Muundo wa Serikali ya awamu ya tano

Muundo wa Serikali ya awamu ya tano

Rais - Lowassa
Waziri mkuu - Dr. John Pombe Magufuli

Mawaziri wataajiriwa kama kazi zingine kulingana na sifa kitaaluma na uzoefu wa kazi.

Msinitukane mimi, shambulieni hoja.
 
Waziri anaweza kuwakilishwa na waziri mwingine wa wizara yoyote. Je unajua kwamba Waziri akisafiri kaimu waziri anakuwa waziri mwingine na sio Naibu Waziri? Mara nyingi sana siku za nyuma Foreign Minister akisafiri, waziri wa sheria alikuwa akikaimu labda kwa kuwa walikuwa jengo moja wakati huo.

Isitoshe, Naibu Waziri haingii kwenye baraza la mawaziri hata siku moja. Katiba hairuhusu!
Wizara ya Dar es Salaam
 
Mtoa Mazda wizara 6 na 7 zote jukumu LA kushighulikia mazingira?
 
Vyeo vya wizara-waziri,naibu waziri,katibu mkuu,naibu katibu mkuu..haya ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma.hawa wote kazi zao ni zipi
 
Wakuu wanaosema cheo cha mkuu wa mkoa kifutwe ni wazi hawajasoma katiba vizuri.cheo cha mkuu wa mkoa kipo kikatiba lakinihakuna cheo cha mkuu wa wilaya kikatiba.
 
Swala la kupunguza mikoa sio tija ufanis mzur unafanywa kama maeneo yataongezwa ili viongoz,wawafikie wananch wao kwa urahis
 
Habari yenu Watanzania wenzangu,

Kila jambo na wakati wake kwa majira yake. Uchaguzi Mkuu unafanyika Oktoba, 2015 siku ya Jumapili. Si rahisi kubashiri nani ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha Urais pengine tusubiri kuona nini kitatokea.

Mara baada ya tarehe 25 Oktoba tutakuwa na mjadala mpana juu ya Muundo wa Serikali ambayo Rais Mpya ataiunda. Nina mawazo ambayo ningependa Rais ajaye ayaweke katika fikra zake na kuyafanyia kazi. Nayo ni haya yafuatayo;

1. Serikali iliyopo ni kubwa mno na ufanisi ni Mdogo; hivyo afikirie kupunguza ukubwa wa Serikali kwa kiwango kikubwa.

2. Muundo wa Utawala hauna tija

Ufafanuzi

1. Ukubwa wa Serikali
Kwa sasa kwa upande wa Tanzania Bara kuna Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wasaidizi wao. Kimsingi hawa wote kazi zao zinashabihiana. Hawa ni Wateule wa Rais na ni wawakilishi wa Taasisi ya Urais katika ngazi zao. Binafsi sioni kitu cha ziada na chenye manufaa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao kwa sehemu wanatumika kama Makada wa CCM. Ushauri wangu ni kuwa Cheo cha RC na DC kiondolewe tubaki na Watendaji ambao ni Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri. Tutaokoa fedha nyingi sana kwa hatua hii tu.

2. Muundo wa Utawala usio na tija
Tumekuwa na Wizara nyingi lakini ufanisi bado mdogo sana. Makusanyo ya kodi na wigo wa kodi bado ni mdogo, Tija katika sekta za uzalishaji bado ipo chini nk. Ushauri wangu ni kuwa na Wizara chache lakini zenye tija. Ninapendekeza Wizara zisizozidi 15 kama ifuatavyo;

1. Wizara ya Fedha, Uchumi na Uwekezaji,
2. Wizara ya Nishati na Madini,
3. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4. Wizara Maji, Ardhi na Maendeleo ya Makazi
5. Wizara ya Ulinzi na JKT
6. Wizara ya Afya, Usafi wa Mazingira na Ustawi wa Jamii
7. Wizara ya Mazingira, Maliasili na Utalii
8. Wizara ya Kilimo, Mifugo, Ushirika na Masoko
9. Wizara ya Viwanda na Biashara
10.Wizara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu
11.Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni
12. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
13. Wizara ya Elimu, Ufundi na Sayansi
14. Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
15. Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma

Hatuna sababu ya kuwa na Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI). Halmashauri ziwajibike moja kwa moja kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS). Kwa kufanya hivyo tutaokoa fedha nyingi sana na kuwa na utekelezaji wa haraka. Kwa hiyo Elimu bure kwa wote, Afya bure kwa wazee, watoto na wajawazito inawezekana kabisa.

