MUUNGANO: Ipigwe kura ya maoni Tanzania nzima. Ndoa za walokole zinavunjika sembuse ya mkeka?

Na ss pia tushachoka ukoloni wa Tanganyika vunja Muungano wa Dhulma mbalini!hakuna anayeogopa hapa ss tuko wazi hatufichifichi msimamo wetu!
ZANZIBAR KWANZA SHENGESHA BAADAE!!!!
SHENGESHA ndio nini,
Muungano uvunjike na wale kupe wanaoona damu ya ngombe sio tamu wakajinyonye damu yao wenyewe.
Zanzibar mko wachache kuliko hata wilaya ya bariadi halafu mnataka muwe na haki sana na watu milioni 45 hii ni sawa kweli?
 
SHENGESHA ndio nini,
Muungano uvunjike na wale kupe wanaoona damu ya ngombe sio tamu wakajinyonye damu yao wenyewe.
Zanzibar mko wachache kuliko hata wilaya ya bariadi halafu mnataka muwe na haki sana na watu milioni 45 hii ni sawa kweli?
Unajua hata ikiwa umesoma kiasi gani ukisimama kwenye dhulma unakuwa mjinga!!!
Hapa hakuna cha mdogo wala mkubwa hizi ni nchi mbili huru
pasu kwa pasu 50%/50% hamtaki kajiungeni na Congo!!
 
je ni faida zipi hizo inazozipata tanganyika kwa kuungana na hawa wazanzibar mbona viongozi wetu kwa upande huu wa tanganyika wanaung'ang'ania sana huu muungano japo sisi wananchi wengi wa tanganyika hatuutaki
 
ukiona hivyo ujue kuna mafungu ya unaudited balance! manaake kwa sisi wabongo ukikuta mwanya uko loose sco magoli mengi uwezavyo, i presume kuna kitu tuu, tutagundua baadae!
 
Samahaninsan badala ya kukupa faida nitakupa hasara. 1. Wazazibari wengi sana wamekuja huku bara kuchukua ardhi yetu. 2.Wazanzibari wanafanya kazi hata kwenye wizara ambazo siyo za muungano. 3. Wazanzibari wengi wamehamishia watoto wao kwenye shule za msingi huku kwetu wakati elimu ya msingi siyo suala la muungano. Ongeza nyingine.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Unajua hata ikiwa umesoma kiasi gani ukisimama kwenye dhulma unakuwa mjinga!!!
Hapa hakuna cha mdogo wala mkubwa hizi ni nchi mbili huru
pasu kwa pasu 50%/50% hamtaki kajiungeni na Congo!!
Wee mbona mgumu sana wa kuelewa?
Sisi hatuwataki ondokeni mkaunde nchi yenu sasa kelele za nini?
Mkitaka nkujitenga ni rahisi sana, mnawaambia wabunge wenu wasihudhurie vikao vyabunge na hapo ndio inakuwa mwisho wa stori yote
 
Maswahiba Eee Acheni dhanaa, Hapa kila upande una dhanaa mbaya kwa mwenzie...... Safisheni nia Heri ipo mbele. "Mkono wa Mungu upo na wale waloshikana pamoja"
 
Ni ujinga kuwa na mtaji wa 45milion kufanya biashara na mtu mwenye mtaji wa 1.5milion,watanganyika muwe na akili tafuteni kwengine kwenye mitaji mikubwa kama nyie mufanye nao biashara wazenji wamekuchokeni,ipo kenye,uganda kafanyeni nao biashara ya muungano.
 
Ni ujinga kuwa na mtaji wa 45milion kufanya biashara na mtu mwenye mtaji wa 1.5milion,watanganyika muwe na akili tafuteni kwengine kwenye mitaji mikubwa kama nyie mufanye nao biashara wazenji wamekuchokeni,ipo kenye,uganda kafanyeni nao biashara ya muungano.

Wakenya na waganda ni wajanja na wanaakili sio rahisi kuwapiga bao bro!
 
Uvunjike tu maana hata ndoa za kanisani mbona zinavunjika siku hizi cha ajabu nini? Hawa wala urojo wanatusaidia nini sisi? zaidi ya kuingiza ma used na kuleta mende toka ulaya? Puuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu:smash:
 
Wakenya na waganda ni wajanja na wanaakili sio rahisi kuwapiga bao bro!

Ujanja mwingi mbele giza(hasara),ona sasa hamjijui hadi leo kama nyie ni watanganyika au watanzania bara au azania au nyasaland au tanzania tanganyika au wadanganyika.
 
Mkuu wangu Chilisosi naunga mkono hoja by 100%, Maana mpaka hapa tulipofika tushachoka na matusi ya Jussa na Seif mara waseme Tanganyika ni mkoloni mweusi, Sasa huu ndo muda wa kufanya maamuzi magumu ikibidi.
Kuwepo muda wa campaign kabla ya referundum kwa pande zote za muungano kwa wanaopenda na kupinga muungano. Matokeo yaheshimiwe wananchi wajishughulishe na maendeleo badala ya porojo zisizokwisha za 'kero za muungano'
 
Mm kinachonishangaza ni Watanganyika kukosa Uzalendo wa Taifa lao!!!
Ss waZanzibar ni Wazalendo ndio mana tunadai mamlaka kamili ya Taifa letu ss kwa nini nyinyi waTanganyika hamdsi chenu!!?
Huku Zanzibar hasa kunanini?mpaka ikawa mnatung'ang'ania hivi!!?
Nyinyi kwanza hamna kitu ndio sasa tunasema nendeni zenu. Kwani wewe ulidhani tunawang'ang'ania? Umekosea mkuu, sisi badala yake tulidhani tunawasaidia ulinzi na kuwapa uraia wa nchi kubwa kumbe nyie mnaona tunawang'ang'ania sijui kwa kipi mlichonacho.
 
Idadi ya wa-Zanzibar walioko Tanganyika inakisiwa kuwa zaidi ya walioko Zanzibar. Pili, Muungano utakapovunjika wasidhani wataendelea kubaki Tanganyika kwa uhuru kama ilivyo sasa; watabanwa moja kwa moja na sheria za uraia na uhamiaji hivyo itabidi warudi kwao labda kwa wale watakaochagua uraia wa Tanganyika.

Nne, sheria muflisi ya "uraia wa nchi mbili" inayopigiwa upatu na Membe marufuku; itatuletea matatizo na hawa jamaa. Tano, endapo watavurugana huko kwao baada ya Muungano kuvunjika, watakaobahatika kuvuka bahari wasidhani wataelekea Kariakoo na Ilala kama ilivyo sasa! Wakionewa sana huruma ni moja kwa moja makambini huko Kongwa, Kiteto, au Nachingwea. Wanapaswa kulijua hilo kwa mapana na marefu yake.

Ha haaaa,mkuu yaani hizo sheria zimenichekesha!
Dah!na tunaitaka tanganyika
 
Back
Top Bottom