Muundo wa Serikali ya awamu ya tano

Muundo wa Serikali ya awamu ya tano

Atawalipaje fadhila wanaozunguka mikoani kumpigia kampeni zaidi 32?Magufuli kwa CCM ni sisimizi tu wala hakuna mabadiliko

Kwani Lawasa yeye huko mikoani anazunguka mwenyewe, hata chopa anaendesha mwenyewe?
 
Mbona wizara ya habari haipo? Au ndio iko kwenye mawasiliano? Muhimu sana hii .

Mimi napendekeza serikali ijayo iwe na wizara hadi 20 ili Kazi na Ajira, Utalii, Madini na Nishati, Ujenzi na Mawasiliano zisimame peke yake, na kuwe na manaibu waziri wasiozi 5 kwenye baraza lote.

Kutoka baraza la watu karibu 60 hadi 25 tutakuwa tumepiga hatua sana
 
Habari yenu Watanzania wenzangu,

Kila jambo na wakati wake kwa majira yake. Uchaguzi Mkuu unafanyika Oktoba, 2015 siku ya Jumapili. Si rahisi kubashiri nani ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha Urais pengine tusubiri kuona nini kitatokea.

Mara baada ya tarehe 25 Oktoba tutakuwa na mjadala mpana juu ya Muundo wa Serikali ambayo Rais Mpya ataiunda. Nina mawazo ambayo ningependa Rais ajaye ayaweke katika fikra zake na kuyafanyia kazi. Nayo ni haya yafuatayo;

1. Serikali iliyopo ni kubwa mno na ufanisi ni Mdogo; hivyo afikirie kupunguza ukubwa wa Serikali kwa kiwango kikubwa.

2. Muundo wa Utawala hauna tija

Ufafanuzi

1. Ukubwa wa Serikali
Kwa sasa kwa upande wa Tanzania Bara kuna Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wasaidizi wao. Kimsingi hawa wote kazi zao zinashabihiana. Hawa ni Wateule wa Rais na ni wawakilishi wa Taasisi ya Urais katika ngazi zao. Binafsi sioni kitu cha ziada na chenye manufaa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao kwa sehemu wanatumika kama Makada wa CCM. Ushauri wangu ni kuwa Cheo cha RC na DC kiondolewe tubaki na Watendaji ambao ni Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri. Tutaokoa fedha nyingi sana kwa hatua hii tu.

2. Muundo wa Utawala usio na tija
Tumekuwa na Wizara nyingi lakini ufanisi bado mdogo sana. Makusanyo ya kodi na wigo wa kodi bado ni mdogo, Tija katika sekta za uzalishaji bado ipo chini nk. Ushauri wangu ni kuwa na Wizara chache lakini zenye tija. Ninapendekeza Wizara zisizozidi 15 kama ifuatavyo;

1. Wizara ya Fedha, Uchumi na Uwekezaji,
2. Wizara ya Nishati na Madini,
3. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4. Wizara Maji, Ardhi na Maendeleo ya Makazi
5. Wizara ya Ulinzi na JKT
6. Wizara ya Afya, Usafi wa Mazingira na Ustawi wa Jamii
7. Wizara ya Mazingira, Maliasili na Utalii
8. Wizara ya Kilimo, Mifugo, Ushirika na Masoko
9. Wizara ya Viwanda na Biashara
10.Wizara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu
11.Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni
12. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
13. Wizara ya Elimu, Ufundi na Sayansi
14. Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
15. Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma

Hatuna sababu ya kuwa na Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI). Halmashauri ziwajibike moja kwa moja kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS). Kwa kufanya hivyo tutaokoa fedha nyingi sana na kuwa na utekelezaji wa haraka. Kwa hiyo Elimu bure kwa wote, Afya bure kwa wazee, watoto na wajawazito inawezekana kabisa.

Aidha, Rais akasimu Mamlaka yake ya uteuzi. Si busara kila uteuzi ufanywe chini ya Ofisi ya Rais. Hali hii imesababisha kujikweza na kuwa na kiburi kwa baadhi ya wateule. Mfano RC hawezi kumfanya chochote RAS kwa kuwa Mamlaka ya Uteuzi ni Rais; Wakuu wa Mashirika hawawezi kuwajibika moja kwa moja kwa Waziri husika badala yake hata wakivulunda inasubiliwa Mamlaka ya Uteuzi kutengua Uteuzi. Huu ni urasimu na ni kuchelewesha maendeleo.

