Muumini wa shetani

Muumini wa shetani

Wa Nyumbani

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
438
Reaction score
67
Waamini walikuwa kanisani, mara shetani akaingia ghafla na kusimama mbele altareni. Mlango ukawa mdogo! watu walitoka nje wakipiga makelele! Baada ya dakika 2 hivi watu wote walikuwa wametoka nje isipokuwa mwenyekiti wa kanisa hilo. Shetani akamuuliza mwenyekiti,

shetani: wewe ndio huniogopi sio?
Mwenyekiti: ndio sikuogopi.
shetani: unasema huniogopi mimi? shetani akasema kwa ukali zaidi.
Mwenyekiti: ndiyo sikuogopi

Hapo shetani lilishangaa.

shetani: kwa nini huniogopi
Mwenyekiti: wewe ni shemeji yangu nitakuogopa kwa sababu gani?
shetani: ehe, mimi shemeji yako kwa vipi?
Mwenyekiti: nimemuoa dada yako na wote tuna tabia zinazofanana.

Shetani akatingisha kichwa, akaondoka.
 
Back
Top Bottom