Hua najiuliza ni kwa nini wabunge wengi wa majimbo karibu wote ya CCM kwa baadhi ya mikoa ni matajiri sana lakini wananchi wao ni maskini sana.
Kwa nini matajiri wengi waliamua kugombea ubunge kupitia CCM? Au uongozi ndani ya CCM una Fursa ya kukwepa kodi bila kushitakiwa wala kuondolewa kwenye utumishi wa umma unapobainika kukwepa kodi.
Mikoa ya Mbeya ,Iringa, Lindi ,Mtwara, Dodoma ,Kigoma, Kilimanjaro, Tanga,Arusha, Zanzibar, Manyara,Masada,Songea na Rukwa wabunge wake na hata wale waliowahi kushika Madaraka ya uwaziri kwa kweli tukijaribu kuwaangalia wengi wao ni watu wa Kawaida sana na hawana Tabia za kujilimbikizia Mali kama hiyo mikoa ambayo sijaitaja. Hata ukiangalia kashfa nyingi za mikataba mibovu na skendo nyingi za ufisadi hazikuwahusisha sana.
Nadhani kuna aina ya wabunge na mawaziri wanaotumia uelewa mdogo wa wananchi kujilimbikizia Mali na Mara. Hata ukiangalia vijana wadogo wanaopewa madaraka wanajilimbikizia Mali kwa haraka haraka utafikiri wanahama nchi.
Lakini cha ajabu wale wakwapuaji hua wana majungu sana na wepesi kuwataja wengine.
Je,Wananunua ubunge au inakuaje?