Muswada wa vyama vya siasa ni mwiba kwa upinzani

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Viongozi wa vyama vya upinzani na asasi za kiraia nchini Tanzania wameonesha kushtushwa na mswada wa mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Mswada huo, kwa mujibu wa wanaoupinga unalenga kurasmisha kisheria uminywaji wa vyama vya siasa na demokrasia kwa ujumla nchini Tanzania.

Tayari mswada huo umeshawasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita, lakini je ni mambo gani hasa yanayolalamikiwa kwenye muswada huo?

1.Kifungu cha 5A kinataka msajili kupewa taarifa kimaandishi na taasisi yeyote ya ndani ama ya nje ya Tanzania itakapotaka kutoa mafunzo ya kiraia ama ya kujenga uwezo kwa chama cha siasa na kutaja wahusika, malengo na nyenzo zitakazotumika katika mafunzo hayo.

Msajili anayo nguvu ya kutoa kibali ama kukataa kufanyika kwa mafunzo hayo na endapo yatafanyika bila kibali taasisi hiyo inaweza kupigwa faini ya mpaka shilingi milioni 30 na watu watakaokutwa na hatia ya kwenda kinyume ni kifungu hicho wanaweza kufungwa kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja gerezani.

2.Kifungu cha 5B cha muswada kinampa nguvu, msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania kuomba na kupewa taarifa yeyote ile ya chama chochote cha siasa.

Afisaa yeyote wa chama cha siasa ambaye ataenda kinyume na takwa hilo, yaani kutokutoa taarifa husika atakuwa ametenda kosa na akikutwa na hatia atapigwa faini ya kuanzia shilingi milioni moja (1)mpaka milioni kumi(10) au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi 12.

Hata baada ya adhabu hiyo, afisa huyo ama chama hicho bado kitatakiwa kutoa taarifa zilizohitajika na iwapo taarifa itaendelea kumininywa basi chama hicho kinaweza kusimamishwa ama kufutiwa usajili.

Wapinzani Tanzania wanadai iwapo kifungu hicho kitapita, mipango yote ya kimkakati ya vyama vya siasa itakuwa wazi na inaweza kutumiwa na serikali katika kuwaminya.

Hoja yao kuu ni kwamba msajili ni mteule wa Rais, ambaye ni mwanachama pia wa chama tawala. Hivyo ofisi ya msajili inaweza kutumika dhidi yao.

3.Kifungu cha 6 cha muswada kinamlinda msajili na wanyakazi wa ofisi yake dhidi ya kufunguliwa mashtaka: "Shauri lolote halitafunguliwa dhidi ya Msajili, Naibu Msajili, Mkurugenzi ama maafisa wengine chini ya Msajili kwa lolote watakalolifanya ama kutolifanya kwa nia njema chini ya sharia hii," kinasomeka kifungu hicho.

4.Kifungu cha 11C kinaruhusu vyama vya siasa kuunda ushirikiano wa kufikia malengo ya pamoja ya kisiasa lakini kanuni za kuunda ushirikiano zitatungwa na waziri. (Waziri huyo ni wa chama tawala.)

5.Kifungu cha 19 A kinasema msajili anaweza kukisimamisha usajili wa chama kwa sababu atakazozitaja na kwa muda atakaouweka mpaka ili chama hicho kiweze kujirekebisha.
Chama ambacho kimesimamishiwa usajili hakitaweza kufanya shughuli zote za kisiasa.
Na iwapo msajili ataona chama hicho hakijajirekebisha anaweza kukifutia usajili.

Kifungu hiki, wapinzani wanadai kinaweza kutumika kuzuia vyama kushiriki uchaguzi kwa kusimamishiwa usajili kabla ya uchaguzi na kurudishiwa usajili baada ya uchaguzi kupita.

6.Kifungu 21 E kinampa msajili nguvu ya kumsimamisha mwananchama yeyeyote wa chama chochote cha siasa ambaye atavunja kifungu chochote cha sheria hiyo.
Waziri pia atatunga kanuni za namna gani wanachama wa vyama vya siasa wanaweza kusimamishwa.

