Muyafahamu haya......U..,U...,U...

Habari waungwana JF!
Hizi ni maana ya Uganga.Uchawi&Ushirikina.
Loh! Jamaa wengi utawasikia wakilalamika na kutoa maelezo mengi kuhusu mambo hayo...
Sasa tuanze kuyaelezea...
1-Uchawi ni nin?
2-Ushirikina ni nini?
3-Uganga ni nini?
Nawakilisha.

Maalim Jumaar..ni cousre ipi kati ya hizo tatu unataka kusomea au unasomea maana naona kunakusanya data kwa ajili ya presentation
 
basi kama yupo jamaa wa FFUnit...wape hii thread wachangie..niujue Uchawi,Ushirikina;Uganga.
Maana hua napata taabu kusikia na kuona watu wengi wakielezea kumbe hata maana hawajui...!
Hata ww huenda usijue...so humu tukusaidie kuyajua.
 
Je kila mganga wa kienyeji anajua uchawi ? Na kila mchawi ni mganga wa kienyeji ?
 
Je kila mganga wa kienyeji anajua uchawi ? Na kila mchawi ni mganga wa kienyeji ?
 
Je kila mganga wa kienyeji anajua uchawi ? Na kila mchawi ni mganga wa kienyeji ?
Vizuri ujue maana ya uganga. huo uchawi ni nin?
Kwa mimi naona hapo kuna vitu viwili.1-Uganga. 2-Uchawi.
 
Maalim Jumaar..ni cousre ipi kati ya hizo tatu unataka kusomea au unasomea maana naona kunakusanya data kwa ajili ya presentation
Naanza kuweka uwazi na ufafanuzi wangu hapa.
Maana nimesubiri maelezo na maswali ili kuweka uwazi imekua natolewa nje ya mada yangu.
1-Uchawi ni maarifa yeyote yalio zaidi ya akili ya kawaida.
Hivyo wachawi ni wengi. Ubaya wa uchawi ni pale mtu 1 au kikundi kingine kitautumia/kutumia maarifa yao kuumiza mwenzie/wenzake. Wenzetu weupe wanaita uchawi upo aina mbili...wenye faida kwa wengine....na ule usiofaida kwa wengine.
Lakin uchawi kwa undani zaid umeelezwa kwenye vitabu vya imadi za dini zaidi.
Hapa nimeeleza kwa ujumla faida na hasara za uchawi. Kwenda kwa mganga wa asili/kienyeji si uchawi....labda huyo mganga afanye vitu vya kudhuru wengine ni uchawi usiofaa. Lakin kuomba mvua ikanyesha itapohitajika huwez sema ni uchawi mbaya...ilhali umeleta faida. Mbaya ni kuomba mvua inyeshe iharibu mazao ya wakulima.
 
Kwa kawaida uchawi siri...na hufanyika sehem ya siri.
Kwa kawaida mchawi hufanya kiroho zaid(spiritual) baada ya maombi yake au vitendo vyake...ndipo huleta madhara ima ya kuonekana au yasionekana. Mwanadam anporogwa na mchawi...hupata madhara aina mbili ya kiroho pili ya kimwili. Hili la kiroho itakua gumu kumuamini kwa kua alierogwa atakua anatuelezea zaidi yale anayohisi yeye...nasi kwa kua hatuyaoni anayohisi itakua vgumu kuyaamini maelezo yake.
La pili la kimwili ni ragisi kumuona na kuamini. Kama alieanguka akatoa damu,akavunjika mguu n.k. Si lazima kuamini kitu hadi kikutokee mwenyewe ...ni vzuri kuamin kwa ushahidi wa kile umeambiwa na unaemuamini.
 
2-Ushirikina ni neno la lugha ya kiarabu lenye maana ya kushiriki(partnership) unaweza kua ww na mwenzi wako mkaitwa washirikina. Lakin maana kubwa inayotumika hapa ni kiimani zaidi. Yaani kumfananisha Muumba na viumbe kua na uwezo au ushirikiano wa sawa. Ndio inaitwa ushirikina kwa kua utakua umechanganya uwezo wake Mungu na viumbe vyake. Ni imaan mbaya kabisa na lazima ikemewe kwa hali yeyote iwayo.
Kwenda kwa mtaalam /mganga hasa watiba za asili si ushirikina. Ushirikina ni vitendo ambavyo vinaweza kufanywa na mtu yeyote hata pasipokwenda kwa mganga wa asili/kienyeji. Iwapo mganga wa asili/kienyeji atafanya kujifananisha uwezo wa dawa zake au maarifa yake na uwezo wa Muumba hapo atakua nae ni mshirikina.
 
3-Uganga ni jambo lolote zuri unaloweza kulifanya kwa mwenzio/wengine. Pia unaweza ukafanyiwa na mwenzio/wengine. Lakin wengi wamezoeshwa kwenda nje ya hospitali za sasa ndio uganga na ni jambo halifai. Hiyo si kweli ni propaganda za kudharau tiba zetu na kujali tiba za sasa. Hili limeweza kujaza ujinga wengi....bila kuangalia row material zinapatikana kwenye vitu asili...ambavyo ndio mtaviita mizizii/mbegu/matunda n.k.
Mara nyingi hawa waganga wa asili/kienyeji wamekua wakichukiwa zaidi pale wanapoelezea chanzo cha matatizo bila kua na kanuni halisi...(ramli) japo neno hili lina aslia ya lugha ya kiarabu lenye maana ya udongo(changa) japo ilmu hiyo ya ramli inayo asili ilipoanzia.
Pia kumekua na ikhtilafu kwa wasomi wa ilmu za dini juu ya swala hilo. Pia ni tafauti tu za kuelewa lugha. Hivyo ni vzuri kueleweshana zaidi undani wa mambo hayo na kuyajadili bila hasira. Pia imezoeleka kwa fulani hapatii vizuri au unamchukia kwa kua ni mjuzi wa ilmu hiyo na yeyote ataekua mjuzi wa ilmi hiyo hafai. Si kweli hiyo.
 
Back
Top Bottom