Muvi na series zilizoandikwa vizuri

Maelezo ya spoils of water tafadhali
You kno I like to explain 🤣🤣🤣

Ipo hivi...
Spoils of wars hua inamaanisha vitu fulani vilivyochukuliwa vitani. Eg; Tz ikipigana na Kenya ikashinda vita basi ichukue vitu itakavyoona vinafaa labda tuseme michele, mifugo,pesa, dhahabu nk. So vitu hivyo vilivyotoka vitani ndio huitwa spoils of wars!

Kama uliangalia vizuri hiyo episode, Jaime &Bronn akiwa na jeshi lake la Lannister walienda kuvamia mji wa High Garden nyumban kwao Lady Olena na Margery Tyrrell. Jaime akamwambia lady olena serci kanituma nikukamate nikupeleke akutese na kukukata kichwa, ila jaime akasema kwa heshima yako nakupa chaguo ujiue mwenyewe. So olena akanywa sumu, but just before that alimwambia jaime "Tell serci i want her to know that it was me" kwamba yeye olena ndio alimuua Jofrey kwa sumu.

Baada ya olena kufa walichukua madhahabu na vitu vingine vingi wakawa wanarudi navyo. Hivyo vitu ndio spoils of war, hence jina la episode. Daenerys alivyofika na dragon wake alichoma mizigo yote waliyokua wamebeba kutoka high garden
 
Better call saul wanaiweka Netflix,.my favorite ni Breaking bad,na one tree hill
Mkuu how BCS waiweke netflix wakati ni mali ya AMC???
Nakubali bcs iliandikwa vizuri binafsi mm ni mpenzi wa black comedy. Hicho ilinifanya niipende sana
 

Bronn alimwambia tukimbia bwana
jamaa akijibu “we’ll hold them off” afu mzee baba akaunguruma kusikia mlio wa Dragon hawakuamini
aiseee its one of my fav Episode
 
Bronn alimwambia tukimbia bwana
jamaa akijibu “we’ll hold them off” afu mzee baba akaunguruma kusikia mlio wa Dragon hawakuamini
aiseee its one of my fav Episode
Moja kati ya episode bora zaidi dunia ndio naipenda zaidi. Ni S6Ep9 War Of bastard. Mpambano kati ya Jon na Ramsey.

Bronn baada ya kuona dragon alikimbia akaaunguka kumbe alikua kaficha kifuko cha dhahabu. Jamaa alikua anajali pesa tu
 
 


Haya sasa kabishane na wataalamu wa International Movies Database - IMDB

Wewe shida huwa ni kajuaji fln hv af narcissism inakusumbua, ukiongezea na magical thinking yako unadhan kila opinion yako ni global opinion.

Kaniletee poll kutoka global movie community yyt ambapo GOT kaizidi Breaking Bad na mimi nitakuonesha namna nguruwe anavyotaga mayai kama kuku. Na usipo nielewa hapo ndo basi tena.
 
Blindspot!
Hii ilinishinda kutazama, maybe nitaipa muda.

The Vampire Diaries
Moja kati ya series maarufu za zamani ila nzuri sana. Binafsi niliingalia kwa kufuata maneno ya watu kwenye pages za series. Niliitazama nikawa naona inaniboa coz hua sipend sana mambo ya supernatural unless yawe Based on true story. Ila baada ya muda kuna character walianza kunivuti.
  • Damon Salvatore; Ubaya ubaya tu jamaa alikua anamnyanyasa mdogo wake. Ni aina ya watu wanajifanya hawajali ila anajali sana kimya kimya, utamchukia sana kwenye S1 ila mbeleni utampenda. Napenda facial expressions ya uigizaji wake yaani kama vile haigizi Kumbe yupo mbele kamera

  • Ellijah Mikaelson; Huyu jamaa ni aina fulani ya watu very loyal. Anaheshim sana makubaliano akitoa ahadi anaishika. Anaijali sana familia yake (The Originals) hua tunamuita Elijah the noble. Halafu ongea yake ya kijentlomen, hana haraka kabisa. Nilianza kuboreka S2 ila alipoonza kuonekana Elijah ilibid niendelee coz alinivutia sana uigizaji wake.

  • Klaus Mikaelson; Huyu ndio adui mkuu kwenye series ila utajikuta unampenda kuliko sterlings. Akitaka kukuua anakuambia kabisa halafu kazi kwako sasa maana lazima itimie atakachosema. Very gentleman na lafudhi yake ya kibritish.
 
Zingatia kichwa cha uzi na Lengo kuu lake. Sio kutafuta series ipi bora bali zile zilizoandikwa vizuri zitajwe.

NB:
Unapenda sana kuniattack personally kwamba mm ni mjuaji, narcissist and other blah blah. Ajabu ni kwamba unaendelea kunifuatilia na kufungua kila nyuzi nazoanzisha. Kama hunipendi just ignore me hutaniona tena hapa jf, sikumbuki kama nishawahi kukuQuote, wala kukutag kwenye mada yoyote iwe yangu au ya mwingine. Kwanini usumbuke na mtu usiyempenda?? Masna binafs nilikua sikujui kama unaExist hapa jf mpaka ulipoanza kuniattack personally kwenye nyuzi nazoanzisha.

Weird-O!!!!😤😤😤😤
 
We dogo una matatizo sio bure.

Kwanza sijaanza kukuquote, wewe ndo umeanza. Nimeandika comment ya kawaida ww ukaniquote

Pili, sikujua huu uzi umeanzisha wewe ningejua nisingepoteza hata time kuandika comment yangu.

Hadi hapo nani kaanza kumfuata mwingine? Acha upuuzi na utoto, umekosa point unaanza kutafuta huruma, ngoja nipress kabisa hio ignore button nisiendelee kuona trash zako.
 
Machaguo ni
-Behave
-Ni Ignore mimi.
Usipochagua kati ya haya basi nitakuchagulia mimi
Nitaku Ignore wewe. Ushajua uzi ni mm nimeanzisha ila bado upo.
 
Mkuu how BCS waiweke netflix wakati ni mali ya AMC???
Nakubali bcs iliandikwa vizuri binafsi mm ni mpenzi wa black comedy. Hicho ilinifanya niipende sana
mambo ya fedha mkuu,me nimeangalia season 6,and walisema wataweka yote but haitakua forever..
 
Msifanye mchezo na Game of thrones nyie? Yani mpaka HBO wameamua kuitolea mini series House of dragon kile chuma akijawai kutokea Toka dunia kuumbwa ndio series iliyoingiza pesa ndefu sana ni balaaa Ile series..
 
Tyler Perry is trash. Kuanzia movies mpaka series.
 
Moja kati ya episode bora zaidi dunia ndio naipenda zaidi. Ni S6Ep9 War Of bastard. Mpambano kati ya Jon na Ramsey.

Bronn baada ya kuona dragon alikimbia akaaunguka kumbe alikua kaficha kifuko cha dhahabu. Jamaa alikua anajali pesa tu

na S6Ep9 ni kifo cha Ramsey pia
yule mwamba ni katili sana ilitakiwa azaliwe na Joffery tumbo moja
 

niliangalia Hii kwa Trend Pia tena kipindi nipo o level
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…