Muungano kambi ya upinzani mashakani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungano kambi ya upinzani mashakani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 26, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Muungano kambi ya upinzani mashakani


  *Mbowe awataka kina Hamadi Rashidi 'wazidi kusubiri'

  Na Tumaini Makene


  ZIKIWA zimebaki takribani wiki mbili kabla bunge la 10 halijaanza vikao vyake vya mkutano wa pili, hatma ya

  vyama vyote vya upinzani kuwa na kambi moja rasmi bungeni, bado ni kizungumkuti, ikiwa vitaweza kuungana hivi karibuni kabla ya mkutano wa bunge ujao au hata baadaye.

  Hayo yamefahamika ikiwa ni siku chache baada ya kamati ya wabunge wachache wa upinzani wasiokuwa katika kambi rasmi ya upinzani, kudai inasubiri majibu ya barua waliyomwandikia Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe, wakiulizia uwezekano wa kuwa kitu kimoja kabla mkutano wa bunge haujaanza, Februari 8, mwaka huu.


  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya wabunge hao wachache, Bw. Hamad Rashi Mohamed, 'kambi' yao inajumuisha Chama Cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi, United Democtratic Party (UDP) na Tanzania Labour Party (TLP).


  Kwa sasa kambi rasmi ya upinzani bungeni inaundwa na Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kutimiza masharti kama inavyoelekezwa katika Kanuni namba 14 (3) ya Kanuni za Bunge za mwaka 2007, inayosema kuwa ili chama cha upinzani kiweze kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni, lazima kiwe na asilimia 12 ya wabunge wote.


  Akizungumza na Majira jana juu ya hatma ya barua aliyoandikiwa, Bw. Mbowe alisema kuwa wabunge hao wanapaswa kuendelea kusubiri, kwani pande hizo zitaweza kuwasiliana kwa njia zilizo rasmi, si kupitia vyombo vya habari.


  Alisema kuwa kwa sababu wabunge hao walimwandikia barua mkuu wa kambi rasmi bungeni kuulizia uwezekano wa vyama vyote kujumuishwa katika kambi hiyo, hawana haja ya kukimbilia kwenye vyombo ya habari, ilihali hawajui iwapo CHADEMA kimeshalijadili suala hilo katika vikao vyake au la.


  "Kwa sasa siwezi kusema chochote kwa sababu suala hili si la Mbowe peke yake, suala hili lina process (taratibu) zake, wenzetu wasubiri majibu, sisi tutawasiliana nao kwa njia rasmi kama wao walivyotuandikia barua...hatuwezi kufanya maamuzi ya kisiasa kwa kupitia vyombo vya habari...la sivyo watu wanaweza kuwa wanatafuta cheap popularity.


  "Hakukuwa na haja ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari, kama walinikosa mimi wangeweza kuwasiliana hata na naibu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni...lakini CHADEMA bado hakijafanya maamuzi, wala si rahisi kufanya maamuzi haraka haraka tu kwa sababu watu fulani au vyama fulani wanataka.


  "Wakati mwingine si sahihi wala si vizuri kufanya maamuzi kwa pressure (shinikizo)...suala hili siwezi kusema no (hapana) wala yes (ndiyo) lakini halihitaji haraka namna hiyo," alisema Bw. Mbowe.


  Mwishoni mwa juma lililopita, wakati wakizungumza katika mkutano wao na waandishi wa habari, kupitia kwa viongozi wao, mwenyekiti wao Bw. Hamad (Wawi-CUF) na katibu wa kamati hiyo Bw. David Kafulila (Kigoma Kusini-NCCR Mageuzi), walisema kuwa hatma ya wao kuwemo katika kambi rasmi ya upinzani inategemea majibu kutoka CHADEMA.


  "Tumemwandikia barua mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe...mnakumbuka kuwa katika mdahalo wangu na yeye, yaani mdahalo kati ya mkuu wa kambi rasmi ya upinzani katika bunge la 9 na mkuu wa kambi wa sasa katika bunge la 10, Mbowe alisema kuwa suala hilo linahitaji mchakato wa vikao vya chama, hawezi kuamua mwenyewe.


