Muuzaji wa M-PESA na msimamizi wa kituo wanahitajika

MNAFU

Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
99
Reaction score
24
Habari zenu wana jamiiforums,

Kuna nafasi za kazi 4 kwa ajili ya wauzaji ktk ofisi zinazotoa huduma ya Mpesa, Tigopesa, Airtel Money na kuuza LUKU pamoja na kuuza gesi – ORYX Gas. Ofisi zote ziko ktk maeneo tofauti katika jiji la Dar es salaam.
Sifa za mwombaji:

1. Awe kijana wa kiume na awe amemaliza kidato cha 4 na kuendelea
2. Uwezo wa kuelewa, kuandika na kusoma kwa haraka
3. Uwezo wa kufanya mahesabu bila kubabaika
4. Awe mchangamfu kwa wateja lakini mwenye kuelewa wajibu wake wa kulinda na kutunza mali za ofisi.

Mshahara: Ni maelewano kutokana na sifa na ujuzi wa mwombaji.

Marupurupu: Mfanyakazi atapata allowance ya kila wiki kusaidia kupunguza makali ya maisha na hii ni nje na mshahara wake.

Kuishi: Mwajiri amepangisha nyumba/chumba kwa ajili ya malazi ya wafanyakazi wake. Kwa hiyo mwombaji anatakiwa kuwa tayari kuishi na wenzie/mwenzie wa jinsia moja.

Pia anahitajika msimamizi (1) wa vituo hivyo vya mauzo mwenye sifa zifuatazo:

1. Awe kijana wa kiume na awe amemaliza kidato cha 4 au 6 na awe na cheti au diploma ya mambo ya fedha au uhasibu.
2. Uwezo wa kusoma, kuchambua na kutengeneza mahesabu ya mapato na matumizi.

4. Awe mwenye kuelewa wajibu wake wa kazi, kulinda na kutunza mali za ofisi.
5. Awe na uwezo wa kuongoza timu ya watu walio chini yake (Leadership skills)
6. Awe na uwezo wa kutunza kumbukumbu na nyaraka muhimu za ofisi.

Mwenye uzoefu atafikiriwa zaidi.

KWA ANAYEHITAJI MOJA YA NAFASI HIZO TAFADHALI PIGA SIMU NA. 0685847144 ILI NIKUUNGANISHE NA OFISI HUSIKA (MWAJIRI).
 
Mkuu Ahsante. Mbona hizo nafasi zinabagua akina Dada. Unataka wanaume tu kwabi kazi ya kubeba zege?
 
Hapana sio kazi ya kubeba zege. Akina dada wanazifanya vizuri kazi hizo ila baadhi ya vituo hivyo unakuta tayari kuna mtu 1 (mwanamume) ambaye keshapingishiwa chumba. hivyo ni rahisi kama atapatikana mwanamume ili mwajiri asilazimike kupanga chumba kingine.
 
Akina dada wanakaribishwa pia Mwajiri ataona namna bora ya kufanya.
 
naruhusiwa kuhamia na wake zangu wawili?! ......... maisha magumu jamani,kha!"
 
Dooh na wake 2. Hiyo Kali sana. Nasikilizia majibu maana naweza pata nami pa kuponea...
 
Mkuu nna mdogo wangu wa kike msaaada wa hizo kazi
 
Habari zenu wanajf.
Kuna nafasi za kazi 4 kwa ajili ya wauzaji ktk ofisi zinazotoa huduma ya Mpesa, Tigopesa, Airtel Money na kuuza LUKU pamoja na kuuza gesi – ORYX Gas. Ofisi zote ziko ktk maeneo tofauti katika jiji la Dar es salaam.
Sifa za mwombaji:
1. Awe kijana wa kiume na awe amemaliza kidato cha 4 na kuendelea
2. Uwezo wa kuelewa, kuandika na kusoma kwa haraka
3. Uwezo wa kufanya mahesabu bila kubabaika
4. Awe mchangamfu kwa wateja lakini mwenye kuelewa wajibu wake wa kulinda na kutunza mali za ofisi.

Mshahara: Ni maelewano kutokana na sifa na ujuzi wa mwombaji.
Marupurupu: Mfanyakazi atapata allowance ya kila wiki kusaidia kupunguza makali ya maisha na hii ni nje na mshahara wake.
Kuishi: Mwajiri amepangisha nyumba/chumba kwa ajili ya malazi ya wafanyakazi wake. Kwa hiyo mwombaji anatakiwa kuwa tayari kuishi na wenzie/mwenzie wa jinsia moja.
Pia anahitajika msimamizi (1) wa vituo hivyo vya mauzo mwenye sifa zifuatazo:
1. Awe kijana wa kiume na awe amemaliza kidato cha 4 au 6 na awe na cheti au diploma ya mambo ya fedha au uhasibu.
2. Uwezo wa kusoma, kuchambua na kutengeneza mahesabu ya mapato na matumizi.
3. Uwezo wa kufanya mahesabu bila kubabaika
4. Awe mwenye kuelewa wajibu wake wa kazi, kulinda na kutunza mali za ofisi.
5. Awe na uwezo wa kuongoza timu ya watu walio chini yake (Leadership skills)
6. Awe na uwezo wa kutunza kumbukumbu na nyaraka muhimu za ofisi.

Mwenye uzoefu atafikiriwa zaidi. KWA ANAYEHITAJI MOJA YA NAFASI HIZO TAFADHALI PIGA SIMU NA. 0685847144 ILI NIKUUNGANISHE NA OFISI HUSIKA (MWAJIRI).

Mkuu kama mwanamke anaitaj na kuhusu malazi atajigharamia mwenyewe inakuaje?anaruhusiwa?au hairuhusiwi kabisa
 
NAWASHUKURU SANA WANA JF. TUMEWEZA KUPATA IDADI TULIYOHITAJI. WENGI TUMEWASILIANA NA HATIMAYE WALIOPATA NI BAHATI YAO.

Wale tuliokubaliana kukutana Jumatatu asubuhi naomba tufanye hivyo kama tulivyokubaliana. Ahsanteni.
 
HABARI ZENU WAKUU

KUMETOKEZEA NAFASI 4 NYINGINE ZA KAZI KAMA IFUATACYO:
1. MSIMAMIZI MSAIDIZI - 1
2. WAUZAJI WA MPESA - 3

Sifa ni kama ilivyo ktk mwanzo wa thread hii isipokuwa mwajiri ni tofauti. Kwa msimamizi Msaidizi ni lazima awe na angalau cheti (Certificate ya Uhasibu).

Kwa muuzaji lazima awe amemaliza angalau form four na ana Cheri - Academic Certificate.

Kwa wenye sifa peleka email ya maombi kwa raja4juma@gmail.com
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom