Muungano lazima ujadiliwe kwa Ukweli na Uwazi! - Jaji Mark Bomani

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,529
113,661
Kwa wale wenye access na Channel Ten, watch kipindi cha Hamza Kassongo Hour, Jaji Mark Bomani, anazungumzia mambo mbalimbali kuhusu nchi yetu.

Amezungumzia suala la muungano lazima lijadiliwe kwa ukweli na uwazi ili kwenye katiba mpya zile kero za muungano zipate ufumbuzi wa kikatiba.
Amesema ni kosa kutokuwepo hadidu za rejea kuhusu muungano huku kuna hoja za tunataka serikali ngapi?. Amesema huwezi kujadili kuhusu serikali ngapi kama hujatoa fursa ya kujadili ni muungano wa aina gani?Ameshazungumzia kuusupport Muungano wa Mkataba!.
Amekiri kuwa Tanzania sasa kama nchi, haina dira wala mwelekeo!. Lazima katiba itamke rasmi Tanzania tunafuata itikadi gani?. Yeye anasupport "Ujamaa na Kujitegemea", na kusisitiza hata Sweeden ni nchi inayofuata siasa ya Ujamaa!.

Miongoni mwa maoni yake ni mawaziri wasiwe wabunge!.

Endeleeni kumfuatilia.

Pasco.
 
Akizungumzia kwa nini wabunge wasiwe mawaziri ili kutimiza na "doctrine of separation of powers", wabunge ni wawakilishi wa umma wenye jukumu la kuisimamia serikali, haiwezekani mbunge huyo ambaye ni msimamizi kujisimamia!.
Mbunge ambaye ni waziri, anakosa muda wa kutosha kuwatumikia wananchi wake hivyo wasipokuwa mawaziri, watapata muda wa kutosha kuwatumikia wananchi!.
Wabunge ambao ni mawaziri, wanatumia uwaziri wao kuelekeza maendeleo kwenye majimbo yao ili kugangamalia majimbo ili waendelee kuchaguliwa.

My take.
Kwenye hili la wabunge kutokuwa mawaziri, kutapunguza sana kiwango cha rushwa kwenye kuutafuta ubunge, maana kuna baadhi ya watu wanautafuta ubunge ili kusaka ulaji kwenye uwaziri, na kiukweli watu hawa sio watumishi wa watu bali ni waganga njaa!, sasa wabunge wakiwa sio mawaziri, then ubunge utakuwa sio great deal kwa baadhi ya watu!. Tutapata wabunge watumishi wa watu genuine!.
Pasco.
 
Kwenye madaraka ya rais, Jaji Bomani anaunga mkono madaraka ya rais yapunguzwe!.
Miongoni mwa maeneo unayopendekeza rais apunguziwe madaraka ya appointment powers.
Amesema kwa sasa rais anauwezo wa kumteua mtu yoyote kushika madaraka yoyote bila vigezo vyovyote!.
Rais apunguziwe madaraka ya uteuzi, apewe vigezo vya kuteua na uteuzi wa wakuu wa vyombo vya dola, lazima uridhiwe na bunge!.

Pasco.
 
Jaji Bomani anataka rais akiboronga ashitakiwe, na akjaeleza katiba yetu inaruhusu rais kushitakiwa kwa makosa yoyote ya uvunjaji wa katiba. Ile kinga ya rais kutoshitakiwa inahusu tuu katika utekelezaji wa majukumu yake ya kirais kwa mujibu wa katiba, kwa makosa mengine yote, rais anapaswa ashitakiwe kama raia mwingine yoyote.

Amemalizia kwa kusisitiza, Watanzania tuitumie kikamilifu, fursa hii adimu ya kuchangia maoni ya kupata katiba mpya.

Kipindi kimemalizika.

Asanteni.

Pasco.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu sijakufahamu vizuri, hivi kasema na yeye anasupport muungano wa mkataba?
 
watu wanautafuta ubunge ili kusaka ulaji kwenye uwaziri
Sidhani.

Hakuna anaejua mshahara wa Waziri, ni siri za nchi, lakini mshahara wa Mbunge na marupurupu yake na maposho ya masafari na matume na mavikao tunayajua, mamilion, tena akikaa miaka mitano, kumi, kumi na tano anaondoka na mabilion!