  "Tunaamini kuwa tangu wakati wa mdahalo huo, ambao uliandaliwa makusudi kwa nia ya kujadili mstakabali wa upinzani bungeni kwa lengo la kuwa na kambi moja inayojumuisha vyama vyote kama ilivyokuwa katika bunge la 9 lililoisha, CHADEMA watakuwa wameshakaa vikao na kuamua juu ya suala hili.


  "Hivyo tumemwandikia barua mkuu wa kambi rasmi ili tujue tunakwenda vipi katika bunge linalotarajiwa kuanza hivi karibuni...tujue kama tunakwenda tukiwa wamoja au tutakwenda kama tulivyo sasa," alisema Bw. Hamad.


  Hata hivyo, jana Majira lilipata habari kutoka kwa mmoja wa wabunge wa upinzani, ambaye hakutaka kutajwa jina lake, lakini akionesha dhahiri kuwa suala la vyama vyote vya upinzani kuunda kambi moja rasmi bungeni, bado ni ndoto ya alinacha.


  "Unajua watu hawataki tu kusema au kuweka wazi mambo mengine, hii ndoa yetu ya wapinzani wote kuwa pamoja ni suala gumu na tata kwa kweli. Upende usipende ushirikiano wa CUF na CCM katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar ni moja ya vikwazo hapa, ni ngumu mno.


  "CUF wanapaswa kukubali kuwa faida waliyoipata kukubali kushirikiana na CCM huko Zanzibar ndiyo gharama ya wao kukosa uhalali wa kuonekana kuwa ni wapinzani wa kuaminika huku bara...kwa mfano hivi anapewa....(anataja jina la mmoja wa wabunge wa CUF) uwaziri kivuli wa mambo ya ndani, hivi atakuwa mtiifu kwa nani, kwa Mbowe au kwa Makamu wa Rais wa Kwanza, ambaye pia ni katibu mkuu wake.


  "Achilia huo mfano, chukua mfano mwingine...hivi kwa mfano tunaingia sasa katika umoja, halafu mmoja wetu anawasilisha hoja binafsi inayogusa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, mfano suala la mabadiliko ya katiba huko yalivyovuruga katiba ya muungano, hivi wabunge wa CUF watasimamia wapi," alisema mbunge huyo.


  Alienda mbali na kutoa madai kuwa CUF kinaviburuza vyama vingine katika kile kinachoitwa kamati ya wabunge wachache wasiokuwa katika kambi rasmi, "wanaburuzwa tu kama msukule akina...(anataja jina la mbunge mwenzake wa upinzani kutoka NCCR-Mageuzi), lakini hamna kitu pale, hata UDP na TLP hawamo mle, basi tu," aliongeza mbunge huyo.


  Lakini pia tumaini la kamati hiyo ya wabunge wa CUF, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP, kuwa na kambi ndogo ya upinzani, limeonekana kutoweka baada ya Spika wa Bunge, Bi. Anna Makinda kunukuliwa na vyombo ya habari akisema kuwa kwa mujibu wa kanuni za sasa za bunge, haiwezekani kuwa na kambi tatu bungeni.


  Alisema kuwa CHADEMA walikuwa na sifa zote za kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni kwa kuwa wana asilimia 12.5 ya wabunge wote, tofauti na vyama vingine vya upinzani, hivyo akavishauri vyama hivyo kuangalia uwezekano wa kuungana na CHADEMA.


  Mabadiliko ya kanuni yalikuwa ni njia mojawapo ya kutaka kupata nafasi ya kutambulika, iwapo ile ya kuwaomba CHADEMA itashindikana "kwa kweli wakati tukibadilisha kanuni wakati ule tulijisahau kuangalia hili...si vizuri kabisa kukiacha nje ya kambi rasmi ya upinzani chama kingine cha upinzani chenye wabunge pia," alisema Bw. Hamad, huku akiungwa mkono na Bw. Kafulila katika mkutano wa mwishoni mwa juma.


