MUSWADA WA MADINI - Why now? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MUSWADA WA MADINI - Why now?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by consigliori, Apr 15, 2010.

 1. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MKUTANO wa 19 wa Bunge unaanza leo (13/4/2010) mjini Dodoma, huku Rais Jakaya Kikwete akiwa ameomba Muswada wa Sheria ya Madini upitishwe kwenye mkutano huo pekee badala ya taratibu za kawaida ambazo hutaka suala hilo lifanyike kwenye mikutano mitatu ya chombo hicho cha kutunga sheria.


  Habari zilizolifikia gazeti hili (Mwananchi) jana zinaeleza kwamba Rais Kikwete, ambaye moja ya ahadi zake kubwa ilikuwa ni kushughulikia suala la madini, amedhamiria kuhakikisha kero zote zilizopo kwenye sekta hiyo zinajadiliwa na Bunge na kuweka sheria itakayozimaliza.

  Imeelezwa kuwa Rais Kikwete, amesaini hati maalumu ya dharura kuliomba Bunge lijadili muswada huo katika hatua zote na kuupitisha katika kikao hicho, tofauti na miswada mingine ambayo hutakiwa kusomwa kwenye mikutano mitatu kabla ya kupitishwa.

  Source - Mwananchi.

  Kwa maoni yangu nadhani muswada huu ulipaswa kuwa umeletwa mapema zaidi ili ujadiliwe vizuri na wataalamu mbalimbali pamoja na wananchi kwa ujumla kabla haujapelekwa Bungeni. Hii ni kutokana na ukweli kwamba sector ya madini ni eneo ambalo lingepaswa kuchangia kwa kiasi kikubwa ktk uchumi kuliko ilivyo sasa.

  Kitendo cha kupeleka mswada huu kama dharura mi inanipa shida sana, sijui JK alikuwa wapi kuadress issue ya Sector ya Madini mpaka akumbushwe kuwa katika ilani ya CCM ktk uchaguzi wa 2005, waliahidi kushughulikia matitizo ktk sector hii. Hii move kwa maoni yangu inauhusiano na uchaguzi mkuu ujao. WATANZANIA TUWE MACHO.
   
 2. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huo muswada una maslahi kwa taifa?!
  Kwangu hilo ndo la msingi, hajalishi umekuja lini na umekuwa wa dharula au la!

  Wabunge chonde chonde kupitisha vitu bila kusoma, tunaomba muusome kwa umakini na ikiwezekana uwekwe hapa jamvini ili tuwasaidie kuusoma na kuuchambua kabla hamjaupitisha.

  Maana kuna wabunge wengine vilaza sidhani hata kama huwa wanasoma miswada!
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mbunge gani atasoma wakati woote sasawanawaza uchaguzi tu!!!!!!!!!!
   
Loading...