Mtu kama Anna Makinda, ambae sio waziri, amekaa bungeni toka wakati najifunza kuimba A, E, I, O, U, HIZI NI HERUFU KUU, karne ya kumi na tisa, ametengeza bungeni mabilion. Mabilion!

Tena ukiwa Mbunge huna headache za uwaziri, unaweza ukakaa kimya bungeni miaka mitano, kama Zhakia Meghji. Alipokuwa Waziri wa Fedha stress kibao, mara sijui kaiba, mara kaletewa memo halina jina kutoka Usalama wa Taifa apitishe matrilioni ya ulinzi wa nchi, mara sijui bajeti imegomba, mpaka jimama wa watu akakonda, akachokaaaaaa! Kikwete kamuibua alikojifichia kampa maisha bungeni, sasa hivi anapeta, anatengeneza mamilioni na ma dili ya mabilion, anapewa diplomatic passport ya ubunge, akitaka anaweza, bila kusachiwa, kusafiri na Twiga, miharadati, ma cheki ya BOT, bila kusachiwa. Akitaka. Mambo sijui ya kujibu hoja za Tundu Lissu sijui Mbatia anataka mitaala wakati hata karatasi ya hati ya Muungano imepotea aaaah aaaaaaaaah! Ya nini? Stress za nini?

Hakuna dili linalolipa kwenye siasa Tanzania kama ubunge.
 
...., Jaji Mark Bomani, anazungumzia mambo mbalimbali kuhusu nchi yetu.

Amezungumzia suala la muungano lazima lijadiliwe kwa ukweli na uwazi ili kwenye katiba mpya zile kero za muungano zipate ufumbuzi wa kikatiba.
Amesema ni kosa kutokuwepo hadidu za rejea kuhusu muungano huku kuna hoja za tunataka serikali ngapi?. Amesema huwezi kujadili kuhusu serikali ngapi kama hujatoa fursa ya kujadili ni muungano wa aina gani?Ameshazungumzia kuusupport Muungano wa Mkataba!.
Amekiri kuwa Tanzania sasa kama nchi, haina dira wala mwelekeo!. Lazima katiba itamke rasmi Tanzania tunafuata itikadi gani?. Yeye anasupport "Ujamaa na Kujitegemea", na kusisitiza hata Sweeden ni nchi inayofuata siasa ya Ujamaa!.

Pasco.

Pasco

Jaji Mark Bomani ameuelezea/ameufafanua ni nini muungano wa mkataba?
Amesema ni kwa nini ana-usupport mfumo huo wa muungano?
Je ametaja faida na hasara ya mfumo huu wa muungano wa mkataba?
Je amesema anataka ziwepo serikali ngapi?
Je ametaka Nchi/jina Tanzania liendelee kutumika kama mfumo huo wa Muungano wa mkataba utakubaliwa na wengi?

Au amerusha maneno tu na kuyaacha yaelee hewani?

Sisi huku hatuna r/luninga.
 
Pasco

Jaji Mark Bomani ameuelezea/ameufafanua ni nini muungano wa mkataba?
Amesema ni kwa nini ana-usupport mfumo huo wa muungano?
Je ametaja faida na hasara ya mfumo huu wa muungano wa mkataba?
Je amesema anataka ziwepo serikali ngapi?
Je ametaka Nchi/jina Tanzania liendelee kutumika kama mfumo huo wa Muungano wa mkataba utakubaliwa na wengi?

Au amerusha maneno tu na kuyaacha yaelee hewani?

Sisi huku hatuna r/luninga.
Mkuu Nonda,
Jaji Mark Bomani kwanza amefafanua Muungano wa Mkataba ni nini, amesema ni muungano kati ya nchi na nchi ambapo zinakubaliana kuungana katika mambo kadhaa tuu, ambayo ndio ya muungano hivyo kila nchi kubakiwa na madaraka yake kamili kama nchi isipokuwa katika mambo yale tuu waliokubaliana!.

Amesema miungano ya mkataba ipo na kutolea mfano baadhi ya nchi za Ulaya ndani ya EU, kuna nchi zimekubali kutumia safaru ya Euro na kuna nchi zimeigomea ikiwemo Uingereza. Kwenye Visa ya Seagean, kuna nchi zimefungua mipaka yake kwa raia wote wa EU na kuna nchi zimefunga.