Aidha, Rais akasimu Mamlaka yake ya uteuzi. Si busara kila uteuzi ufanywe chini ya Ofisi ya Rais. Hali hii imesababisha kujikweza na kuwa na kiburi kwa baadhi ya wateule. Mfano RC hawezi kumfanya chochote RAS kwa kuwa Mamlaka ya Uteuzi ni Rais; Wakuu wa Mashirika hawawezi kuwajibika moja kwa moja kwa Waziri husika badala yake hata wakivulunda inasubiliwa Mamlaka ya Uteuzi kutengua Uteuzi. Huu ni urasimu na ni kuchelewesha maendeleo.

Ninashauri Serikali ijayo izingatie haya. Sisi ni nchi changa lazima tuwe na namna bora zaidi ya kutumia raslimali zetu kwa matokeo makubwa.

Asanteni kwa michango yenu wana JF.

Sawa sawa mleta mada umemaliza ila bado nyingi zinatakiwa kumi name 13 wizara tuu
 
Naunga mkono mkuu, lakini angeongeza wizara moja ya mambo ya muungano. Pia manaibu wasiwepo. Tuwe na mawaziri 16 tu.

Mkuu,hauwezi kuwa na serikali ndogo kvile alafu usıwe na manaibu waziri.Mfano wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi,nı pana sana.Licha ya uwepo wa Makatibu wakuu NA wakurugenzi bado Naibu wazirı awepo na awe mwenye mamlaka makubwa kidogo.
 
Habari yenu Watanzania wenzangu,

Kila jambo na wakati wake kwa majira yake. Uchaguzi Mkuu unafanyika Oktoba, 2015 siku ya Jumapili. Si rahisi kubashiri nani ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha Urais pengine tusubiri kuona nini kitatokea.

Mara baada ya tarehe 25 Oktoba tutakuwa na mjadala mpana juu ya Muundo wa Serikali ambayo Rais Mpya ataiunda. Nina mawazo ambayo ningependa Rais ajaye ayaweke katika fikra zake na kuyafanyia kazi. Nayo ni haya yafuatayo;

1. Serikali iliyopo ni kubwa mno na ufanisi ni Mdogo; hivyo afikirie kupunguza ukubwa wa Serikali kwa kiwango kikubwa.

2. Muundo wa Utawala hauna tija

Ufafanuzi

1. Ukubwa wa Serikali
Kwa sasa kwa upande wa Tanzania Bara kuna Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wasaidizi wao. Kimsingi hawa wote kazi zao zinashabihiana. Hawa ni Wateule wa Rais na ni wawakilishi wa Taasisi ya Urais katika ngazi zao. Binafsi sioni kitu cha ziada na chenye manufaa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao kwa sehemu wanatumika kama Makada wa CCM. Ushauri wangu ni kuwa Cheo cha RC na DC kiondolewe tubaki na Watendaji ambao ni Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri. Tutaokoa fedha nyingi sana kwa hatua hii tu.

2. Muundo wa Utawala usio na tija
Tumekuwa na Wizara nyingi lakini ufanisi bado mdogo sana. Makusanyo ya kodi na wigo wa kodi bado ni mdogo, Tija katika sekta za uzalishaji bado ipo chini nk. Ushauri wangu ni kuwa na Wizara chache lakini zenye tija. Ninapendekeza Wizara zisizozidi 15 kama ifuatavyo;