7.Kifungu cha 22, Swala la mapato ya vyama vya siasa pia linapendekezwa kufanyiwa mabadiliko kupitia muswada huo na endapo utapitishwa itakuwa ni marufuku kwa vyama vya siasa kupokea fedha kutoka taasisi au mtu yeyote nje ya nchi kama kinavyopendekeza kifungu cha 22.

8.Kifungu cha 24 kinampa uwezo msajili kuzuia ruzuku ya chama kwa muda atakaouweka wazi au usiowekwa wazi akiona matumizi ya fedha hizo yana mashaka.
Pia chama kitakachopata hati chafu ya mkaguzi haitapewa ruzuku kwa miezi 6 (sita).

9.Msajili pia wakati wowote ule anaweza kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu (CAG) kufanya ukaguzi maalum pale atakapokuwa na mashaka na matumizi ya rasilimali za chama cha siasa.

Akiongea na mwandishi wa BBC Zuhura Yunus hivi karibuni Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif amesema endapo muswada huo utapita vyama vya upinzani vitakuwa na wakati mgumu kujiendesha.

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema hatua hiyo ni muendelezo wa kile alichokiita ni hatua ya nne ya udikteta ambayo ni kudhibiti vyama vya siasa.

Hata hivyo msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amesema muswada huo hauna nia yoyote ovu dhidi ya vyama vya siasa na amewataka wadau wote wenye maoni ya kuboresha wayawasilishe kwenye warsha itakayofanyika Zanzibar Desemba 21-22.

"Kama kweli wana hoja za msingi basi wataziwasiisha kwenye warsha ya mashauriano itakayofanyika Zanzibar...lakini hakuna nia yoyote inayokusudiwa kutekelezwa kupitia muswada huu," jaji Mutungi ameliambia gazeti la Kingereza la The Citizen.

----------
Wapinzani mnalo, nyie ndo mnasababisha yafuatayo...
1.Kuchelewesha ndege zetu kuja Novemba 2018.
2. Kuchelewa Kuhamia Dodoma kabla ya mwaka kuisha.
3. Kuingiza korosho za nje na kuendekeza kangomba ambapo wakulima wamecheleweshewa malipo.
4. Mmesababisha mafao ya kustaafu kupungua kutoka 50% hadi 25%
5. Mmesababisha Makato ya HESLB kupanda kutoka 8% hadi 15%
6. Mmesababisha tukose misaada na mikopo ya nje katika sakata la ushoga.
7.Mmesababisha Mishahara kutoongezeka, madaraja hakuna kupanda tangu ajira mpya ya 2012, 213, ... ,increment hakuna.
8. Milioni 50 kila kijiji haziji kwasababu mlishaandaa saccos za kuzipiga. Mmenoa, Hampati.

Mswaada huu utawanyoosha vizuri. Mkibishi TUNAWAFYEKELEA MBALI.

Nyie ndo mnasababisha wote tuisome namba wakati "WACHA WAISOME NAMBAA EEH" ilikuwa inawahusu nyie.
 
Hahahaaaaaa! Kweli tuendako siko kabisa. Hazina nia njema hata kidogo. Naamini lengo hasa ni kuilinda CCM kiendelee milele na milele. Walioandika haya ni watu wabaya Sana. Hata was I on na dini ni Weka. Siamini km hitaji lao ni Pesa tu. Hakika vyama vya upinzani havitakuwepo labda vile vya kimkakati na Chama Tawala. Wasifikiri wanawakomoa wapinzani bali tunajikomoa watz. Wakibaki CCM pekee watafanya mabaya zaidi. Watangaze tu kufuta vyama vyote tuwe na kimoja Maisha yaendelee.
 
Kwa huu upuuzi unaoendelea tusitegemee maendeleo.
Watu wenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo hawawezi kujishughulisha na upupu wa namna hii. Naisitikia nchi yangu Tanzania.
 
Hati wakifanya kitu kwa nia njema hawawezi kushitakiwa. Mfano yale waliofanya kule Korogwe na kumtangaza mtu kupita bila kupingwa. Kosa no kosa ulitende kwa nia njema au vinginevyo. Tume ya uchaguzi lazima wawe accountable kwa vitendo vyao. Mswada huo ni wa kunyonga demokrasia na kuua upinzani. Bila upinzani basi li CCM kama alivyosema Nyerere litasinzia na kufanya litakavyo.
 
