Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,869
- 828,403
Tony Kapola anatumia nguvu nyingi sana kuusafisha uongo wa mkewe kwenye muujiza wa gesi.. Anatumia cover up ya Biblia takatifu na vijembe vyenye matusi ndani yake! Lakini hatafanikiwa bali ndio anazidi kuharibu
Ukweli ni kwamba hakuna watu mahiri wa kutoa mifano ya uongo kama hawa wahubiri na wake zao.. Kuna wakati mtu anatoa mfano wa uongo ama ushuhuda feki mpaka inakera
Mke wa Tony Kapola alichotoa ni ushuhuda wa muujiza feki ambao hakutegemea kama utaenda viral mitandaoni
Waumini ni kama mikondoo . huwa hawahoji kwakuwa wanahubiriwa na wanachotakiwa kufanya ni kuamini... Sasa kwa dunia ya leo ya utandawazi unaweza kuwa control waumini wako lakini si watu wengine nje ya waumini wako
Twendeni na huu uhalisia wa maisha muone yule mama na mumewe walivyo majuha
Kwa ukwasi walionao na maisha wanayoishi haiingii akilini hata siku moja kwamba wanatumia jiko la gesi lisilo na option ya umeme.. Never!
Kwa maisha wanayoishi haiingilii akilini kwamba wanatumia gesi yenye regulator ya kawaida isiyoonesha kiwango cha gesi.. Siku hizi kuna regulator za kisasa zinazokuonesha kiwango cha gesi kilichopo
Kwa maisha ya ukwasi wanayoishi haingilii akilini kabisa kwamba hawana wafanyakazi wa ndani kama mpishi, mfanya usafi nknk
Inawezekana hata kama wapo wafanyakazi lakini mzee hupenda kula kilichopikwa na mkewe ama kuna siku mama huamua kuingia mwenyewe jikoni! Na siku hiyo ndiyo ikawa hivyo na kukutana na gesi ikiwa imekwisha!
Hapa kuna jambo lingine la kuzingatia.. Kwakuwa mama si mpishi wa mara kwa mara hivyo hajui kwamba kuna wakati regulator hufungwa na mtu aliyetumia mara ya mwisho...Hapo bila kuifungua regulator iruhusu gesi kupita, kule kwenye burner hakutawaka!
Pengine bila kulijua hili mama akaripoti kwa mzee .. Mzee akaja jiloni akapiga maombi akaupuliza mtungi ukajaa gesi akafunguq regulator. Mama akawasha kwenye burner.. Gesi ikawaka kwa kasi.. Na ikawa ni muujiza tayari😂😂😂
Hapa kuna mtu aliingizwa cha kike naye akaenda kuwaingiza wengine! Mtungi wa gesi sio puto jamani.. Kwamba utapuliza na kuona kabisa linajaa hewa! Kapola yeye kapuliza mtungi wa gesi na kuujaza gesi.. Sasa sijui ni ule mkubwa au ni ile inayogawiwa vijijini maarufu kama mitungi ya mama!?🤔😩
Kwa uzoefu wangu kwenye miujiza ya dharura kama hiyo.. Hakukuwa na haja Tony aanze kuupuliza mtungi bali ilikuwa ni kitendo cha kuamrisha ama kuomba kiimani na jambo likawa!
Ni kama tu wale wachawi konki.. Wao hawahitaji pesa! Maana hawana matumizi nazo kwakuwa kila watakacho hukipata kwa kutamka tu!
Kapola alikuwa na uwezo wa kutamka shibe na wakashiba.. Alikuwa na uwezo wa kutamka chakula kiive bila gesi na ikawa nknk.. Lakini muujiza wa kupuliza mtungi mtupu na ukajaa gesi ni uongo uliopitiliza!