Ninashauri Serikali ijayo izingatie haya. Sisi ni nchi changa lazima tuwe na namna bora zaidi ya kutumia raslimali zetu kwa matokeo makubwa.

Asanteni kwa michango yenu wana JF.
JF inakosa watu kama wewe siku za hivi karibuni. Nakuunga mkono kwa hoja nzuri.
 
Punjab; Wizara ya Michezo, Utamaduni na Sanaa (Of course nimeambiwa tuongeze na Habari) ni muhimu sana. Hii ndio yenye kutambulisha utaifa wetu. Taifa lisilokuwa na utamaduni wake na kuuenzi ni sawa na taifa MFU. Nadhani ipo haja ya kuendelea kuwa na Wizara hii.

No need to have no.11. Ministry of Sports Arts and Culture the activities can go to no. 14 or under an independent governing body financed by the government
 
Hata kama ataiba hatatuonesha kuliko hawa wakwetu...wanatuonesha halafu wanatubeza..wanatutukana....wanatuganya hatujasoma kabisa....Mfano hai na yale yaliyotokea kwenye hotel moja Morogoro...ni madola kwa madola kwa mwanamama na kutaka kuharibu jina la hotel.
 
Ninapenda niwashukuru kwa michango mizuri ambayo mmeendelea kuiweka katika Mada hii. Nimepitia michango yenu yote ambayo mingi inalenga kuboresha zaidi. Ninakubaliana kabisa kuhusu uwepo wa WIZARA YA MAMBO YA NJE. Nadhani hii sasa itafanya Wizara zifike 16. Hatuna sababu yeyote ya kuwa na utitiri za Wizara kwani tunaongeza gharama za uendeshaji wa serikali ilihali TIJA inabaki pale pale. Ama kuhusu uwepo wa Wakuu wa Mikoa, ninatambua wapo Kikatiba, swali ni je, Kutokuwepo kwao kutapunguza nini?
 
Mbona wizara ya habari haipo? Au ndio iko kwenye mawasiliano? Muhimu sana hii .

Mimi napendekeza serikali ijayo iwe na wizara hadi 20 ili Kazi na Ajira, Utalii, Madini na Nishati, Ujenzi na Mawasiliano zisimame peke yake, na kuwe na manaibu waziri wasiozi 5 kwenye baraza lote.

Kutoka baraza la watu karibu 60 hadi 25 tutakuwa tumepiga hatua sana

Hakuna haja ya kuwa na manaibu waziri kwenye nchi inayotegemea mjsaada ya wahisani kwenye bajeti.
 
Utamaduni ndio nguzo kuu ya maendeleo ya mataifa makubwa duniani.

Tanzania hatuna utamaduni wa kitaifa unaotutambulisha. Leo vijana wamekosa dira ya maisha kwa sababu ya muingiliano wa tamaduni mbalimbali za nje.

Ningependa tuwe na wiza ya utamaduni na michezo tu, ifanye mapinduzi makubwa ya kitamaduni kwa watoto wetu kuanzia wanapoanza kusoma chekechea hadi chuo kikuu.

Wasomi wetu walioko vyuoni wanakatisha tamaa, wapo wapo tu.
 
Mkuu Nimependa Maono Yako.

Nadhani Pale Kwenye Wizara Namba sita Pangekuwa WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII.

Then Usafi wa Mazingira ukawa ndani ya wizara namba saba.

Na Kwa Kuwa Umespecify Wizara ya Vijana, Basi Ni Vyema Kukawa na Wizara Inayospecify Watoto Pia. Makundi Haya Mawili Ukiongeza na Wanawake ni Muhimu Sana.

Ahsante.
 
Lowasa ataiweza hyo ila magufuli hawezi.wanaompigia debe kila mmoja kashachagua yake.
 
Kwani utumishi wa uma ni wito sio ajira!!! Nauliza tu....
 
Habari yenu Watanzania wenzangu,

Kila jambo na wakati wake kwa majira yake. Uchaguzi Mkuu unafanyika Oktoba, 2015 siku ya Jumapili. Si rahisi kubashiri nani ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha Urais pengine tusubiri kuona nini kitatokea.