Dah hilo dubwasha likipita ndo tumekwisha kabisa. Hasa kwa ninavyowafahamu wabunge wa ccm, lazima litapita tu.

Maskini Tanzania yetu!
 
Ntashangaa wabunge wa ccm wakipitisha utafikiri siku moja hawata hamia upinzan mnao tegemea siasa Ndiyo muishi kazi mnayo
Hata yule Dr naniii...... Sasa hiv ni baloz alikua sisiem akaenda upinzan akaibua ishu ya ufisad akarud tena sisiem
Je hii sheria ingekuwepo angeweza kuibua ule ufisad tukaujua????? Yetu macho
 
hiyo december 21 wapinzani wahakikishe wanakwenda huko zanzibar na kutoa hoja zao, wakipuuza huo mswaada utapita na huyo kiazi mutungi atesama "tulishirikisha wadau"!
 
Viongozi wa vyama vya upinzani na asasi za kiraia nchini Tanzania wameonesha kushtushwa na mswada wa mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Mswada huo, kwa mujibu wa wanaoupinga unalenga kurasmisha kisheria uminywaji wa vyama vya siasa na demokrasia kwa ujumla nchini Tanzania.

Tayari mswada huo umeshawasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita, lakini je ni mambo gani hasa yanayolalamikiwa kwenye muswada huo?

1.Kifungu cha 5A kinataka msajili kupewa taarifa kimaandishi na taasisi yeyote ya ndani ama ya nje ya Tanzania itakapotaka kutoa mafunzo ya kiraia ama ya kujenga uwezo kwa chama cha siasa na kutaja wahusika, malengo na nyenzo zitakazotumika katika mafunzo hayo.

Msajili anayo nguvu ya kutoa kibali ama kukataa kufanyika kwa mafunzo hayo na endapo yatafanyika bila kibali taasisi hiyo inaweza kupigwa faini ya mpaka shilingi milioni 30 na watu watakaokutwa na hatia ya kwenda kinyume ni kifungu hicho wanaweza kufungwa kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja gerezani.

2.Kifungu cha 5B cha muswada kinampa nguvu, msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania kuomba na kupewa taarifa yeyote ile ya chama chochote cha siasa.

Afisaa yeyote wa chama cha siasa ambaye ataenda kinyume na takwa hilo, yaani kutokutoa taarifa husika atakuwa ametenda kosa na akikutwa na hatia atapigwa faini ya kuanzia shilingi milioni moja (1)mpaka milioni kumi(10) au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi 12.

Hata baada ya adhabu hiyo, afisa huyo ama chama hicho bado kitatakiwa kutoa taarifa zilizohitajika na iwapo taarifa itaendelea kumininywa basi chama hicho kinaweza kusimamishwa ama kufutiwa usajili.

Wapinzani Tanzania wanadai iwapo kifungu hicho kitapita, mipango yote ya kimkakati ya vyama vya siasa itakuwa wazi na inaweza kutumiwa na serikali katika kuwaminya.

Hoja yao kuu ni kwamba msajili ni mteule wa Rais, ambaye ni mwanachama pia wa chama tawala. Hivyo ofisi ya msajili inaweza kutumika dhidi yao.

3.Kifungu cha 6 cha muswada kinamlinda msajili na wanyakazi wa ofisi yake dhidi ya kufunguliwa mashtaka: "Shauri lolote halitafunguliwa dhidi ya Msajili, Naibu Msajili, Mkurugenzi ama maafisa wengine chini ya Msajili kwa lolote watakalolifanya ama kutolifanya kwa nia njema chini ya sharia hii," kinasomeka kifungu hicho.

4.Kifungu cha 11C kinaruhusu vyama vya siasa kuunda ushirikiano wa kufikia malengo ya pamoja ya kisiasa lakini kanuni za kuunda ushirikiano zitatungwa na waziri. (Waziri huyo ni wa chama tawala.)

