Muungano uwe wa nchi moja

Muungano uwe wa nchi moja

" hujui kama karibu gulf coutries zote zimejengwa/kuendelezwa na waZanzibari, baada ya mapinduzi wengi wao walipokimbilia sehemu hizo? ikiwa tumeweza kuzi transform nchi hizo kwa nini tusiweze kwetu? serikali moja hata hao madalali CCM Znz hawalitaki hili, sisi sasa tumo kupanga kupangua kuuvunja kabisa huu Muungano. HATUUTAKI kabisa!!"

Aisee, vunjeni hata sie hatuutaki kabisaaaaa! Sijuwi hao wanasias wanaofaidika nao. Kuna vyeo na maslahi wanayoyapata muungano ukiwepo. Lianzisheni wallah tutawasapoti!
 
Eneo la Unguja na Pemba kama ilivyo Mafia kijiografia ni sehemu ya ardhi ya iliyokua Tanganyika...

"nafikiri sahihi kusema eneo lote la Tanganyika lilikuwa ni ardhi ya Zanzibar. sijui wajua kama dola ya Zanzibar ipo kabla ya hiyo yenye kuitwa Tanganyika?"

Pili, asilimia zaidi ya 50 ya wakazi wa Pemba na Unguja asili yao ni kutoka kwa mikoa ya iliyokua Tanganyika, tofauti ya tamaduni imetokana na tawala za kikoloni zilizokuwepo visiwani na bara.

"tupo wenye asili ya kutoka bara, lakini si kwa asilimia kama hiyo usemayo wewe. sijajua hili la utamaduni, nijualo kwa kweli utamaduni wetu ni tofauti kabisa na wa huko Tanganyika, lafudhi, chakula, tabia, nk. wapo waZenji wenye asili ya Tanganyika na bado wanaendelea na mila zao"

Hivi ushawahi jiuliza kabla ya uvamizi wa Waarabu ni kina nani walikua wakiishi katika visiwa vya Pemba na Unguja?

" ulipokuja huo uvamizi wa waarabu uuitao wewe, tayari Waarabu walikuwepo miaka mingi nyuma, tokea asili visiwa hivi ni mchanganyiko wa watu wa makabila mbali mbali tabu kusema nani kaja mwanzo. unajua nani kaupa jina mji wa Dar es Salaam? na ni neno la lugha gani na lina maana gani?"
habari ndo hiyo
 
Aisee, vunjeni hata sie hatuutaki kabisaaaaa! Sijuwi hao wanasias wanaofaidika nao. Kuna vyeo na maslahi wanayoyapata muungano ukiwepo. Lianzisheni wallah tutawasapoti!

bro/sis: sisi tayari tumeshalianzisha zamani, linaendelea na halina kusita hadi kieleweke, support yenu ni muhimu sana kufanikisha hili. ni habari kubwa ipo Znz sasa, japo vyombo vya habari havitaki kuzitoa, kwa kukusaidia kidogo, tembelea "mzalendo.net" utapata mwanga wa jambo hili
 
Paka hakamatwi sharubu bwana kiufupi hatutaki tena muungano haukuletwa na mungu,muungano huu unatambulika makaburini huko!

we ni mpemba asilia,mkivunja muungano na zanzibar inameguka vpande vwili unguja na pemba...
 
Ndugu Watanzania wenzangu. Jambo lisipingika kuwa hoja ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imo mawazoni mwetu karibu kila siku. Mara Watanganyika wanalalamika na mara nyingi sana Wazanzibari wanalalamika zaidi. Wote hawa wanalalamika kwa kuwa kuna nchi mbili na kila moja anaona mwenzake anapata zaidi.

SULUHU YA MATATIZO YA MUUNGANO ni kuwa na NCHI MOJA TU badala ya nchi mbili kama ilivyo sasa. Kwa kuwa na nchi mbili tumesababisha yafuatayo:
1. Malalamiko yasiyoisha
2. Mgogoro wa CCM na CUF uliodumu kwa miaka zaidi ya 10 hivyo kuzorotesha maendeleo,
3. Kuwepo kwa Serikali mbili ya Muungano (ambayo ndani yake pia ziko mbili(Muungano na Tanganyika)) na ya Zanzibar
4. Uwepo wa viongozi wengi. Tunalazimika kuwa na Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu bila sababu hivyo kuongeza gharama kubwa kwenye serikali.
5. Nchi moja kulazimika kuendesha mabunge mawili yaani lile la Muungano na lile Baraza la Wawakilishi.
6. Halama za kamati mbalimbali za pamoja za serikali na za vyama mbalimbali.

Kwa ujumla gharama ni kubwa sana zitokanazo na huu mfumo kuliko faida yake. Wakati tunaangali mchakato wa katibu mpya naomba pia tupate nafasi ya kuuangalia hili suala.

"Ni kweli mkuu wa Zanzibari twaulalamikia sana Muungano huu. kwanza hauna uhalali kisheria, wala kisiasa, ni Nyerere kwa utashi wake aujuao mwenyewe na walokuwa wakimtumia ndio alimlazimisha Father K, tena kwa vitisho hasa ukikumbukia wakati ule siku chache tu baada ya mapinduzi ambayo pia yalipangwa na Nyerere.

