MV UKEREWE MBIONI KUKAMILIKA

MV UKEREWE MBIONI KUKAMILIKA

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
MV UKEREWE MBIONI KUKAMILIKA

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) inatekeleza mradi wa ujenzi wa vivuko vipya 6.

Moja ya Vivuko hivyo ni Kivuko MV. UKEREWE ambacho kitakwenda kutoa huduma kati ya Kisorya Wilayani Bunda Mkoani Mara na Rugezi Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza ambacho mpaka sasa ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 82% na kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 170 na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.

Kivuko hicho kinakwenda kukiongezea nguvu kivuko MV. UJENZI kinachotoa huduma eneo hilo ambacho kinao uwezo wa kubeba tani 85, abiria 330 na magari madogo 10.
 

Attachments

  • FB_IMG_1744724394711.jpg
    FB_IMG_1744724394711.jpg
    51 KB · Views: 15
Back
Top Bottom