  Semina elekezi


  Wakati huo huo, wabunge wa bunge la 10 wamekumbushwa kuwa wanao wajibu wa msingi katika maeneo manne, ambayo ni; katika majimbo yao ya uchaguzi, kwa nchi, kwa vyama vyao na kisha kwa dhamira zao wenyewe.


  Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais Dkt. Ghalib Bilal wakati akifungua semina elekezi kwa wabunge wote jana Dar es Salaam, akiongeza kwa kutoa wito kuwa wanapaswa kuwa karibu na wananchi waliowachagua ili kwa pamoja waweze kutafuta majawabu ya kero mbalimbali zinazowakabili.


  "Kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatekeleza mojawapo ya kazi yenu muhimu-uwakilishi wa wananchi. Miaka mitano kuanzia sasa si mingi," alisema Dkt. Bilal.


  Spika na hoja binafsi za wabunge


  Naye Spika wa Bunge, Bi. Anna Makinda jana alisema kuwa hatakuwa na tatizo kwa hoja binafsi yoyote itakayowasilishwa ofisini kwake almuradi iwe imekidhi vigezo vya kikanuni kuiwezesha kujadiliwa bungeni, baada ya kuangaliwa na wataalamu.


  Alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) juu ya mgawo wa umeme na sakata la kampuni tata ya Dowans, ambapo alisema mpaka sasa mbunge huyo bado hajawasilisha hoja yake hiyo mbali na kuwa tayari ameshawasilisha barua ya kusudio la kuwasilisha hoja.


  "Ni muhimu mkaelewa mpaka sasa alichowasilisha (Kafulila) ni barua ya kusudio la kuleta hoja binafsi, si hoja binafsi...hivyo ni vitu viwili tofauti kabisa...lakini sina tatizo na hoja yake au ya mbunge mwingine yeyote, kinachotakiwa ikidhi kanuni za bunge tu...akileta tutakaa na wataalamu tutaifanyia kazi, ikiwa haina tatizo tutamwambia ajiandae kuiwasilisha," alisema Bi. Makinda.


  Habari zilizopatikana jana jioni katika eneo la semina elekezi ya wabunge na kuthibitishwa na Bw. Kafulila, zilisema kuwa ofisi ya bunge imejibu barua ya mbunge huyo, ikimtaka awasilishe hoja yake ofisi za bunge, tayari kwa kufanyiwa kazi.


  "Ndiyo nimepata barua hiyo, lakini ni ya siri, siwezi kukuonesha...lakini jibu la lini nitawasilisha hoja yangu ofisi ya spika siwezi kulisema sasa, labda kesho nitakuwa katika nafasi nzuri ya kusema," alisema Bw. Kafulila.

  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Tatizo la CUF ni kudhani ya kuwa il wawe kwenye kambi ya upinzani ni lazima wapewe vyeo kama kwenye ile serikali ya mseto na CCM...kule Zanzibar.............lakini ukweli una baki pale pale ya kuwa upinzani ni itikadi tu na wala siyo vyeo..................................Hili watajifunza lini?
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,920
  Likes Received: 12,112
  Trophy Points: 280
  Jibu zuri sana 'keep on waiting' au kwa lugha ya kigeni unawekwa kwenye waiting list, kwa tafsiri yangu kama wana haraka sana wanaweza kujaribu sehemu nyingine, Ha ha haaaaaa my poor Hamad.
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  CUF waache kutaka vyote... in simple logic CUF si Wapinzani bali ni serikali!
   
 5. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,071
  Likes Received: 4,008
  Trophy Points: 280
  sasa mkuu hapo mbona kama una-support CUF kuwamo madarakani huko Zanzibar? hebu soma hiyo sentensi yako vizuri...
   
