Muswada: Jinai mtumishi wa uma atakayekopa bila kupata kibali cha waziri wa fedha

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,130
8,351
Kuna muswada umefikishwa bungeni wa kutaka kuwachukulia hatua watumishi wa umma watakao kopa kwenye taasisi za fedha bila kupata kibali cha waziri wa fedha...iwapo atabainika kutakua na fine ya mil 5 au kifungo cha miaka kadhaa au vyote pamoja. Nafikiri namba zinasomeka
 
OC za kuwawezesha kufanya kazi zimezuiwa,hata kufanya maendeleo binafsi kwa kupitia mikopo itakayokatwa kwenye mishahara yao nayo ni nongwa??,hivi hawa watumishi wameikosea nn haswaa serikali hii?,watakuwa na morali ya kufanya kazi kweli?,hivi wanasiasa wetu huko bungeni wapo kwa ajili ya nani haswaa?
 
Huo muswaada ni kwa wakuu wa taasisi za umma. Utawataka kuomba kibali hazina kabla ya kukopa. Source ITV habari
 
Itv walichemka kwenye muhtasari wa habari kwa kusema watumishi wa umma.

Waliposoma habari kwa kina na kwa maelezo picha ya AG bungeni ndio yalileta habari kwa usahihi.
 
OC za kuwawezesha kufanya kazi zimezuiwa,hata kufanya maendeleo binafsi kwa kupitia mikopo itakayokatwa kwenye mishahara yao nayo ni nongwa??,hivi hawa watumishi wameikosea nn haswaa serikali hii?,watakuwa na morali ya kufanya kazi kweli?,hivi wanasiasa wetu huko bungeni wapo kwa ajili ya nani haswaa?
Mwananchi wanakipenda sana chama cha mapinduzi kata 21/1, acha kiongeze moto.
 
Kuna muswada umefikishwa bungeni wa kutaka kuwachukulia hatua watumishi wa umma watakao kopa kwenye taasisi za fedha bila kupata kibali cha waziri wa fedha...iwapo atabainika kutakua na fine ya mil 5 au kifungo cha miaka kadhaa au vyote pamoja. Nafikiri namba zinasomeka
Wangeongezea na kunywa bia mpaka kibali cha waziri.
 
Kuna muswada umefikishwa bungeni wa kutaka kuwachukulia hatua watumishi wa umma watakao kopa kwenye taasisi za fedha bila kupata kibali cha waziri wa fedha...iwapo atabainika kutakua na fine ya mil 5 au kifungo cha miaka kadhaa au vyote pamoja. Nafikiri namba zinasomeka
Mkuu unapotosha, pitia vizuri vyanzo vya.habari yako
 
PSPF iko kwa ajili ya watumishi wa umma ,huenda sasa ni wakati muafaka kwa mfuko huu kutoa mikopo ili kuwakwamua watumishi kiuchumi
 
Kuna muswada umefikishwa bungeni wa kutaka kuwachukulia hatua watumishi wa umma watakao kopa kwenye taasisi za fedha bila kupata kibali cha waziri wa fedha...iwapo atabainika kutakua na fine ya mil 5 au kifungo cha miaka kadhaa au vyote pamoja. Nafikiri namba zinasomeka
Muww mnasikiliza habari vizuri basi muelewe vizuri ili kuepusha uwezekano wa kupotosha. Haya uelewe hivyo hivyo maana umesharipoti.
 
Zuio hilo la kukopa bila kibali cha Waziri wa Fedha ni kwa wakuu wa taasisi za umma pekee na sio mikopo binafsi kwa watumishi wa umma.

Na mikopo hiyo ni ile kwa ajili ya taasisi zao na sio mikopo binafsi

Swadakta mkuu,kwa maelezo hayo,ze zred iz clozed,senks kwa taarifa,ilaaaaaaaa,hivi Halmashauri za Wilaya sio taasisi za umma kweli,tupate kwanza definition ya muswada huu kwamba taasis ya umma ni nn
 
Back
Top Bottom