Hayo ya Serikali moja yasahau kabisa!! kwa sisi waZnz tulio wengi, imefika wakati tuuvunje kabisa huu wenye kuitwa Muungano (wa kipekee dunia nzima). sisi huku tayari kumekucha, tumo katika harakati zetu za kuuvunja. na haturudi nyuma katu.

Tukimaliza hapo ndio tutaulizana kama tuungane ama la na ni Muungano wa aina gani tuutakao, lakini kwa Muungano huu tulionao, wala msidanganywe, WaZnz HATUUTAKI! tuna sababu zetu nyingi sana za kusema hivyo, sio chuki au ubaguzi kama wengi wanavyodhani."
 
we ni mpemba asilia,mkivunja muungano na zanzibar inameguka vpande vwili unguja na pemba...

"Ba Hamad?, kwani kabla ya Muungano 1964 tulikuwa na mtengano baina ya Pemba na Unguja? zilizopita ilikuwa ni chuki zilizopandikizwa na CCM kwa manufaa yao. na ukweli ni baina ya CUF na CCM sio kama hivyo mlivyofanywa muamini kuwa ni baina ya visiwa NO! Mnapenda sana kumtukuza baba yenu wa Taifa 'Mchonga meno' ukweli sisi huku Znz hatumpendi kabisa, wala hana thamani kwa waZnz walio wengi wetu. mimi nahisi kwa upande wenu ndio mjipange kwani huoni kuwa tumekusaidieni sana sisi nyinyi kushikamana? hata hivyo hatukuombeeni yajiri hayo ni ndugu zetu wa damu twawapendeni."
 
bro/sis: sisi tayari tumeshalianzisha zamani, linaendelea na halina kusita hadi kieleweke, support yenu ni muhimu sana kufanikisha hili. ni habari kubwa ipo Znz sasa, japo vyombo vya habari havitaki kuzitoa, kwa kukusaidia kidogo, tembelea "mzalendo.net" utapata mwanga wa jambo hili

Mkuu nimekusoma! Mie naamini wanasiasa ndio wanaotuzingua kwa interest zao. Wanasiasa wengi wa Zbr si wakweli! Wakiwa bara kwenye nafasi zao wanautetea muungano, wakija huko wanasema hawautaki! Wanafiki ni wengi wanaogopa kujulikana hadharanikama hawautaki muungano, ukweli ni kwamba hawautaki. Na ikitokea ikafanyika kura ya maoni kama muungano uvunjwe au la, nakuapia zaidi ya 80% watasema hawautaki muungano. Wanasiasa ni wanafiki sana, tuuvunje tu kila nchi iwe huru kujifanyia mambo yake kuliko kuwa na muungano feki kama huu!
 
Dawa ya Muungano ni kuuvunja tu. Baada ya kuuvunja, kila upande atafanya mambo yake akiwa bila kuogopa upande mwingine. Waunguja na Wapemba walioko Tanganyika watarudi kwao visiwani, na wale Watanganyika walioko Pemba au Unguja pia watarudi kwao Tangayika. Ingawa visiwa hivi vilikuwa ni sehemu ya Tangayika miaka yote tangu utawala wa Seyyid Said bin Sultan aliyekuwa na makao yake huko Zanzibar, huku Tangayika ikiwa ni sehemu yake ya kuvuna pembe na watumwa, visiwa hivyo vilikuja tenganishwa na Tanganyika wakati wa utawala kijerumani ambao uliviacha visiwa hivyo vizhukuliwa na Uingereza kusudi wao wajerumani wapate visiwa vya Heligoland. Chini ya Makubaliano yale, maji yote yanyovizunguka pamoja na visiwa vya mafia vilibaki sehemu ya Tanganyika, ndiyo maana mwanazoni waingereza waliona ni afadhali wamwache Sultan aendelee kuvitawala kwa vile ilikuwa ni vigumu kuvilinda iwapo maji yanayovizunguka ni mali ya nchi nyingine. Kwa hiyo tukishavunja Muungano, basi maji yote yale yatakuwa ni mali ya Tangayika isipokuwa ukanda mwembamba sana unaounganisha Unguja na Pemba; kwa maana nyingine, itakuwa ni marufuku kwa Wazenj kutumia maji yale ama kwa kuvua samaki au kwa kuchimba mafuta, itabidi wajibane kwenye ule ukanda unaounganisha Zanzibar na Pemba tu.
 
Najua unataka kuwaudhi wazanzibari, hii sio suluhisho, tunahitaji serikali tatu. Hivi mafia ina mjumbe baraza la wawakilishi. Ni Tanzania bara ua visiwani?

Hivi umeshawahi kujiuliza serikali ya tatu itakuwa na kazi gani? Nani atakuwa amiri mkuu wa JWTZ? Ni rais wa Muungano au rais wa Tanganyika? Na jeshi linatoka wapi? Zanzibar au Tanganyika? Na nani atagharimia matumizi ya serikali ya tatu? Ni Zanzibar au Tanganyika? Tafakari.
 
Back
Top Bottom