 6. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ile Siku ya Mdahala ya vyama vya upinzania uliorushwa moja kwa moja na ITV, hapo ndipo Bwana Hamadi alinishangaza! Yeye alikurupuka tu mwishoni wakati Mbowe anahitimisha na kuanza kusema, waambie wananchi wajue kwamba ukiwa kiongozi wa upinzani bungeni unapewa fungu milioni 7! Duu kumbe nikajua kumbe wanalipwa? Sasa kwa kipindi chote kile mbona hakusema kama alikua analipwa? na sasa anataka tena kuwa kiongozi ili aendelee kupata hizo pesa! Kumbe yeye hana upinzani wa kweli anakimbilia pesa tu! Kwani yeye kazaliwa kuwa kiongozi tu! Yan huyu angepewa nnji hii ndo wale wale kina Gabo na Mugabe!
   
 7. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwani wao si wanajijua ni wapinzani? sasa wanataka nini tena wawe wapinzani kwa kuchangia hoja ki-upinzani na siyo lazima wapewe vyeo, ila baadhu ya kamati bora wapewe udp na nccr kuliko cuf na mrema(tlp)
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nadhani suala linalowatoa udenda cuf na nccr ni ile bajeti ya kambi ya upinzani pamoja na vyeo vikiwemo vya usemaji kambi ya upinzani, uwaziri kivuli, uongozi katika kamati mbalimbali za bunge, n.k.

  Nilimsikia Kafulila wakati anahojiwa na TBC jana baada ya mkutano wa semina elekezi ya wabunge, alisema kuwa sababu hizo ndizo zinazoifanya chadema kukataa kuwashirikisha vyama vingine vya upinzani kwenye hiyo kambi.

  Mimi nabaki najiuliza: cuf na nccr tangu mwanzo walionekana kuwapinga CDM kwa kila kitu, likiwemo suala la kutomtambua rais na ndio maana wakati chadema wanatoka kwenye ukumbi wa bunge kususia hotuba ya mkwere vyama hivyo hivyo vilishirikiana na ccm kuwazomea chadema.

  Vilevile wakati wa mdahalo wa kambi ya upinzani bungeni uliooneshwa na kituo cha itv hamad rashid aliikashfu sana chadema, sasa inakuwaje leo wanajibembeleza kuungana na hao hao? Suala hapa ni mafao na wala sio maslahi ya nchi. Kaeni pembeni cuf na nccr kama mlivyoamua tangu awali.

  "Usitukane wakunga na uzazi ungalipo"
   
 9. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Naona wamwambie makinda aangalie utaratibu wa kuwa na kanuni mpya za kuwa na kambi ndogo au wabaki kama wawakilishi wa wananchi bungeni bila ya kupigania vyeo. Sio mpaka anaekosa pa kwenda analetwa kuungana na cdm. No,no!
   
 10. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CUF+NCCR MAGEUZI=CCM, Hao njaa zitawaua, mbona CDM hawakuwa na fujo bunge lililopita wakati wao wakiziramba hela za kambi ya upinzani kwa kwenda mbele, Kunya anye kuku akinya bata kaharisha.
   
 11. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,920
  Likes Received: 12,112
  Trophy Points: 280
  Kafulila kwa kusema hivyo anafikiri anatibu au anatibua zaidi, mimi najua haya mambo si ya kuongea kwenye vyombo vya habari anayakuza bila sababu za msingi wangemalizana kimya kimya, sisi wengine hatuhitaji kujua kama walituma barua au walipigiana simu.
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Maoni yangu binafsi, shillingi ina pande kwa mtazamo huo ni vizuri tukawa na vyama vikubwa viwili vya siasa ili kuharakisha maendeleo. Marekani wana Republican na Demacratic, uingereza wana Labour na..

  Hapa kwetu tuwe na CCM (cha wala nchi) na CHADEMA (walalahoi)
   
 13. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kwani kuwa upinzani mpaka uwe kambi rasmi? Upinzani ni hoja na sio kambi au vyeo. Anyway tutawajua tu kwa matunda yao wiki chache zijazo!
   