5.Kifungu cha 19 A kinasema msajili anaweza kukisimamisha usajili wa chama kwa sababu atakazozitaja na kwa muda atakaouweka mpaka ili chama hicho kiweze kujirekebisha.
Chama ambacho kimesimamishiwa usajili hakitaweza kufanya shughuli zote za kisiasa.
Na iwapo msajili ataona chama hicho hakijajirekebisha anaweza kukifutia usajili.

Kifungu hiki, wapinzani wanadai kinaweza kutumika kuzuia vyama kushiriki uchaguzi kwa kusimamishiwa usajili kabla ya uchaguzi na kurudishiwa usajili baada ya uchaguzi kupita.

6.Kifungu 21 E kinampa msajili nguvu ya kumsimamisha mwananchama yeyeyote wa chama chochote cha siasa ambaye atavunja kifungu chochote cha sheria hiyo.
Waziri pia atatunga kanuni za namna gani wanachama wa vyama vya siasa wanaweza kusimamishwa.

7.Kifungu cha 22, Swala la mapato ya vyama vya siasa pia linapendekezwa kufanyiwa mabadiliko kupitia muswada huo na endapo utapitishwa itakuwa ni marufuku kwa vyama vya siasa kupokea fedha kutoka taasisi au mtu yeyote nje ya nchi kama kinavyopendekeza kifungu cha 22.

8.Kifungu cha 24 kinampa uwezo msajili kuzuia ruzuku ya chama kwa muda atakaouweka wazi au usiowekwa wazi akiona matumizi ya fedha hizo yana mashaka.
Pia chama kitakachopata hati chafu ya mkaguzi haitapewa ruzuku kwa miezi 6 (sita).

9.Msajili pia wakati wowote ule anaweza kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu (CAG) kufanya ukaguzi maalum pale atakapokuwa na mashaka na matumizi ya rasilimali za chama cha siasa.

Akiongea na mwandishi wa BBC Zuhura Yunus hivi karibuni Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif amesema endapo muswada huo utapita vyama vya upinzani vitakuwa na wakati mgumu kujiendesha.

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema hatua hiyo ni muendelezo wa kile alichokiita ni hatua ya nne ya udikteta ambayo ni kudhibiti vyama vya siasa.

Hata hivyo msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amesema muswada huo hauna nia yoyote ovu dhidi ya vyama vya siasa na amewataka wadau wote wenye maoni ya kuboresha wayawasilishe kwenye warsha itakayofanyika Zanzibar Desemba 21-22.

"Kama kweli wana hoja za msingi basi wataziwasiisha kwenye warsha ya mashauriano itakayofanyika Zanzibar...lakini hakuna nia yoyote inayokusudiwa kutekelezwa kupitia muswada huu," jaji Mutungi ameliambia gazeti la Kingereza la The Citizen.

----------
Wapinzani mnalo, nyie ndo mnasababisha yafuatayo...
1.Kuchelewesha ndege zetu kuja Novemba 2018.
2. Kuchelewa Kuhamia Dodoma kabla ya mwaka kuisha.
3. Kuingiza korosho za nje na kuendekeza kangomba ambapo wakulima wamecheleweshewa malipo.
4. Mmesababisha mafao ya kustaafu kupungua kutoka 50% hadi 25%
5. Mmesababisha Makato ya HESLB kupanda kutoka 8% hadi 15%
6. Mmesababisha tukose misaada na mikopo ya nje katika sakata la ushoga.
7.Mmesababisha Mishahara kutoongezeka, madaraja hakuna kupanda tangu ajira mpya ya 2012, 213, ... ,increment hakuna.
8. Milioni 50 kila kijiji haziji kwasababu mlishaandaa saccos za kuzipiga. Mmenoa, Hampati.

Mswaada huu utawanyoosha vizuri. Mkibishi TUNAWAFYEKELEA MBALI.

Nyie ndo mnasababisha wote tuisome namba wakati "WACHA WAISOME NAMBAA EEH" ilikuwa inawahusu nyie.
Kama kweli muswada ndivyo ulivyo,haina haja ya kuuendeleza huo muswada, basi bora uletwe muswada wa kurudisha mfumo wa chama kimoja cha siasa,vinginevyo kwa muswada huo ccm ipendwe isipendwe itatawala milele mpaka mwisho wa dunia.Kimsingi kama kweli ndiyo huo muswada, vyama vyote vya kweli vya upinzani vitaondoshwa.Miswada inapopelekwa bungeni izingatie maslahi mapana ya taifa siyo kwa kukibeba chama fulani.
 
