MV Lami Kigamboni: Kama si salama mbona bado kinafanya kazi?

wazirihusika

Member
May 17, 2013
83
82
"MV lami haipakii abiria kwasababu sio salama,tunaomba abiria wote wasubiri MV kigamboni"hilo ni tangazo tulilozoea watu tunaoishi Kigamboni.

Sasa nashindwa kuelewa kama kile kivuko sio salama inakuaje kinapandisha waendesha baiskeli,bajaji,mikokoteni na magari pamoja na madereva wa hayo magari?

Kama mmekiri kivuko si salama kwa abiria kwanini msiache kupakia hata hao waendesha baiskeli,au wakiegesha vyombo vyao washuke wasubiri MV Kigamboni kiwavushe ili waweze kutoa vyombo vyao vya usafiri.
 
Si salama kwa abiria wasio na hivyo vyombo vingine yaani watembea kwa miguu
 
Mv LAMI sio salama hata kwa magari kina mlima mkali pale langoni unavyoingiza gari au kushuka ni lazma gari itaparuza chini hasa gar ndogo
 
We umeshaambiwa si salama bado unakomaa, tukusaidiaje sasa? Tusipende kua watu wa kubishana na maelekezo kile siku, hata ajali nyingi zinazotokea pale ferry ni kwa sababu ya ubishi na ujuaji mwingi wa wengi wetu
 
Hivi kuna anayefahamu ile mv kigamboni ina uwezo kubeba watu wangapi kiusalama? yaani kulingana na ilivyosanifiwa?
 
Back
Top Bottom