Muungano uwe wa nchi moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano uwe wa nchi moja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzalendo Mkuu, May 6, 2012.

 1. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ndugu Watanzania wenzangu. Jambo lisipingika kuwa hoja ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imo mawazoni mwetu karibu kila siku. Mara Watanganyika wanalalamika na mara nyingi sana Wazanzibari wanalalamika zaidi. Wote hawa wanalalamika kwa kuwa kuna nchi mbili na kila moja anaona mwenzake anapata zaidi.

  SULUHU YA MATATIZO YA MUUNGANO ni kuwa na NCHI MOJA TU badala ya nchi mbili kama ilivyo sasa. Kwa kuwa na nchi mbili tumesababisha yafuatayo:
  1. Malalamiko yasiyoisha
  2. Mgogoro wa CCM na CUF uliodumu kwa miaka zaidi ya 10 hivyo kuzorotesha maendeleo,
  3. Kuwepo kwa Serikali mbili ya Muungano (ambayo ndani yake pia ziko mbili(Muungano na Tanganyika)) na ya Zanzibar
  4. Uwepo wa viongozi wengi. Tunalazimika kuwa na Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu bila sababu hivyo kuongeza gharama kubwa kwenye serikali.
  5. Nchi moja kulazimika kuendesha mabunge mawili yaani lile la Muungano na lile Baraza la Wawakilishi.
  6. Halama za kamati mbalimbali za pamoja za serikali na za vyama mbalimbali.

  Kwa ujumla gharama ni kubwa sana zitokanazo na huu mfumo kuliko faida yake. Wakati tunaangali mchakato wa katibu mpya naomba pia tupate nafasi ya kuuangalia hili suala.
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Wanzanzibar wana mentality kuwa zanzibar ikjitenga inaweza kuwa kama Dubai,Qatar,Oman hivyo wao neno muungano kwao nikama unawawekea kijinga chamoto kwenye kidonda!
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Siyo nchi moja ni selikari moja..
   
 4. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  Eneo la Unguja na Pemba kama ilivyo Mafia kijiografia ni sehemu ya ardhi ya iliyokua Tanganyika...
  Pili, asilimia zaidi ya 50 ya wakazi wa Pemba na Unguja asili yao ni kutoka kwa mikoa ya iliyokua Tanganyika, tofauti ya tamaduni imetokana na tawala za kikoloni zilizokuwepo visiwani na bara.
  Hivi ushawahi jiuliza kabla ya uvamizi wa Waarabu ni kina nani walikua wakiishi katika visiwa vya Pemba na Unguja?
   
 5. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Uko sahihi bro. Hata hivyo Ukiwa na nchi moja ndiyo ndiyo utakuwa na serikali moja. Tatizo ni kuwa mpaka sasa nchi hizo bado ziko mbili!

   
 6. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nilishawai kusema hapa, miungano uliyodumu duniani na kufanikiwa ni Ile ya serikali moja tu. Tusijidangaya na maswala ya serikali mbili, tatu, nk. Zaidi ya serikali moja ni kuendeleza umimi ambayo matokeo yake ni manung'uniko yasiyokwisha. Pia gharama za uendeshaji wa nchi zitakuwa kubwa.

  Hata tukiweka serikali tatu haya mambo ya manung'uniko ndiyo yatazidi kuongezeka maana kila serikali itataka ijione yenyewe ndiyo zaidi ya mwingine kwa wale inaowatumikia. Marekani ni Muungano wa nchi zaidi ya 40, wana serikali moja ya kitaifa. Umoja na maendeleo yao ni matokeo ya serikali moja. Iweje sisi tuwe na maserikali utitiri?
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Najua unataka kuwaudhi wazanzibari, hii sio suluhisho, tunahitaji serikali tatu. Hivi mafia ina mjumbe baraza la wawakilishi. Ni Tanzania bara ua visiwani?
   
