Tumelia sana, tumeomboleza sana, tumesikitika sana, sasa tuamke usingizini kuanzia Leo.
✍🏿 21/05/1996 tulipatwa na janga kubwa sana la kuzama kwa MV Bukoba iliyo tengenezwa tangu 1979 ikawa imefanya kazi kwa miaka 17 ndipo ikazama ziwa Victoria.
✍🏿MV Bukoba ilikua na uwezo wa kubeba watu wasiozidi 430, na mizigo tani 850, taarifa zinasema miili 391 iliopolewa 495 haikupatikana kwani ilikua imebeba watu zaidi ya 1000. Tume ya Uchunguzi iliundwa na kuja na mapendekezo yao yatokanayo na uchunguzi wao.
✍🏿 Tarehe 10/09/2011zaidi ya watu 2000 walizama katika ajali ya MV Spice Islender iliyokua ikifanya safari zake kuelekea Zanzibar ambapo watanzania wengi sana walikufa maji.
✍🏿Miezi 10 baadae baada ya ajali ya MV Spice I slender, ajali mbaya ikatokea kwenye MV Skagit siku ya 18 Julai 2012 ilikua ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar.
✍🏿Meli hii ya MV spice Islender ilizama katikati ya Mkondo wa Nungwi huku ikiwa imebeba watu 2470,kinyume kabisa na uwezo wake wa kubeba abiria na mizigo, hivyo bado watanzania walikua wana machungu ambayo yalikua hayajafutika akilini mwao.
✍🏿Serikali ya Zanzibar iliunda Tume ya Uchunguzi wa ajali hiyo, tume ikiwa chini ya Jaji Abdulhakim Ameir Issa, ikiwa na wajumbe 10, walipewa madodoso ya kuzingatia ikiwa ni pamoja na;
Kuangalia chanzo cha ajali, Idadi ya waliokuwemo chomboni, kubainisha aina na uzito wa mizigo, taratibu za ulipaji fidia kwa waliopatwa na maafa, sifa na uwezo wa mabaharia waliokua wanaoongoza chombo, sheria, kanuni, na taratibu zilizo vunjwa, watu waliotenda makosa hayo na hatua za kinidhamu.
✍🏿Lakini pamoja na matokeo ya tume hiyo na mapendekezo yake ya muda mfupi na mrefu Tume ilikua na udhaifu mmoja tu kwamba ilisheheni Wataalam wa Sheria na Wataalam wa Mambo ya Baharini, bila kujumuisha Wahandisi(Mechanical& Marine Engineers), Mathematicians, Computer Engineers, kama ilivyokua tume ya iliyoundwa 1912 kuchunguza meli ya TITANIC kwani ilichukua watalaam wabobevu kutoka katika taaluma mbali mbali.
✍🏿Pamoja na hayo tume hizo zilizoundwa kuchunguza matukio yote matatu zilikuja na mapendekezo mazuri kabisa juu ya ustawi wa safari za majini, moja ya mapendekezo ilikua ni kubadirisha jina la kikosi cha KMKM kuwa ni Navy Squared. Ili kuongeza ufanisi wa kuokoa pindi matatizo yatokeapo majini.
✍🏿Tarehe 20/09/2018 ajali ya kutisha kupitia MV NYERERE iliyoondoka na Watanzania zaidi ya 235 huku 41 tu wakisalimika, imerejesha majonzi upya lakini pia inatupasa kuamka kutoka katika usingizi mnono wa Pono ambao TEMESA, SUMATRA na vyombo vingine vya serikali vilikua vimeuchapa kwa muda mrefu.
✍🏿Ni rai yangu kwamba kila mtendaji wa serikali aende akasome ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 itamkumbusha dhamana aliyopewa na wananchi, kwa ibara hii ilipaswa vyombo vya serikali viwe vimeokoa zaidi ya wananchi 40 kuliko kuokoa MTU 1 huku vikizidiwa na wananchi.
✍🏿Baada ya tukio la MV Nyerere ni wakati sasa wa mamlaka ya uteuzi kuangalia uhalali wa zoezi la uokoaji wa wahanga kusitishwa jioni ya SAA kumi na mbili eti Kisa Giza. Kwamba hakukua na uwezekenao wa kusogeza generator kubwa zenye uwezo wa kuzalisha umeme kijiji kizima ili wawamlike mwenzetu.
Ni wakati wa kuangalia uhalali wa kuchelewa kufika kuokoa wahanga tangu saa nane Mchana.
Ni wakati wa serikali kuchukua hatua kwa kuzingatia, idadi ilianzaje kufika 200 + ikiwa chombo kina uwezo wa kuchukua watu wasio zidi 101.
