Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni batili!

Sideeq

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
2,422
434
Tunaambiwa kuwa Tanganyika na Zanzibar ziliungana lakini hatuna tunachokijua zaidi ya hapo na hata kama kulikuwa na makubaliano ya muunagano basi Muungano wenyewe ni batili kwa sababu zifuatazo:

-Hakuna hati yoyote ya makubaliano ambayo wananchi wa Tanganyika na Zanzibar au wawakilishi wao wanaweza
kuonyeshwa.

-Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar hawakushirikishwa katika maamuzi ya kuungana, hivyo hawashurutishwi
kuutambua.

- Muungano umeleta maafa; umwagaji damu, upotezaji wa mali, uharibifu wa mali, udhalilishaji,ufujaji wa
pesa,vifungo n.k kinyume cha nadharia nzima ya Muungano wa nchi zozote zile, nchi haziungani kwa ajili ya kumwaga
damu,kupoteza mali n.k

Kwa sababu hizi ninawaomba wananchi wa pande zote mbili mupeleke maoni ya kuukana Muungano katika mabaraza ya Katiba.
 
Ndio mana unakaribia kufikia ukomo wake. Wait and see, huu muungano umeshafikia kikomo, you will see it break before you die, unless you die before the time
 
Ikiwa tume hii ya katiba imeweka mambo saba tu yawe ya muungano sasa ile 'Article of the Union' imekataliwa? maana tunaambiwa yalikuwa kumi na moja. Kwa maoni yangu kwenda vinginevo nje ya 'AoU' ni kwamba Tanzania haipo kwa maana ya muungano.
 
Ikiwa tume hii ya katiba imeweka mambo saba tu yawe ya muungano sasa ile 'Article of the Union' imekataliwa? maana tunaambiwa yalikuwa kumi na moja. Kwa maoni yangu kwenda vinginevo nje ya 'AoU' ni kwamba Tanzania haipo kwa maana ya muungano.
Nitaliongezea hili katika sababu za kuubatilisha muungano.
 
Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar hawakushirikishwa katika maamuzi ya kuungana, hivyo hawashurutishwi
kuutambua.
Right.

Na mpaka leo, mpaka kwenye rasimu hii, hakuna ridhaa ya wananchi.

Baada ya kutoa rasimu ya Katiba, Warioba alikaa chini akatoa mahojiano marefu sana na gazeti la Mwananchi.

Ukimsikiliza kuhusu Muungano alisema kwamba, kama ukisema tuanze upya, tuunde Tanganyika tuanze na pande mbili halafu ndio uwaulize wananchi, je wanataka Muungano, na wanataka Muungano wa aina gani, Warioba kasema haitawezekana kuungana kwa sababu kila upande au upande fulani utakuja na masharti ambayo yatakuwa magumu kuya accomodate.

Sasa najiuliza, Mzee Warioba, ina maana huu Muungano ni wa shuruti? Kwamba unakiri kabisa, unasema wewe mwenyewe kwamba left to our own device, tukiachiwa huru kabisa kabisa, tujiamulie letu kuhusu Muungano, Muungano hautakuwa. Kwa hiyo ina maana kwa sababu tulishaingia mkenge (yani mtego Mzee Warioba, kwa Kiswahili cha leo), tushaingia mkenge kwa hiyo ndio imekula kwetu, imetoka hiyo, siyo?

Namshangaa sana Jaji Warioba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom