Mvua kutoka Thailand: Lowassa ajitetea bungeni

Mvua kutoka Thailand: Lowassa ajitetea bungeni

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Posts
18,830
Reaction score
12,318
Leo Jenister Mhagama amempa nafasi Lowasa atoe ufafanuzi baada ya upotoshaji. Nimejiuliza je angekua Tundu Lisu angepewa nafasi?

Baada ya waziri wa mazingira kukanusha juu ya uwepo wa utaalamu wa kuleta mvua toka southern east asia(akijibu swali la suzan lymo juu ya mvua toka thailand zilizoahidiwa na serikali)...lukuvi akasimama na kumpinga waziri wa mazingra kwa kusema utaalamu huo upo na unatumika..tatizo bajeti haikua nzuri ndio maana kipindi kile serikali haikutekeleza ahadi hìyo. Baada ya mkanganyiko huo,mh lowasa akasimama nakusema 'nathibitisha maelezo ya lukuvi ndio sahihi'.

----------------------------------

Dodoma.Suala la mvua za kutengeneza kutoka nchi ya Thailand maarufu kwa jina la ‘Mvua za Lowassa' liliwagonganisha mawaziri wawili wa Serikali bungeni jana. Ubishi mkali ulizuka baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Terezya Huvisa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi waliokuwa wakivutana juu ya ukweli kuhusu teknolojia hiyo.

Wakati Waziri Huvisa akisema kwamba hakuna utaalamu wa aina hiyo, Lukuvi alisimamia kumpinga na kusisitiza kuwa jambo hilo lipo.
Suala la mvua hizo lililetwa nchini na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa mwaka 2007, baada ya kufanya ziara Thailand ambako alivutiwa na utaalamu wa kutengeneza mvua na kuahidi kuuleta nchini.

Kutokana na mvutano wa mawaziri hao, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alipewa dakika moja na Mwenyekiti wa Bunge, Jenister Mhagama kutoa ufafanuzi ambapo aliunga mkono hoja ya Lukuvi. Malumbano hayo yalisababishwa na swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo ambaye alihoji mpango wa kutengeneza mvua ulipoishia kwa kuwa Serikali imekuwa kimya.
"Sasa ni miaka takriban sita au saba tangu Serikali ilipokuja na mpango wa kutengeneza mvua ambao iliuchukua kutoka nchi za wenzetu, mpango huo umefikia wapi?" aliuliza.

Akijibu swali hilo, Waziri Huvisa alisema: "Mimi ni Rais wa Mazingira wa Afrika, nasema hakuna kitu kama hicho, si Marekani wala Malaysia ambao wanaweza kutengeneza mvua, hayo ni mabadiliko ya tabianchi tu." Waziri Lukuvi alionyesha kutokuridhishwa majibu hayo, ndipo aliposimama kutoa ufafanuzi na kusema Lowassa alikwenda Thailand ambako kuna utaalamu huo na kusisitiza kwamba upo na bado unaendelea kutumika hata Ujerumani wanakotumia mitambo ya kijeshi kusambaratisha mawingu.

Alisema kilichokwamisha mpango huo nchini ni ufinyu wa bajeti ya Serikali. Baada ya majibu hayo, Lowassa alisimama akitaka kutetea wazo lake. Hata hivyo, kabla ya kumruhusu, Mhagama alimwomba akae chini kwanza ili atoe maelekezo. "Mheshimiwa Lowassa, yeye siyo waziri na hivyo hastahili kutoa majibu ya Serikali, lakini kwa kutumia kanuni zetu bungeni kuhusu kutengeneza utaratibu mzuri wa kuongoza Bunge, naomba Lowassa usimame sasa walau kwa dakika moja au mbili utoe ufafanuzi," alisema Mhagama.

Aliposimama Lowassa alizungumza kwa ufupi; "Nakushukuru Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kukazia tu kuwa jibu lililotolewa na Mheshimiwa Lukuvi ndilo jibu sahihi."

Majibu hayo yalisababisha Bunge kulipuka kwa shangwe.

Mara baada ya majibu ya Lowassa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza naye alisimama akitaka kutoa maelezo. Hata hivyo, Mhagama alisema inatosha na kuwaagiza mawaziri hao kukutana kuliangalia jambo hilo badala ya kuwa na majibu kinzani. Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Rachel Mashishanga alitaka kujua ni kwa nini Serikali isirasimishe utaalamu wa kuleta mvua kutoka kwa waganga wa jadi walioko Mikoa ya Katavi na Rukwa ili maeneo yanayokabiliwa na ukame yapate mvua?

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, alipinga mpango huo na kusema hakuna kitu kama hicho isipokuwa wapo watu wenye utaalamu wa kuangalia mawingu yanayoendana na mvua. Alisema watu wote wanaosema kuwa wanaweza kutengeneza mvua kwa imani za kishirikina ni waongo na hivyo hawapaswi kuaminiwa.

Alisema siyo wakati mwafaka kwa Serikali kushinikizwa kurasimisha utaalamu huo wa kuleta mvua kwa kuwa hakuna tafiti zozote zilizofanyika na kuthibitisha kuwapo kwake.