Huo muswaada upinzani tuendelea kuupinga kwa nguvu zote na tunajua watoa misaada ndio watatujibia vizuri.
Embu wajiulize kama tu swala la takwimu. na kuwazuia watoto walipata mimba kuendelea na masomo. na swala la mashoga liliwaghalimu vile.

Je kwa kutunga hiyo sheria za kipumbavu za kutaka kuua vyama vya upinzani. unafikiri wahisani wataamua nini?
 
'Kwa Hapa tukipofikia kutokana Na Ombwe la Uongozi wa Rais Kikwete tunahitaji Rais Kama Kagame' - Wachambuzi Na Wanasiasa Uchwara 2005-2015
 
Viongozi wa vyama vya upinzani na asasi za kiraia nchini Tanzania wameonesha kushtushwa na mswada wa mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa.

Mswada huo, kwa mujibu wa wanaoupinga unalenga kurasmisha kisheria uminywaji wa vyama vya siasa na demokrasia kwa ujumla nchini Tanzania.

Tayari mswada huo umeshawasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita, lakini je ni mambo gani hasa yanayolalamikiwa kwenye muswada huo?

1.Kifungu cha 5A kinataka msajili kupewa taarifa kimaandishi na taasisi yeyote ya ndani ama ya nje ya Tanzania itakapotaka kutoa mafunzo ya kiraia ama ya kujenga uwezo kwa chama cha siasa na kutaja wahusika, malengo na nyenzo zitakazotumika katika mafunzo hayo.

Msajili anayo nguvu ya kutoa kibali ama kukataa kufanyika kwa mafunzo hayo na endapo yatafanyika bila kibali taasisi hiyo inaweza kupigwa faini ya mpaka shilingi milioni 30 na watu watakaokutwa na hatia ya kwenda kinyume ni kifungu hicho wanaweza kufungwa kati ya miezi sita mpaka mwaka mmoja gerezani.

2.Kifungu cha 5B cha muswada kinampa nguvu, msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania kuomba na kupewa taarifa yeyote ile ya chama chochote cha siasa.

Afisaa yeyote wa chama cha siasa ambaye ataenda kinyume na takwa hilo, yaani kutokutoa taarifa husika atakuwa ametenda kosa na akikutwa na hatia atapigwa faini ya kuanzia shilingi milioni moja (1)mpaka milioni kumi(10) au kifungo kisichopungua miezi sita na kisichozidi miezi 12.

Hata baada ya adhabu hiyo, afisa huyo ama chama hicho bado kitatakiwa kutoa taarifa zilizohitajika na iwapo taarifa itaendelea kumininywa basi chama hicho kinaweza kusimamishwa ama kufutiwa usajili.

Wapinzani Tanzania wanadai iwapo kifungu hicho kitapita, mipango yote ya kimkakati ya vyama vya siasa itakuwa wazi na inaweza kutumiwa na serikali katika kuwaminya.

Hoja yao kuu ni kwamba msajili ni mteule wa Rais, ambaye ni mwanachama pia wa chama tawala. Hivyo ofisi ya msajili inaweza kutumika dhidi yao.

3.Kifungu cha 6 cha muswada kinamlinda msajili na wanyakazi wa ofisi yake dhidi ya kufunguliwa mashtaka: "Shauri lolote halitafunguliwa dhidi ya Msajili, Naibu Msajili, Mkurugenzi ama maafisa wengine chini ya Msajili kwa lolote watakalolifanya ama kutolifanya kwa nia njema chini ya sharia hii," kinasomeka kifungu hicho.

4.Kifungu cha 11C kinaruhusu vyama vya siasa kuunda ushirikiano wa kufikia malengo ya pamoja ya kisiasa lakini kanuni za kuunda ushirikiano zitatungwa na waziri. (Waziri huyo ni wa chama tawala.)