Paangaliwe inakuwaje hakuna kamandi ya majini ikiwa wanajua fika tume mbali mbali zimewahi kutoa mapendekezo hayo, au tunajisikia raha kuunda tume, zikalipwa fedha halafu report zao zinafungiwa ndani kama desa tu?. Nafikiri tume hii inayoundwa itakuja na robo 3 ya findings ni zile zile za zamani, na mapendekezo yatafanana tu na tume ya Jaji Abdulihakim Ameir Issa.
Nimeona Jana mheshimiwa Rais kavunja Board ya TEMESA, SUMATRA, mwanzo mzuri wa uwajibishaji, lakini pia nashauri kila aliyehusika kwa uzembe huu basi awajibishwe accordingly na busara sio mpaka watumbuliwe, wachukue hatua wajitumbue wenyewe.
✍🏿Nimesema MV Nyerere ituamshe kwa sababu, Leo hii huwa najiuliza hivi maana ya Mwendokasi ni nini? Mimi nilikua nafkri ni mabasi kwenda kwa mwendo sana tofauti na mradi wa Mwendokasi wa Dar es Salaam, ambao magari yanakwenda kwa kasi huku yakiwa yamejaza watu kupita kiasi, mpaka milango inashindwa kujifunga hivi hii ndo maana ya Mwendo kasi? Tunataka nalo hili watu 300 wave ndipo tuomboleze tena kama taifa?
Nimewahi panda Kivuko cha Kigamboni, kinajaza sana watu mpaka sehemu ya kupakia gari hivi nacho tunasubri kizame kwanza ndipo tuje tuomboleze baada ya hapo tutakua tumejifunza?
✍🏿Upeo wangu unanituma kama kuna waziri wa uchukuzi siku moja acha V8 ofsini panda mwendokasi baada ya hapo ujiulize kwamba kwanini mabasi Yale wameweka seat? Na kwanini watu wanashindwa hata kuhema? Na limits ya kubeba abria mabasi Yale ni ngapi? Je tunajiandaa kumwajibisha mkata ticket? Anaeangalia TSh650 na siyo uhai wa anaetoa TSh 650? We have to back in our senses.
✍🏿Huu ni wakati wa, kununua vifaa maalumu vya uokoaji, kutengeneza Navy squads,Jeshi la Zima moto na uokoaji ambao watawaokoa kwa ustadi wa hali ya juu, watanzania wakati wa hatari na majanga kama haya ya MV Nyerere na yaliyo tangulia.
✍🏿 Huu ndo wakati wa kuhakikisha sheria za usafiri zinafuatwa ipasavyo, kama mnaweza kuzuia watu wasipige picha wakiwa kwenye vivuko, nafkri mnaweza zuia na idadi ya watu wanaotakiwa kusafiri, hili liwe kwa boda boda, bajaji, dala dala, mabasi ya mikoani vyombo vya majini na angani.
✍🏿Ajali zibaki za asili yaani mfano breki zimefeli, au tyre ilikua mpya imepasuka (haya tunaweza sema ni natural calamities/disaster) siyo abiria wamezidi, au chombo kibovu kimeruhusiwa kusafiri, hatutawaelewa.
✍🏿Wakati wa misiba ieleweke kila mmoja hulia kivyake, viongozi wa kisiasa, na mawaziri ni vema mkatambua hilo, tusiwapangie watu namna ya kulia.
✍🏿Wapo watakalaumu, wapo watakao sema vibaya, wapo watakao andika kwa hisia Kali kuonyesha uozo uliosababisha ndugu zao wapoteze maisha, viongozi lazma wawavumilie huko ndo kuomboleza, msibani wapo ambao hulia kwa kuwakumbka marehemu, wengine hutukana kabisa kwa uchungu.
✍🏿Hebu fikiri unaenda hospital daktari anashindwa kwa uzembe wake, kumhudumia mkeo anahitaji kujifungua, baadae ukapoteza mama na mtoto hivi unapolia utakua unasemaje? Hivi akaja MTU akakuambia nisisikie unalia nitakuchukulia hatua so what? Viongozi mnapokumbushwa kuacha uzembe wa kiutendaji msiwakoromee wananchi, kwanza tambueni hao ndo waliowaajiri kwa kuwapa dhamana ya kuwaongoza.
Mwisho lakini sio kwa umhimu, matukio mazito kama ya misiba, yasitugawe kisiasa, yatulete pamoja tulie pamoja, tukubaliane kuboresha kwa manufaa ya wananchi wetu.
Naamni janga la MV Nyerere litakua ni la mwanzo na mwisho labda itokee kama tendo la Mungu (Force Majeure) na sio haya ambayo binadamu wanayasababisha kwa uzembe wao.
Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki watanzania, waishi kwa upendo, ukawe faraja kwao katika kipindi hiki kigumu.
Emmanuel Chengula