Amesema muungano wa mkataba, kila nchi inabaki ni nchi kamili ila yale mambo ya muungano ndio yanaendeshwa na kitengo maalum ambapo nchi zote zinagharimia uendeshaji kama EU.

Hakusema faida na hasara, hakusema Tanzania iwe na serikali ngapi wala hakuzungumzia jina la Tanzania, bali amesisitiza haki za watu wanaitwa minority na kusema katika muungano wetu wa watu milioni 44 na watu miliini moja, maoni ya Wazanzibari kuhusu muungano lazima yazingatiwe kwa makini kabisa maana wao ndio minority!.

My Take.
Kwa vile muungano wetu ni dhima ya Nyerere na Karume tuungane kuwa kitu kimoja (union), ukishaunganisha vitu viwili unatakiwa upate kitu kimoja na sio viwili tena, hivyo matatizo yote ya muungano, yatamalizika rasmi kwa kuwa nchi moja yenye serikali moja, na Zanzibar itakuwa ni mkoa mmoja wenye wilaya mbili za Zanzibar na Pemba na ili kuwazuia Wanzanzibari wasilalamike kuwa wanamezwa, tunahakikisha rais wa muungano siku zote atoke Zanzibar, ila pia tunabadili mfumo kutoka presidential kwenda perliamentary, ili rais abaki ni ceremonial tuu!.
Pasco.
 
My Take.
Kwa vile muungano wetu ni dhima ya Nyerere na Karume tuungane kuwa kitu kimoja (union), ukishaunganisha vitu viwili unatakiwa upate kitu kimoja na sio viwili tena, hivyo matatizo yote ya muungano, yatamalizika rasmi kwa kuwa nchi moja yenye serikali moja, na Zanzibar itakuwa ni mkoa mmoja wenye wilaya mbili za Zanzibar na Pemba na ili kuwazuia Wanzanzibari wasilalamike kuwa wanamezwa, tunahakikisha rais wa muungano siku zote atoke Zanzibar, ila pia tunabadili mfumo kutoka presidential kwenda perliamentary, ili rais abaki ni ceremonial tuu!.
Pasco.

Mkuu Pasco.

Sipingani na pendekezo lako la kuungana na kuwa kitu kimoja.Kitu ambacho naona mahesabu ya kuwa kitu kimoja kuwa ndio ilikuwa dhima ya Nyerere na Karume ni kuongeza chumvi.

Je Nyerere na Karume waliunganisha nchi kuwa moja? Kama jawabu ni ndio.
Kwa nini Nyerere na Karume walikubaliana kuunganisha mambo 11 tu ambayo yalipewa jina la "mambo ya muungano"?

Je kwa nini kwa miaka 48 zimekuwepo serikali 2 na mamlaka 3 za kisheria?
Ufafanuzi:mamlaka za kisheria( mambo ya muungano, mambo ya Tanganyika(bara/Tz bara) yasiyo ya muungano na mabo ya Zanzibar yasiyo ya muungano).

Mkuu Pasco
Katika karne ya 21, kuna nchi ambayo inakubali kugeuzwa mkoa au kujigeuza mkoa?
Sudan imezaa nchi mbili, Indonesia imeachia East Temor ipumue kwa msaada ya Jaji Chande(jaji mkuu wa Tz)
Scotland ndio imeshakubaliana na UK gvt kuitisha kura ya maoni ya uhuru wa Scotland.
Kosovo imezaliwa.

Pia sio lazima kuwa unapounganisha vitu viwili ni lazima upate kitu kimoja.
mfano:Baba na mama wanapoungana basi familia huongezeka na sio kupungua na anapozaliwa mtoto, idadi inakuwa ni tatu na sio mbili wala moja. Kitu cha ajabu ni kuwa hawa wawili na mwanzo hujawa na furaha kwa idadi kuongezeka.:becky:

Pia huo mfano alioutoa Jaji Bomani wa EU, nilipotizama nimeona kitu union lakini sio nchi moja. Au kithungu kinanipiga chenga?

Usirudi kusema wao wanashirikiana lakini hawakuungana. Hilo ndio linalojionesha katika mambo 11 ya muungano, kushirikiana.

Mtoto wa mkulima nafikiri anajutia kauli ya "Zanzibar si nchi".

