Muuza mayai. Inafundisha sana...

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Alimuuliza, "Je! Unauza mayai shilingi ngapi ?"

Muuzaji mzee akajibu, nauza 500 kwa yai moja, Madam . '

Akamwambia, 'Nitachukua mayai 6 kwa kwa mia tatu tatu au nindoke.'

Muuzaji mzee akajibu, 'Njoo uchukue kwa bei unayotaka.

Labda, huu ni mwanzo mzuri kwa sababu sijaweza kuuza hata yai moja leo. '

Alichukua mayai na kuondoka huku akijiona ameshinda.

Aliingia kwenye gari lake la kupendeza na kisha akaenda kwenye mgahawa na rafiki yake.

Huko, yeye na rafiki yake, waliagiza kila kitu walichokipenda,

Walikula kidogo na wakaacha masalia ya yale waliyoagiza.

Kisha akaenda kulipa bili hiyo.

Bili hiyo ilimgharimu elfu 80, na alitoa laki moja na na kumtaka mmiliki wa mgahawa, abaki na chenji,

Tukio hili linaweza kuonekana kuwa la kawaida kwa mmiliki lakini, chungu sana kwa muuzaji yule mzee maskini muuza mayai.

Jambo ni kwamba, Kwa nini kila wakati tunaonyesha kuwa tuna nguvu tunaponunua kutoka kwa wahitaji? Na kwa nini tunapata ukarimu kwa wale ambao hawahitaji hata ukarimu wetu?

Nilisoma mahali pengine:

'Baba yangu alikuwa akinunua bidhaa rahisi kutoka kwa watu masikini kwa bei kubwa, ikiwa hata hakuihitaji.

Wakati mwingine hata alikuwa akilipa zaidi kwa ajili yao.

Nilifadhaika na kitendo hiki na kumuuliza kwanini anafanya hivyo? Ndipo baba yangu akajibu, "Ni sadaka iliyofunikwa na heshima, mtoto wangu"

Najua wengi wenu hawatashiriki ujumbe huu lakini ikiwa unahisi kuwa watu wanahitaji kusoma chapisho hili, basi sambaza ujumbe huu japo kwenye vikundi viwili tu,.
 
Swali. Kama bill ilikuwa ni tsh 80,000 kwa nini alitoa 100,000? Lengo la kusema change ibaki lilitoka wapi wakati angeweza kutoa 80,000 tu na hamna note ya 100,000 ambayo sasa ingekatwa tsh 80,000 arudishiwe tsh 20,000? Hapo mi ndo sijaelewa kabisa.
 
Kwani huwezi kutoa sh 50000 wakati unadaiwa 30000 na ukasema hiyo 20000 keep change?? Kipi cha ajabu hapo mkuu??
 
Swali. Kama bill ilikuwa ni tsh 80,000 kwa nini alitoa 100,000? Lengo la kusema change ibaki lilitoka wapi wakati angeweza kutoa 80,000 tu na hamna note ya 100,000 ambayo sasa ingekatwa tsh 80,000 arudishiwe tsh 20,000? Hapo mi ndo sijaelewa kabisa.
😂 😂 😂 😂 😂
 
Mkuu, labda hii ni hadithi ya huko ulaya ambapo mnunuzi alitoa dola mia kwa malipo ya dola 80. Sema tu hapa imetafsiriwa na kuwekwa vionjo vya kiafrika ili kufikisha ujumbe kwa hadhira husika!!

Mimi hivyo ndio ninadhani!!
 
Nimejifunza kitu hapa maana hata mimi muda mwingine uwalalia wenye uhitaji wakati nikienda sehemu nzuri nikakuta mdada mzuri akanipa huduma namwambia keep the remaining balance.
 
Basi alipaswa hat aseme jamaa walikula msosi wa tsh 7,000 wakatoa 10,000 wakamwambia muuzaji keep change.😁😁😁 Ila wakatoa 100,000 muuzaji akahesabu pesa yake 80,000 zikabaki 20,000 mkononi...mteja akasema keep change? Jamaa angemuuliza change gani?

Mkuu, labda hii ni hadithi ya huko ulaya ambapo mnunuzi alitoa dola mia kwa malipo ya dola 80. Sema tu hapa imetafsiriwa na kuwekwa vionjo vya kiafrika ili kufikisha ujumbe kwa hadhira husika!!

Mimi hivyo ndio ninadhani!!
 
Basi alipaswa hat aseme jamaa walikula msosi wa tsh 7,000 wakatoa 10,000 wakamwambia muuzaji keep change. Ila wakatoa 100,000 muuzaji akahesabu pesa yake 80,000 zikabaki 20,000 mkononi...mteja akasema keep change? Jamaa angemuuliza change gani?
We punguza sifuri moja tu kwani tatizo Nini
 
Swali. Kama bill ilikuwa ni tsh 80,000 kwa nini alitoa 100,000? Lengo la kusema change ibaki lilitoka wapi wakati angeweza kutoa 80,000 tu na hamna note ya 100,000 ambayo sasa ingekatwa tsh 80,000 arudishiwe tsh 20,000? Hapo mi ndo sijaelewa kabisa.
Hii ni story ambayo ni translated kutoka lugha nyingine,lakini ujumbe wake ni dhahiri kwa lugha zote.fanya hivi,kwenye shilingi 100000 weka dola 100,na kwenye shilingi 80000 weka dola 80,nadhani utaelewa ujumbe
 
Back
Top Bottom