Chanzo: Mwananchi
 
alooooooooooooooo halafu hili bunge letu halipo serious manake mambo ya msingi wanayafanyia utani hii ni fedheha kwa taifa hili
 
Baada ya waziri wa mazingira kukanusha juu ya uwepo wa utaalamu wa kuleta mvua toka southern east asia(akijibu swali la suzan lymo juu ya mvua toka thailand zilizoahidiwa na serikali)...lukuvi akasimama na kumpinga waziri wa mazingra kwa kusema utaalamu huo upo na unatumika..tatizo bajeti haikua nzuri ndio maana kipindi kile serikali haikutekeleza ahadi hìyo. Baada ya mkanganyiko huo,mh lowasa akasimama nakusema 'nathibitisha maelezo ya lukuvi ndio sahihi'.
 
Huyu mama Huviza ana matatizo kweli. Tangu siku ile alipochemka kwenye mapori tengefu (ya Wizara ya Maliasili na Utalii) akisema ni maeneo oevu yaliyo chini ya Wizara ya Mazingira, nilimchoka kabisa. Hajui kabisa tofauti ya maeneo tengefu na maeneo oevu. Huyu ndiye anayeongoza wizara!! Kazi kweli kweli.
 
Ilikuwa lazima ajibu kwasababu ilikuwa ni mipango yake ya kifisadi. Serikali kipindi kile haikuwa na tatizo la Bajeti kama anavyosema Lukuvi. Kama tatizo ilikuwa ni Bajeti, alifanya ziara ya nini kule Thailand kuitafuta hiyo mvua! Tunachokijua ni kuwa ule, Utawala ambao alikula nao dili ulipinduliwa!
 
mi nakumbuka mara baada ya lowassa kutoka huko thailand hakumaliza hata wiki.....rais wa thailand akapinduliwa na ndio ukawa mwisho wa habari ya mvua hiyo.....haya mambo ya kusema bajeti haikutosha yanatoka wapi?
 
Baada ya waziri wa mazingira kukanusha juu ya uwepo wa utaalamu wa kuleta mvua toka southern east asia(akijibu swali la suzan lymo juu ya mvua toka thailand zilizoahidiwa na serikali)...lukuvi akasimama na kumpinga waziri wa mazingra kwa kusema utaalamu huo upo na unatumika..tatizo bajeti haikua nzuri ndio maana kipindi kile serikali haikutekeleza ahadi hìyo. Baada ya mkanganyiko huo,mh lowasa akasimama nakusema 'nathibitisha maelezo ya lukuvi ndio sahihi'.

Lukuvi si kikaragosi cha Lwaigwanan, mlitegemea hapo asemeje wakati aliyeleta wazo hilo la mvua za Ki-richmond ni Lwaigwanan?
 
Mkuu funguka zaidi upotoshaji gani?

Kuna swali liliulizwa kuhusu mvua ya Thailand ambapo Lowasa akiwa Pm alihaidi kuwaleta wataalam.
Waziri akajibu hakuna cha mvua wala nini kutoka Thailand Wao wenyewe wanaukame.
Lukuvi akaibuka na kujibu ThaIland wanauwezo wa kutengeneza mvua.
Pakatokea mtafaruku bungeni na Lowasa kusimama kutaka kutoa majibu.
Akaruhusiwa na kusema maelezo ya Lukuvi ni sahihi.
Swali ni je, ingekua ni mbunge wa chadema angepewa nafasi atoe majibu ya swali la mbunge bungeni?
 
Alichothimbitisha LUKUVI ni utaalamu wa kisayansi ambao nchi nyingine wanafanya hakumpinga waziri acha upotoshaji ndipo lowasa akasimama na kuendelea kuthibitisha kwamba alilosema lukuvi ni kweli,
 
Jibu la waziri ni la wasomi na wataalam wa wizara! Wamepiga mahesabu na kuona haiwezekani. Lukuvi na sheikh Abdallah Lowassa wanafanya siasa
 
Mambo mengine ni aibu
tz inashindiwa kupanda miti kutunza mazingira
tupate mvua wanawaza kununua mvua loooh;
au ndo hizo ten percent zinawasumbua.
 
mi nakumbuka mara baada ya lowassa kutoka huko thailand hakumaliza hata wiki.....rais wa thailand akapinduliwa na ndio ukawa mwisho wa habari ya mvua hiyo.....haya mambo ya kusema bajeti haikutosha yanatoka wapi?

Waziri mkuu huyo wa Thailand (wakati huo) alikuwa ni Thaksin Shinawatra. Ambaye ni kaka wa waziri mkuu wa sasa wa Thailand.
 
Duh!!Ama kweli maajabu ya kila aina yapo tanzania,gesi ipo lakini tunaambiwa na waziri uwezo wetu ni juice na matunda gesi ni ya wakoloni,sheikh abdalah lowassa enzi zake watu wanakata miti kupikia mazingira yanakuwa na ukame analeta deal la mvua za kichina(bandia)...haki ya nani aliyeturoga kafa!!!
 
Swala la msingi hapa je kuna utaalamu huo wa kuleta mvua kwa njia za kisayansi jibu rahisi kabisa ni NDIO haya mengine yote ni siasa za kwetu ila technology inaruhusu kabisa
 
Serikali lazima itekeleze mpango wa mvua ya kutengeneza. Ishu ni bajeti tu
 
hana lolote jenister anajaribu kutengeneza network ya kijinga.
 
Back
Top Bottom