5.Kifungu cha 19 A kinasema msajili anaweza kukisimamisha usajili wa chama kwa sababu atakazozitaja na kwa muda atakaouweka mpaka ili chama hicho kiweze kujirekebisha.
Chama ambacho kimesimamishiwa usajili hakitaweza kufanya shughuli zote za kisiasa.
Na iwapo msajili ataona chama hicho hakijajirekebisha anaweza kukifutia usajili.

Kifungu hiki, wapinzani wanadai kinaweza kutumika kuzuia vyama kushiriki uchaguzi kwa kusimamishiwa usajili kabla ya uchaguzi na kurudishiwa usajili baada ya uchaguzi kupita.

6.Kifungu 21 E kinampa msajili nguvu ya kumsimamisha mwananchama yeyeyote wa chama chochote cha siasa ambaye atavunja kifungu chochote cha sheria hiyo.
Waziri pia atatunga kanuni za namna gani wanachama wa vyama vya siasa wanaweza kusimamishwa.

7.Kifungu cha 22, Swala la mapato ya vyama vya siasa pia linapendekezwa kufanyiwa mabadiliko kupitia muswada huo na endapo utapitishwa itakuwa ni marufuku kwa vyama vya siasa kupokea fedha kutoka taasisi au mtu yeyote nje ya nchi kama kinavyopendekeza kifungu cha 22.

8.Kifungu cha 24 kinampa uwezo msajili kuzuia ruzuku ya chama kwa muda atakaouweka wazi au usiowekwa wazi akiona matumizi ya fedha hizo yana mashaka.
Pia chama kitakachopata hati chafu ya mkaguzi haitapewa ruzuku kwa miezi 6 (sita).

9.Msajili pia wakati wowote ule anaweza kumtaka Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu (CAG) kufanya ukaguzi maalum pale atakapokuwa na mashaka na matumizi ya rasilimali za chama cha siasa.

Akiongea na mwandishi wa BBC Zuhura Yunus hivi karibuni Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif amesema endapo muswada huo utapita vyama vya upinzani vitakuwa na wakati mgumu kujiendesha.

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema hatua hiyo ni muendelezo wa kile alichokiita ni hatua ya nne ya udikteta ambayo ni kudhibiti vyama vya siasa.

Hata hivyo msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amesema muswada huo hauna nia yoyote ovu dhidi ya vyama vya siasa na amewataka wadau wote wenye maoni ya kuboresha wayawasilishe kwenye warsha itakayofanyika Zanzibar Desemba 21-22.

"Kama kweli wana hoja za msingi basi wataziwasiisha kwenye warsha ya mashauriano itakayofanyika Zanzibar...lakini hakuna nia yoyote inayokusudiwa kutekelezwa kupitia muswada huu," jaji Mutungi ameliambia gazeti la Kingereza la The Citizen.

----------
Wapinzani mnalo, nyie ndo mnasababisha yafuatayo...
1.Kuchelewesha ndege zetu kuja Novemba 2018.
2. Kuchelewa Kuhamia Dodoma kabla ya mwaka kuisha.
3. Kuingiza korosho za nje na kuendekeza kangomba ambapo wakulima wamecheleweshewa malipo.
4. Mmesababisha mafao ya kustaafu kupungua kutoka 50% hadi 25%
5. Mmesababisha Makato ya HESLB kupanda kutoka 8% hadi 15%
6. Mmesababisha tukose misaada na mikopo ya nje katika sakata la ushoga.
7.Mmesababisha Mishahara kutoongezeka, madaraja hakuna kupanda tangu ajira mpya ya 2012, 213, ... ,increment hakuna.
8. Milioni 50 kila kijiji haziji kwasababu mlishaandaa saccos za kuzipiga. Mmenoa, Hampati.

Mswaada huu utawanyoosha vizuri. Mkibishi TUNAWAFYEKELEA MBALI.

Nyie ndo mnasababisha wote tuisome namba wakati "WACHA WAISOME NAMBAA EEH" ilikuwa inawahusu nyie.
Sasa upinzani unasababishaje kukwamisha maendeleo nchini?? Fedha za maendeleo zinashikiliwa na upinzani? Awamu hii maccm yatazoa kinyesi lumumba .
 
Back
Top Bottom