 8. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 60
  Kwa kweli watananzia tunasahau sana baba wa taifa mwalimu Nyerere alisema nini. Muungano wa serikali mbili kuelekea moja jamani haya mengine yote ni tamaa tu na udini.
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mwalimu alisema hivyo sawa, watanganyika walisema nini? Wazanzibari walisema nini? Kwani hii ni nchi ya mtu fulani?
   
 10. l

  lum JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mawazo hayapigwi rungu

  serekali moja haiwezekani kwa sababu katiba ya zanzibar inasema ZANZIBAR NI NCHI NA MIPAKA YAKE kwa mujibu wa katiba ya znz sheria yoyote itakayohitilafiana na katiba hii sheria hiyo itakuwa batili na katiba hii ndio itakayokuwa NA nguvu za kisheria ndio vipengele hivi vimefungwa haviwezi kurekebishwa na baraza la wawakilishi mpaka kwa kura ya maoni (password) ya wazanzibar wakubali.pamoja na mambo mengine ndio SABABU katiba ya muungano kuandikwa upya kwa kuwa inasema tanzania ni nchi moja haina pa kutokea hapo
   
 11. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mzalendo God Bless You kwa topic hii. ILA CAPITAL CITY IHAMIE DARESSALAAM tuepuke gharama na umalaya wa waheshimiwa Dodoma. (Dodoma yaweza baki mji wa ma Universities na kilimo)
   
 12. A

  Albimany JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kwaupande wa > Zanzibaar wazo hilo ni haramu hata kulifikiria. Wazanzibari kwa sasa hawafikirii tena serekali ngapi ziwepo katika muungano! wanachofikiria ni vipi watauvunja muungano!.

  Kama alivyoelezea mchangiaji mmoja hapo juu kua "kura ya maoni ndio kod ya wazanzibari kwa sasa kwajambo lolote zito kama hilo. na ninavyoamini ni kua zaidi ya asilimia 80 hawautaki muungano na kama watalazimishwa kuungana basi ni Muungano wa mkataba kama wa nchi za Ulaya au EAC.
   
 13. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Capital city dunia nzima huambatana na Ikulu. Sisi ni wa kwanza Duniani ambao mji mkuu na Ikulu viko sehemu tofauti
   
 14. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ni mwanya wa kuvuja pesa za wananchi wetu, wewe fikiria gharama ya kusafirisha na kuilisha serikali nzima mara zote kwenye vikao Dodoma. asilimia ngapi ya viongozi na ma MP wanaishi Dar?
   
 15. k

  karafuu Member

  #15
  May 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Paka hakamatwi sharubu bwana kiufupi hatutaki tena muungano haukuletwa na mungu,muungano huu unatambulika makaburini huko!
   
 16. k

  kicha JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 180
  kua huru kimawazo usiogope, kwa iyo ndo unataka kusema nini hasa, bcs kila mtu anajua nchi ziligawanya kwa misingi gani, nahofia kesho utasema kenya na uganda ni eneo la pembezoni mwa tanganyika sasando iweje.
   
 17. k

  kicha JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 180
  nadhani ayo ni mawazo yao tu ambapo kila mtu ana haki ya kuwaza, umesahau mbowe alipokua na sera ya kuigawa tanzania na kua kama USA?
   
 18. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ndio hicho...wanafikiri kua sheikh akija kutoka dubai akanunua kile kisiwa basi wataenda kujenga mahoteli, ma shoppin mallz kama vile dubai....hiyo ndio ndoto yao...wameshatawaliwa na waarabu once...wanataka itokee tena mara mbili??
   
 19. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Safari bado ni ndefu lakini kwa kila hali Muungano ni sehemu moja ya matatizo yetu.
   
 20. M

  Mzenji73 JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  " hujui kama karibu gulf coutries zote zimejengwa/kuendelezwa na waZanzibari, baada ya mapinduzi wengi wao walipokimbilia sehemu hizo? ikiwa tumeweza kuzi transform nchi hizo kwa nini tusiweze kwetu? serikali moja hata hao madalali CCM Znz hawalitaki hili, sisi sasa tumo kupanga kupangua kuuvunja kabisa huu Muungano. HATUUTAKI kabisa!!"
   
Loading...