Mara baada ya tarehe 25 Oktoba tutakuwa na mjadala mpana juu ya Muundo wa Serikali ambayo Rais Mpya ataiunda. Nina mawazo ambayo ningependa Rais ajaye ayaweke katika fikra zake na kuyafanyia kazi. Nayo ni haya yafuatayo;

1. Serikali iliyopo ni kubwa mno na ufanisi ni Mdogo; hivyo afikirie kupunguza ukubwa wa Serikali kwa kiwango kikubwa.

2. Muundo wa Utawala hauna tija

Ufafanuzi

1. Ukubwa wa Serikali
Kwa sasa kwa upande wa Tanzania Bara kuna Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wasaidizi wao. Kimsingi hawa wote kazi zao zinashabihiana. Hawa ni Wateule wa Rais na ni wawakilishi wa Taasisi ya Urais katika ngazi zao. Binafsi sioni kitu cha ziada na chenye manufaa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao kwa sehemu wanatumika kama Makada wa CCM. Ushauri wangu ni kuwa Cheo cha RC na DC kiondolewe tubaki na Watendaji ambao ni Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri. Tutaokoa fedha nyingi sana kwa hatua hii tu.

2. Muundo wa Utawala usio na tija
Tumekuwa na Wizara nyingi lakini ufanisi bado mdogo sana. Makusanyo ya kodi na wigo wa kodi bado ni mdogo, Tija katika sekta za uzalishaji bado ipo chini nk. Ushauri wangu ni kuwa na Wizara chache lakini zenye tija. Ninapendekeza Wizara zisizozidi 15 kama ifuatavyo;

1. Wizara ya Fedha, Uchumi na Uwekezaji,
2. Wizara ya Nishati na Madini,
3. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4. Wizara Maji, Ardhi na Maendeleo ya Makazi
5. Wizara ya Ulinzi na JKT
6. Wizara ya Afya, Usafi wa Mazingira na Ustawi wa Jamii
7. Wizara ya Mazingira, Maliasili na Utalii
8. Wizara ya Kilimo, Mifugo, Ushirika na Masoko
9. Wizara ya Viwanda na Biashara
10.Wizara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu
11.Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni
12. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
13. Wizara ya Elimu, Ufundi na Sayansi
14. Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
15. Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma

Hatuna sababu ya kuwa na Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI). Halmashauri ziwajibike moja kwa moja kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS). Kwa kufanya hivyo tutaokoa fedha nyingi sana na kuwa na utekelezaji wa haraka. Kwa hiyo Elimu bure kwa wote, Afya bure kwa wazee, watoto na wajawazito inawezekana kabisa.

Aidha, Rais akasimu Mamlaka yake ya uteuzi. Si busara kila uteuzi ufanywe chini ya Ofisi ya Rais. Hali hii imesababisha kujikweza na kuwa na kiburi kwa baadhi ya wateule. Mfano RC hawezi kumfanya chochote RAS kwa kuwa Mamlaka ya Uteuzi ni Rais; Wakuu wa Mashirika hawawezi kuwajibika moja kwa moja kwa Waziri husika badala yake hata wakivulunda inasubiliwa Mamlaka ya Uteuzi kutengua Uteuzi. Huu ni urasimu na ni kuchelewesha maendeleo.

Ninashauri Serikali ijayo izingatie haya. Sisi ni nchi changa lazima tuwe na namna bora zaidi ya kutumia raslimali zetu kwa matokeo makubwa.

Asanteni kwa michango yenu wana JF.

Asante kwa maoni ako mkuu!
 
Ukiongeza Mambo ya nje tu inakamilika hiyo provisional govt!
 
It makes sense. Bahati mbaya hilo kwa CCM halitawezekana! Hata kama Magufuli akiwa na utashi, CCM watamkwamisha tu!
 
Magufuri atakuja na baraza lisilopungua watu 32 ili awaridhishe wapiga kampeni wake.,na wale wataalamu wa matusi.
 
Haya ni masuala ya msingi kujadili, pia ili kupunguza gharama watendaji wakuu wanaostahili magari wakopeshwe magari ili wawe wanayahudumia wenyewe kwa mafuta na matengenezo hii itawfanya kuwa na nidhamu ya matumizi.
 
Back
Top Bottom