Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,780
- 107,339
Kuna wakati unaweza kusoma kitu ukabaki unajiuliza mambo mengi sana juu ya mwandishi wa kitu hicho. Aliwaza nini,alipata wapi hii stori,ana akili yenye uwezo gani hadi kuandika kitu hiki. Basi ndio maswali mengi ambayo hua najiuliza juu ya huyu George Raymond Martin kutokana na uandishi wake wa collection ya vitabu vya A song of Ice and Fire almaarufu kama Game of thrones.
Huyu mzee alijitahidi na tunaweza kumwita moja kati ya wanadamu walioweza kutumia akili zao vizuri katika kufikiria vitu extraordinary. Lakini pia kuna genius mwingine anaitwa J.R.R. Tolkien, huyu jamaa ni hatari sana katika uandishi wa High Fantasy kwakweli nashindwa kuelewa kati yake na George nani mkali zaidi kaandika novel kama The hobbit,The lord of the Rings,The Slimarillion,Unfinnished tales etc. Hawa watu wawili ni definition ya kuwa Genius and critical Thinker. Ila wengi wanakubali Tolkien ni bora zaidi kuliko George.
If you think this has happy ending, you haven’t paying attention
-Ramsey Bolton
Mwezi wa sita mwaka 2006 Agent wa George martin alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwake kwa jina la David Benioff, akamwambia kua alikua yupo interested na novels za A song of Ice and Fire amesikia wengi wanavisifia kua nivizuri, japo yeye ni mpenzi wa fantasy novel ila hajawahi kuvisoma vitabu hivyo! Yule Agent alimtumia vitabu vinne, david alisoma kurasa mia za kitabu cha kwanza kiitwacho A game of thrones . kisha akampatia rafiki yake D.B.Weiss kitabu hicho akisome, ndani ya masaa 36 D.B. Weiss alikua amemaliza kitabu chote.
David Benioff anasema kwamba hadi martin kuwakubalia kutengeneza series aliwauliza swali linasema Nani ni mama wa Jon Snow ? wakafanikiwa kulijibu kutokana na mahesabu Fulani waliyopiga ambayo ni R+L = J (Rhaegar +Lyanna = Jon) Martin alikua amewaambia kua mama wa Jon anaweza kua mtumishi aitwae wylla au mwanamke kutoka familiatajiri aitwae Ashara Dyne..Walipoweza kuchekecha akili wakagundua Jon si mtoto wa Ned bali wa dada yake Lyanna..Martin alithibitisha kwamba hawa watu wana akili so akawapa Go ahead ikumbuke kwamba wakati wanauliza swali hilo walikua hawajasoma vitabu vya mbele vinavyoonyesha kua jon hatoki ukoo wa stark
Kazi ikaanza sasa ya kutengeneza series, david na Weiss ndio wameandika scripts na kuongoza episode nyingi zaidi. Martin yeye kuanzia season 1-4 kila episode ya kwanza yeye ndio alikua anandika scripts na dialogues. Baadae ilibidi aache kuandika maana alitaka aweke nguvu zaidi kumalizia kitabu (mshenzi sana huyu jamaa ana arosto mbaya, miaka kumi sasa ila hajatoa hicho kitabu cha The Wind of winter) ila alikua anapitia sripts zote na kuzisahihisha kabla ya kuwa approved…David na Weiss walikua wanaajiri mwandishi mmoja wa script kwa baadhi ya waigizaji. Mfano Brayn Cogman yeye alikua ni mahususi kuandika script za Arya stark tu.
G.R.R. Martin katengeneza dunia ya kufikirika kupitia uandishi wake, D.B.Weiss na David Benioff waliungana na George Martin kuteletea Tamthilia nzuri na inayopendwa na watu wengi zaidi duniani “Game of Thrones” katika series kali nilizowahi angalia basi 1.GOT 2.Prison Break 3. 24hours. Kinachowavutia watu kwenye hii series sio mapigano au sex scene ila ni story line yake ilivyo.
Katika kitu walichofanikiwa hawa jamaa katika kuandaa hii series ni kwamba hata ufanye huwezi kutabiri tukio lolote lijalo pia humu ndani mtu yoyote anaweza kufa muda wowote hata kama ndio sterling. Kama unataka kuangalia hii series basi ule msemo eti sterling hauawi basi sahau..Even Jon snow alikufa,Danny alikufa Ned,Rob nk … Lakini pia Character Development, wameaanza na waigizaji wengine bado wadogo kabisa wakawa nao hadi mwisho wamekua watu wazima kama Bran,Sansa,Arya,Jon, nk
Lakini uwezo wao mkubwa wa Weiss na Benioff umekithirika kwa jinsi walivyoweza kutengeneza lugha mbalimbali zilizotumika ndani ya series kama lugha ya Dortharaki,High Valerian, rafudhi mbalimbali…Halafu kila mwigizaji ana ana slang yake na aina ya maneno anayongea kwa kingereza kigumu hasa mfano jinsi anavyoongea Jaqen H’egar ni tofauti na watu wengine, Sendor clagne ana maneno tofauti kabisa ya kibabe kidogo wanataka kufanana na Bronn maana wote wakiongea lazima waweke neon https://jamii.app/JFUserGuide. Ila sehemu walipotumia akili kuhakikisha kila neon linaloongewa lazima liwe point ni kwa maneno anayozungumza Varys na Tyrion Lannisters.
