Mvi kichwani katika umri mdogo

NGULI

JF-Expert Member
Mar 31, 2008
4,803
637
Ndg wana JF

Mimi nikijana mdogo wa kiume wa kitanzania mwenye umri wa miaka 28 lakini kichwa changu chote ni cheupe kwa hivi sasa kina mvi ziliianza kuota nikiwa na miaka 21.

Sasa nataka kuoa na kila msichana nae kutana nae ananiambia shikamoo bro hata dada zangu na kaka zangu wananiambia shikamoo, je zaidi ya kupaka mapiko yenye madhara kwa afya ya mtu je kuna njia mbadala ya kurudisha uoto wa asili?

Upara sio solution nitazidi kukimbiza marafiki na mchumba naye msaka kwa vile kichwa changu kina mabonde mabonde lazima tukuubaliane sio wote tunaoweza kunyoa upara.

Nitshukuru kwa kunipa ushauri kwenye hili tatizo linalonikera

Nawakilisha na aksanteni.
 
Nguli kama ulikuwepo kwenye mawazo yangu.Kwa muda wa miaka hii nimekuwa nikikutana na vijana chini ya miaka 35 yani mvi kibao kichwani.Yani ni vijana kabisa.Tofauti na wazee wetu wa zamani kabisa mpaka uone mvi ni miaka 60.
Kuna vijana ambao nimesoma nao nikikutana nao ni mvi kidevu chote.
Nadiriki kusema karibu 75% ya vijana wana mvi.
Wataalamu mtuambie tatizo ni nini? na dawa?
 
Watu wananimabia nile vyakula vya protin tena ndio kama inazididsha vile.
 
kuna wimbo mmoja waliimba sijui wakenya wale, ila ulikua ukiimba hivi, nanukuu "kipara na nywele nyeupe si uzee" hapo mkuu hakuna dawa cha muhimu ni kuikubali tu hiyo hali yako na pia nadhani mvi si kigezo cha wewe kukosa mke, wapo wamependwa walemavu, nk. mi nadhani kama mtu anakupenda ni lazima atakubaliana pia na hali yako ulivyo. Omba mungu utapata tu mke ndugu yangu na sio kujisikia inferior
 
Mkuu,

Unazidi kunisononesha, niko serious mwenzenu nitakosa mke hivix2

Wala usiogope Mkuu Nguli, kinachojalisha ni mawazo na tabia zaidi, mwonekano weka kando la sivyo mademu wasingekuwa wanasasambua kwa EL. Kama mwanamke anaangalia mvi, nampa pole. Mwalimu wangu ana miaka 76 na mvi hazifiki 10.

Tena bora wewe miaka 28, mimi zilinibana toka niko sekondari, sizifichi wala nini na watoto wapo bwerere.
 

Thanks DINGI,
Nimepata hizi point hapa chini........

People can get gray hair at any age. Some people go gray at a young age - as early as when they are in high school or college - whereas others may be in their 30s or 40s before they see that first gray hair. How early we get gray hair is determined by our genes. This means that most of us will start having gray hairs around the same age that our parents or grandparents first did
 

Attachments

  • K_hair_turn_gray1.gif
    K_hair_turn_gray1.gif
    9.7 KB · Views: 106

Similar Discussions

Back
Top Bottom