 14. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Cuf hawawezi tena kuwa wapinzani,tlp ndo kabisaaaaaa,udp nayo haiko mustand kivile na nccr itakuwa ndoa ya kinafki maana tayari mwenyekiti wake taifa ana kesi dhidi ya halima mdee.so cha msingi hapo ni kuwamwaga tu kama ifuatavyo.
   
 15. z

  zdaima New Member

  #15
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inashangaza kidogo. inaonekana wachangiaji karibu wote ni Chadema oriented hawataki kabisa kujikita katika hoja za msingi. kumbukeni ni hao hao chadema walikuwa ndani ya kambi ya upinzani iliyoongozwa na CUF mmesahau nafasi ya dr slaa kwenye kambi? leo hii. kuna nini hapa ? hoja ya kuwa cuf iko serikalini haina mashiko si wangetengeneza kanuni za maashirikiano na atakae kwenda kinyume akaondolewa "Automatic" chadema ni wabinafsi tu na hawawezi kukiri hiovyo hata kama ni wewe huwezi wasizuge.watanzania wanahitaji upinzani mmoja wenye mashirikiano kama ilivyokuwa bunge lililopita .
  Nyinyi wahafidhina wa chadema msiotaka kukosolewa twambieni kwa udhati wa nafsi zenu faida za chadema kuvitenga vyama vyengine kama si kuwagawa watanzania ni nini ? na iweje leo wanatumia hoja dhaifu kuvitenga vyama vyengine kwa sababu za minyukano tu kipindi cha uchaguzi jamani viongozi wa chadema pevukeni kisiasa mambo madogo yasiwagawe ni bora zaidi mambo yanayowagusa wananchi yakapata nguvu moja ya upinzani kuliko utengano .
  tabiri kwa nature ya siasa za tz si muda mrefu chadema itafitinishwa na hata katika kambi ya upinzani . bila ya kuwepo mtu mwengine kutoka chama chengine chenye nguvu watashindwa kusuluhihwa pale wanapotofautiana miongoni mwao
  .mitazamo tofauti ya kisiasa na maslahi ya leo tu hujui kesho isiwafanye viongozi wa chadema kuwa vipofu leo ni wao kesho ni wenzao .ndio nyie nyie mtakaokuja kulia hapa jamii forum aah nccr ,cuf tlp nk wanawatenga wenzao mnakumbuka cuf ilipotaka kufanya hivyo watu walipiga makelele mbona kleo kimya au kwa sababu ni chadema ? waandishi wa habari vipi? mpo? mambo shwari ule umoja sasa hivi si muhimu tena ? wakati utaahukumu .
   
 16. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo Z(anzibar)Daima unataka kuwa blackmail chadema kwa position za bunge lililopita?
   
 17. z

  zdaima New Member

  #17
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana Yeshuahamelech.nadhani umenifahamu sana tu .hapa hakuna blackmail wala judgement tupite kwenye point tu.Hapa chadema inakiuka misingi na dhana nzima ya upinzani bungeni na wanajenga utamaduni mpya mbaya na wao itakuwa ndio waanzilishi sioni faida na bora wakaacha misimamo hio ya kuadabishana.
  masahihisho. mimi ni Zdaima wala sio Z(anzibar) daima.asante.
   
 18. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,920
  Likes Received: 12,112
  Trophy Points: 280
  Mbona nyie huko zanzibar mmevitenga vyama vingine kwenye serikali ya umoja tuwaite wabinafsi, wepesi sana kuona nyuma ya nyani wakati nyote ni nyani wale wale.
   
 19. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sawa kabisa mkuu
   
 20. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  umetumwa wewe na aliyekutuma mwambie umewakosa.cuf zanzibar na umoja wao wa kitaifa wanavyowafanyia vyama vingine unaona kweli au unaongea tu ka chapombe?
   
Loading...