Ukianza kuitazama usianze kuchagua waigizaji waliokuvutia,subiri ufike hata season ya 5 huko ndio unaweza kupata mwanga maana muda wowote muigizaji unayempenda anaweza kufa, mimi mwanzo kabisa nilimpenda jon snow,Arya na Robb halafu nikajua Ned ndio sterling kumbe hata season 2 hafiki anakufa mapema sana.
Kwenye hii series unaweza ukampenda mtu baadae ukamchukia sana halafu baadae ukampenda tena mfano theon greyjoy nilimpenda mwanzo alipowageuka starks nikamchukia sana akatekwa na Ramsey nikampenda Ramsey ila baadae nikaja kumpenda zaidi theon kwa aliyoyafanya kulipa deni la usaliti. Katika series kuna watu utawachukia sana sana hasa King Joefrey (huyo nimemchukia kabisa sitaki kuona muvi yake yoyote) na Ramsey huyu jamaa anakera mno asee. Halafu ypo kama joker anakuua yupo anakutania (alimuua baba yake akawa anasema baba yake ameuawa kwa sumu na maadui wakati watu wameona tobo la kisu).
Mwingine ni Sercie huyu ndio mtu anayechukiwa zaidi katika series maana yupo mpaka mwisho mashabiki wa GOT walikua wanamtukana kabisa live live na kuwaandikia waandaaji wa series kua hawampendi ikabidi Lena Hadey atoe tamko kua ni uigizaji tu ila hana roho mbaya kama watu wanavyomuona ndani ya series as sercie (Mimi nilimpenda kwenye muvi ya 300 na 300:Rise of Empire pekee) Sikuamini kama Robb na mkewe (Oanna Chaplini mjukuu wa Charlie chaplin) watakufa yaani niliumia sana kama kweli vile. Season 8 episode 3 niliingalia nikiwa ninahofu kuu maana muda wowote waigizaji ninaowapenda wanaweza kufa… Kiufupi huwezi tabiri lolote katika series hii hta kidogo
Ni series inayopendwa na maarufu wengi wakiwemo Queen Elizabeth na Barack Obama, Wakati wanashoot season 7 nchini Ireland malkia alikua huko ikabidi aende location kuwatembelea waigizaji yeye malkia favourate actor alikua Arya stark, Alipofika waandaaji wa series wakamkaribisha akalie kile kiti cha Iron Throne ila alikataa.
Why? Malkia wa Uingereza haruhusiwi kukalia kiti kingine chochote kinachoitwa Throne/Kiti cha ufalme tofauti na kile anachokalia yeye rasmi. Hata hiyo kigoda/stuli yako ukiita Throne bas kwake ni mwiko kukalia. Obama ndio alikua mshabiki li alia wa series hii Jon snow akiwa ndio favourate characters, Mwisho wa season 5 inaonyesha Jon snow kauawa unaambiwa Obama alipaniki hadi akapiga simu kabisa kwa waandaaji wa series akaomba kujua hatima ya Jon snow baada ya kufariki.
Season 6 ilipotoka tu Obama ndio alikua mtu wa kwanza kuiona maana aliomba apewe episode One inaitwa the Red Woman ambapo Priestess Malissandre alimfufua Jon Snow. Hata season 7 ilipotoka Weiss na Benioff walishajua Obama ni shabiki mkubwa hivo walimpelekea season 7 yote yeye ndio akawa tena mtu wa kwanza kuangalia season 7.
Sasa wewe upo tandale mabondeni huko hujui hata jioni utakula nini unaangalia hii series kwenye tv yako ya chogo tena imetafsiriwa hafu unaangalia vipande kadhaa unasema ni mbaya, haieleweki wakati watu wakubwa ambao wanajua ndani ya mwezi mzima watakula nini wanaipenda na kuifuatilia.
Be careful ukiangalia wanatumia kingereza kigumu cha kizamani, hasa akiongea Tyrion ana misemo yake ambayo usipokua makini humuelewi..Na Ser davos hua anaongea haraka haraharaka. Mambo makubwa niliyojifunza kwenye hii series ni LOYALTY