Muungo wa google na wikipedia ni tishio jipya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungo wa google na wikipedia ni tishio jipya

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Nov 30, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kumekuwa na Malalamiko kadhaa ya watu yanayoelekezwa kwa google kwa kipindi kirefu sasa kutokana na baadhi ya huduma zake ambazo nyingi ni bure kabisa lakini hazinufaishi wale waloandaa kazi hizo au kuzizalisha mfano mzuri ni ule huduma yao ya kutafuta vitabu kwa njia ya mtandao ambapo unaweza kutafuta vitabu bure kabisa .

  Kuna huduma ya google earth ambapo unaweza kutumia programu hiyo kwa ajili ya kutembelea maeneo mengi ya dunia bure kabisa na kuna baadhi ya maeneo kuna picha na video za maeneo hayo unayotembelea kwa njia ya mtandao mtu anapotumia programu hii kutembelea sehemu Fulani kwa njia ya mtandao mfano sehemu ya makumbusho wale wenye makumbusho hawafaidiki kwa njia nyingi .

  Hayo na mengine mengi nisingependa kuyaongelea sana kwa leo ila leo napenda kuongelea suala la Kampuni ya Google kuungana na Wikipedia katika shuguli zao kadhaa , tukumbuke kwamba wikipedia ni mtandao ambao watu wanaingia kwa ajili ya kuchangia makala na mengine mengi yanayohusu maisha ya binadamu na viumbe wengine , unapochangia kitu kwenye wikipedia ujue mwingine anaweza kuja kurekebisha ulichoandika au kuongezea umekitoa kwa ajili ya kutumika popote .

  Kwa sababu google imezoea kutoa huduma zake nyingi bure kwa watu wake wameamua kuungana na wikipedia tovuti nyingine inayotoa huduma zake bure pia lakini ambayo itamnufaisha zaidi google kibiashara haswa kwa watu wanaotafuta vitu kutokana na lugha wanazoongea au kutumia zaidi wao .

  Tuchukulie mfano wa google earth ambapo unaweza kutumia huduma hiyo kutembelea maeneo mengi duniani pamoja na kuchukuwa vipimo vya maeneo unayotembelea , kwa kujiunga na wikipedia ina maana siku moja utakapotembelea bagamoyo , pembeni yake utapata makala inayohusu bagamoyo tena kwa lugha yako unayopenda wewe hii itaweza kuvutia watu wenye hoteli na huduma zingine bagamoyo kutangaza huduma zao kwenye sehemu hiyo ya google earth .

  Hapo hapo kwenye programu hiyo ya google earth ina sehemu ya kuonyesha jinsi watu walivyosambaa duniani , kama wataungana na wikipedia kwenye huduma hii ina maanisha sasa unapotafuta bagamoyo kwenye google earth ukapeleka bagamoyo na kusoma makala zao sasa unaweza kuangalia jinsi neno hilo linavyotumika maeneo mengine duniani na tafsiri zake nyingi hii inaweza kusaidia kuleta watu karibu zaidi .

  Bila kusahau huduma kama Twitter , Facebook na mitandao mengine ambayo watu huweka taarifa zao na kuwasiliana na watu wao wengi , huduma zote hizi zinaweza kutumika kwa wakati mmoja ikawa hatari sana kwa watu wengi wale wanaopenda kujificha jificha .

  Pamoja na kwamba tunapenda huduma za mawasiliano zinazotuweka karibu zaidi , inabidi sasa watu wajiandae kwa mambo mengi na makubwa zaidi ambapo maslahi yao yanaweza kuguswa kwa namna moja au nyingine .

  Hayo ni mawazo yangu tu
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Google imeungana na Wikipedia kivipi?
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwenye huduma za lugha na tafsiri
   
 4. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wewe hujui kila Website ambayo unaisearch kupitia google wamelipia Asilimia? fulani wewe?? weka data za kueleweka au umezipata wapi? wamejiunga kivipi lete data
   
 5. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Siyo kweli kwamba kila website unayosearch kupitia google lazima walipe, hiyo ina-aply tuu kama unatangaza biashara yako kupitia google ads otherwise ni bure. Ila google anaweza kukulipa ukiwa na website na kuruhusu ads zake kuonekana katika site yako.
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yes ndio ila kwa nchi nyingi za kiafrika imekuwa ishu kidogo kwenye masuala ya malipo kwa nchi za afrika ya mashariki kenya pekee ndio unaweza kulipwa kupitia citibank zingine zote ni kufuata utaratibu fulani ambapo ni mrefu sana
   
Loading...