1. Wizara ya Fedha, Uchumi na Uwekezaji,
2. Wizara ya Nishati na Madini,
3. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
4. Wizara Maji, Ardhi na Maendeleo ya Makazi
5. Wizara ya Ulinzi na JKT
6. Wizara ya Afya, Usafi wa Mazingira na Ustawi wa Jamii
7. Wizara ya Mazingira, Maliasili na Utalii
8. Wizara ya Kilimo, Mifugo, Ushirika na Masoko
9. Wizara ya Viwanda na Biashara
10.Wizara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu
11.Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni
12. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
13. Wizara ya Elimu, Ufundi na Sayansi
14. Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
15. Ofisi ya Rais-Utumishi wa Umma

Hatuna sababu ya kuwa na Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI). Halmashauri ziwajibike moja kwa moja kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS). Kwa kufanya hivyo tutaokoa fedha nyingi sana na kuwa na utekelezaji wa haraka. Kwa hiyo Elimu bure kwa wote, Afya bure kwa wazee, watoto na wajawazito inawezekana kabisa.

Aidha, Rais akasimu Mamlaka yake ya uteuzi. Si busara kila uteuzi ufanywe chini ya Ofisi ya Rais. Hali hii imesababisha kujikweza na kuwa na kiburi kwa baadhi ya wateule. Mfano RC hawezi kumfanya chochote RAS kwa kuwa Mamlaka ya Uteuzi ni Rais; Wakuu wa Mashirika hawawezi kuwajibika moja kwa moja kwa Waziri husika badala yake hata wakivulunda inasubiliwa Mamlaka ya Uteuzi kutengua Uteuzi. Huu ni urasimu na ni kuchelewesha maendeleo.

Ninashauri Serikali ijayo izingatie haya. Sisi ni nchi changa lazima tuwe na namna bora zaidi ya kutumia raslimali zetu kwa matokeo makubwa.

Asanteni kwa michango yenu wana JF.

Haya yote yatatekelezeka tukipata tu katiba ya wananchi,chini ya utawala wa CCM hayo kufanyika ni ndoto.
 
Wakuu wanaosema cheo cha mkuu wa mkoa kifutwe ni wazi hawajasoma katiba vizuri.cheo cha mkuu wa mkoa kipo kikatiba lakinihakuna cheo cha mkuu wa wilaya kikatiba.

Yeyote mwenye utimamu wa akili hawezi sema nafasi za wakuu wa Mikoa zifutwe.Kınachotakiwa nı utaratibu bora wa namna wanavyotakiwa kupatikana.Kuna watu ambao hata kwa uelewa wao wanatamani kusema hata mawazirı wasiwepo.Wengi wetu tunachangia tukiwa na vınasaba vya wivu.
 
katiba mpya ndio muarobaini wa mambo yote hayo
 
Mimi naona mawazo yote hadi sasa yanajenga..Lamsingi napendekeza serkali yeyote itakayo kaimu madaraka isichelewe kupeleka miswada ya haya mapendekezo tunayotoa humu ndani wakati tukisibiria mchakato mpya wa katiba ya wananchi..

Naunga hoja mkono 100/100..
 
No need to have no.11. Ministry of Sports Arts and Culture the activities can go to no. 14 or under an independent governing body financed by the government
 
16. Mambo ya Nje17. Mambo ya MuunganoMawaziri,Makatibu Wakuu, Ras na Wakurugenzi wa Miji,Manispaa na wilaya tosha!
Tunataka Ilani ya Ukawa(Chadema) Inayofanana na Rasmu ya katiba ya warioba. Magufuli Usitudanganye lolote wewe ni ileile kasoro majina
 
Safari hii apatikane Waziri mwenye asili ya ki asia hasa kwenye wizara ya fedha...hata akiwa siyo raia.
 
  • Magufuli Pombe Asitudanganye Eti ataweka Baraza Dogo la Mawaziri, Wakati waliomuweka agombee Ilani yao haisemi hivyo Wananchi tafadhari sana Msdanganyike
 
Iko powa but wilaya Na mikoa ziwe kama awali,kwani sion mabadiliko licha ya kupeana madaraka na vyeo,huku pesa za watanzania zikifujwa kwa kasi
 
Namba 11 ongeza habari. Kuna mdau amesema kuwa manaibu waziri wasiwepo maana ni kweli hawana tija.
 
Back
Top Bottom