Mkuu Pasco, hivi kwa nini sisi wadanganyika tumekazania kuwa ni lazima wazanzibari wakubali serikali moja kama njia ya kumaliza kero za muungano?

Kwa nini tunataka Zanzibar iwe mkoa?
Tunayo Mafia ambayo imepiga hatua kubwa za kimaendeleo,uchumi unapaa as per CCM slogan. Hivi tutaweza kuishawishi Zanzibar ijione katika miaka miwili baadae baada ya kukubali kuwa mkoa iishie kuwa kama Mafia?

Hivi hakuna nchi ndogo ndogo duniani? Sao Tome, Cape Verde, Mauritius, Seychelles, Fiji, Comoro, nk.

Mimi naamini njia ya kutatua matatizo ya muungano ni kuumaliza muungano wenyewe. Kama hilo linatupa shida basi niungane na Jaji Bomani kusema leta Tanzania union ya mfumo wa EU.
 
Haya ndo mawazo ya kisomi na ya kutokuwa na unafiki, siyo mawazo kama yaliyotolewa na Mh. Malecela na Katibu Mkuu Kiongozi - Sefue, na ukiweka ya Mh, Mamvi, ya Katiba ieleze Rushwa ni nini, inashangaza sana!
 
Kasema ili kuondoa malalamiko juu ya Muungano ,ipitishwe kwanza kura ya maoni kama wazanzibari wanautaka Muungano au la? la pili wakiwa wanautaka je serikali ngapi wanataka hivyo hivyo na Watanganyika....My takae hii katiba inaweza isifanikiwe kwa jinsi tunavyo ona ubabe,vitisho na kulanzimisha mambo ....referenced to Bunge right now how is behaving is quite out of truck..we need to reconsider kweli ndo hawa watajadili rasimu ya katiba kweli?????
 
[h=2]ni heading isomeke hivi please "DK 45 "Judge Bomani anane NENO Juu ya Katiba Mpya"[/h]
 
Muungano wa Karume na Nyerere ndio tumeusikia juzi walihasimiana mpaka kuzungumza wakawa hawasemi, kuna kila aina ya sababu ya kusema haukuwa na ukweli au udhati baina yao, pengine ulijengwa kwa personal interests za viongozi hao. Tuunde muungano utakaoridhiwa na wananchi wenyewe, sio kuendeleza legacy ya watu ambao inawezekana walikuwa na nia njema lakini wananchi wenyewe sioni kama walishikishwa kwa kinna.

nakuunga mkono katika suala la president na vice president kuwa na nafasi ya ceremonial tu, pia ni wishful thinking kuona tunakuwa nchi moja, lakini naona ikiwa wazanzibari watakubali nchi moja basi hakuna haja ttena ya kuwawekea mipaka ya mikoa na wilaya kwa sababu za kuepusha khofu ya kumezwa, kwani kama ni nchi moja na visiwani zikawa mkoa mpya ndani ya tanzania kama sio kumezwa sijui tutaitaje. lakini turudi kwenye mada, hivi unafikiri kutakuwa na demokratic legitimacy ya wazanzibari milioni moja kuwa kikatiba awe ndio rais wa muungano hata ikiwa rais mwenyewe atakuwa butu asie na madaraka yoyote. Hivi huu muungano ni adhimu sana kiasi kwamba tuko tayari kuwa na katibba ya autocratics inayoshurtisha rais kutokea katika minority wa milioni moja? Katika nchi zilizotokea fujo kubwa na kuuana moja ya sababu kubwa ni minority kushika nafasi kubwa katika uongozi, sioni kama nasi tutakuwa katika right path ya aina hiyo.

Lakini juu ya yote nikupongeze kwa kuwa muwazi na mkweli hususan katika muono wako wa serikali moja, mimi ni muumini wa mkataba, lakini mwishowe wananchi ndio wawe waamuzi wa mwisho, ikiwa moja, mbili, tatu au vyovyote tunahope serikali itakuwa makini kusikiliza matakwa ya wadau ambao ni wananchi.
 
Kuna mtu anafikiri wazbr wa sasa ni sawa na wa miaka ya 64 anajidanganya,kwa mawazo yake anataka tuizike zbr kama ilivyozikwa tanganyika,never,jamhuri ya watu wa zbr 4rever never die.
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Back
Top Bottom