Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,096
- 22,824
Katika nyakati hizi hizi za miaka hii kulikuwapo na muuza matunda nadhifu na msomi. Ambaye alikuwa mpya katika biashara ya uuzaji matunda sokoni.
Alianzisha biashara kubwa na ya mzigo mkubwa na kuipamba mandhari ya banda lake kwa ustadi wa hali ya juu. Wateja walimiminika kuchungulia bidhaa katika genge lake kwa wingi sana. Katika hali ya kustaajabisha hakuna mteja alitoka na matunda na walitoka na kuja kununua kwa wauzaji wengine ambao hawakuwa maridadi na nadhifu kama huyu muuzaji nadhifu katika mpangilio wao wa bidhaa na mazingira ya magenge yao.
Siku kadhaa za biashara muuzaji akaanza kuona mambo yake hayamuendei vema. Akaona amuone mzee jirani yake hapo ambaye ni muuzaji matunda mkongwe kuliko wote ili amuelezee shida yake.
Muuza matunda nadhifu akamuendea mzee mkongwe na kumuongelesha. "Mzee nimeweka biashara yangu nadhifu kushinda nyote hapa, nilileta mzigo mwingi kuwashinda nyote ila hadi sasa umenidodea kwann? "[emoji36][emoji24]
Mzee mkongwe akauliza ," KWANINI HAUUZI MATUNDA? "
Muuza matunda nadhifu akajibu," wateja huwa wanataka kupewa matunda kwa bei ya chini sawa na mnayouza nyie ila mimi ninajua matunda yangu ni bora zaidi na matunda yanathamani zaidi kwajiri ya chakula, vinywaji, kutengeneza vipodozi na manukato, makapi kulishia wanyama, na hata mbolea. Thamani ya hivi vitu vyote vinabebwa na tunda kwann sasa niuze bei ya chini kama nyie msio jua thamani ya matunda yenu.
Mzee mkongwe akamjibu " Katika miaka yote ya biashara, sikuwahi kumwambia mteja anachotaka ila nilimsikiliza anachotaka na kumpatia. Kichwa chenye masikio yanayosikiliza vizuri hujifunza zaidi kuliko chenye mdomo unaoongea sana, mteja ni mfalme hivyo lazima aonyweshwe utii. Umejaza matunda tofauti gengeni ila mengi ni yale yanayofurahisha nafsi yako kuwa hapo dukani na sio yale wateja wanataka. Unawapangia wateja bei kwasababu ya thamani unayopanga na nafsi yako ila sio makubaliano na wateja. Udongo huko shambani umekupa matunda bure kama ungedai thamani kama namna unavyodai wewe basi usingepata chochote".
Muuza matunda nadhifu akaondoka kwa fedheha na kurejea gengeni kwake na kuamua kuuaza kwa bei nusu na ya chini kushinda wauzaji wengine wote na kutoa matunda ya nyongeza kabisa kama zawadi. Ila hakupata wanunuzi kabisa kwasababu wateja waliokuwa wakija waliomba kuonja matunda na kuyakagua ambayo mengi yalionyesha kuharibika nusu kama sio kuoza kabisa.
Muuza matunda nadhifu akamrejea mzee na kumuelezea kinachoendelea katika genge lake na biashara yake ya matunda.
Mzee mkongwe akamsikiliza kisha akamjibu, " Pale awali ulipoanza biashara wateja walikuwa wakikugombania na kutaka kununua matunda ila uliwagomea kwasababu ulikuwa na msimamo wako binafsi wa kulinda thamani ya biashara yako ambayo uliitengeza wewe kichwani na wao hawakuiona na ndio maana walikuomba muelewane ili uwauzie kwa bei muafaka ila ulikataa kulinda ufahari wa biashara yako na thamani ambayo hata wewe hauitumii na hakuna mteja alisema anaihitaji.
Muuza matunda nadhifu akamuuliza, "kwann sasa hawataki kununua na nimekubali kushusha bei na kuwasikiliza?"
Mzee mkongwe akamjibu, " Wewe upo tayari kununua unachowauzia wateja? Umegundua kuwa kuna hasara inakujia kwa kasi huko mbeleni kwa matunda yako kuharibika, je unahisi ni sahihi wateja watoe pesa zao kununua hasara yako ya matunda mabovu? Biashara huwa ni asubuhi jioni ni mahesabu."
Muuza matunda nadhifu akabakia ameduwaa asijue la kufanya kwa maana matunda yake hayauziki, muda umekwenda na unazidi kwenda, na biashara na mtaji wake unaelekea kuishia hapo.
Hii ni story fupi yenye mafunzo yaliyojificha (Codes).
*Muuza matunda nadhifu= Binti mrembo
*Wauza matunda sokoni =. Mabinti wengine
*Matunda = uzuri wa mwanamke
*Soko la matunda = Maisha
*Wateja wa matunda = Vijana wa kiume wanaotafuta mke.
*Muuza matunda mkongwe = Mwanamke mtu mzima.
*Shambani matunda yanapotoka = Uumbaji wa MUNGU.
* Matunda mabovu = mwili uliopitiwa na wanaume tofauti.