Nafikiri kulikuwa na complication nyingine ambayo nurse asingeweza kuhandle, ndiyo maana Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Fredrick Mlekwa, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa alisema "Ni kweli tumefuatilia kuhusu suala la muuguzi wa zamu kuongea na simu, tumemuhoji amekiri muda huo alikuwa akiongea na simu na kufafanua kuwa alikuwa akiwasiliana na daktari wa zamu kwa ajili ya kuomba msaada zaidi wa kumsaidia mzazi huyo,"alisema na kuongeza kwamba suala hilo watazidi kulichunguza. Dkt. Mlekwa amerejea kutoa wito kwa wakazi wa Shinyanga kuwa na tabia ya kuheshimu taratibu za hospitali zilizopo na kueleza kuwa ni kosa la kisheria kwa wananchi wa kawaida kuingia ndani ya wodi ya wazazi, hali ambayo inaweza kusababisha maambukizo mbalimbali kwa watoto wanaozaliwa kwa vile wanakuwa hawapatiwa chanjo za kinga.