko ya tabianchi tu." Waziri Lukuvi alionyesha kutokuridhishwa majibu hayo, ndipo aliposimama kutoa ufafanuzi na kusema Lowassa alikwenda Thailand ambako kuna utaalamu huo na kusisitiza kwamba upo na bado unaendelea kutumika hata Ujerumani wanakotumia mitambo ya kijeshi kusambaratisha mawingu.

Alisema kilichokwamisha mpango huo nchini ni ufinyu wa bajeti ya Serikali. Baada ya majibu hayo, Lowassa alisimama akitaka kutetea wazo lake. Hata hivyo, kabla ya kumruhusu, Mhagama alimwomba akae chini kwanza ili atoe maelekezo. "Mheshimiwa Lowassa, yeye siyo waziri na hivyo hastahili kutoa majibu ya Serikali, lakini kwa kutumia kanuni zetu bungeni kuhusu kutengeneza utaratibu mzuri wa kuongoza Bunge, naomba Lowassa usimame sasa walau kwa dakika moja au mbili utoe ufafanuzi," alisema Mhagama.

Aliposimama Lowassa alizungumza kwa ufupi; "Nakushukuru Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kukazia tu kuwa jibu lililotolewa na Mheshimiwa Lukuvi ndilo jibu sahihi."

Majibu hayo yalisababisha Bunge kulipuka kwa shangwe.

Mara baada ya majibu ya Lowassa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza naye alisimama akitaka kutoa maelezo. Hata hivyo, Mhagama alisema inatosha na kuwaagiza mawaziri hao kukutana kuliangalia jambo hilo badala ya kuwa na majibu kinzani. Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Rachel Mashishanga alitaka kujua ni kwa nini Serikali isirasimishe utaalamu wa kuleta mvua kutoka kwa waganga wa jadi walioko Mikoa ya Katavi na Rukwa ili maeneo yanayokabiliwa na ukame yapate mvua?

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, alipinga mpango huo na kusema hakuna kitu kama hicho isipokuwa wapo watu wenye utaalamu wa kuangalia mawingu yanayoendana na mvua. Alisema watu wote wanaosema kuwa wanaweza kutengeneza mvua kwa imani za kishirikina ni waongo na hivyo hawapaswi kuaminiwa.

Alisema siyo wakati mwafaka kwa Serikali kushinikizwa kurasimisha utaalamu huo wa kuleta mvua kwa kuwa hakuna tafiti zozote zilizofanyika na kuthibitisha kuwapo kwake.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom