Mustakabali wa Taifa letu uko mikononi mwetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mustakabali wa Taifa letu uko mikononi mwetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntagunata, Aug 9, 2011.

 1. N

  Ntagunata New Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  With all these scams emerging day by day ... where are we really heading to?

  Which stone is not turned?
   
 2. President Elect

  President Elect JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu wananchi wazalendo wapenda maendeleo, naomba sana mnielewe na mnivumilie.

  Awali ya yote, nawapa pole sana wananchi wenzangu kwa tabu mnazozipata kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili, hii ni changamoto kubwa kwetu sote. Nchi yetu tukufu na Taifa letu tukuka la Tanzania litatimiza miaka 50 ya uhuru mwezi Desemba mwaka huu, hiki ni kipindi kizuri kwetu sote kubadili msimamo na mtizamo dhidi ya watawala, kwamba badala ya kuwaachia kila kitu juu ya mustakabali wa nchi yetu, wakati sasa umefika wa kuwa na mawazo chanya juu jinsi ya kutuvusha kutoka hapa tulipo kuelekea nusu karne ijayo.

  Tanzania ni Taifa huru, je wananchi wake ni watu huru?

  Ndugu wananchi, tufunguke kifkra na kimatendo pia. Mimi nimechukua jukumu la kuongoza vuguvugu la mapinduzi ya kweli yatakayoleta ukombozi wa kweli wa mwananchi wa kawaida.

  Nawaomba sana mniunge mkono ndugu zangu ili tujikomboe na tuweze kupiga hatua, kutoka kwenye hali ya Taifa huru lenye watu maskini na wanyonge ndani ya nchi yetu, na kuwa watu huru wenye matumaini ya kufaidi rasilimali za nchi yetu.

  Tanzania ni nchi yenye vyama vingi vya siasa, ila wananchi wake wengi si wanachama wa vyama hivyo, nami nawakilisha kundi hili kubwa la wazalendo wapenda amani ambao hawafungwi na itikadi za chama chochote cha siasa.

  Katiba mpya ya nchi yetu ni lazima izingatie demokrasia ya kweli, kwa kuruhusu wagombea huru wasiotokana na vyama vya siasa katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

  Nimalizie kwa kuwatakia ndugu zangu waislam swaum yenye wingi wa heri katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, asanteni sana.
   
 3. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwakuwa makampuni ya mafuta yamegoma kuuza mafuta kwa bei iliyopendekekezwa hata baada ya kupunguziwa kodi, na kwakuwa police wetu FFU wetu wanajua tuu kuwapiga mabomu waandamanaji wa amani, na kwa kuwa inatuhumiwa kwamba Kikwete na Rizwani ni wafanyabiashara wakubwa wa mafuta, mimi ninapendekeza tuingie mitaani tuvichome moto vituo vyote vya mafuta vilivyogoma tukianza na Engen na tuzuie na kuchoma malori yote ya mafuta yanayosafirisha nje ...

  Hakuna sababu ya kuruhusu hawa wafanya biashara kupelekeka mafuta nje wakati sisi hapa hawatuuzii...

  Ni hoja yangu
   
 4. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Ni swali tu!

  Kila ninapopita watu wote kwa umoja wao wanakubaliana kuwa hali sivyo kama wanavyotarajia katika nchi hii na lawama zote zinakwenda kwa Serikali na kiongozi wao mkuu.

  1. Je ni watu kutokuwa na imani na serikali iliyoko madaerakani?
  2. Ni watu kutokuwa na mwongozo wa maisha katika kukuza uchumi na kujenga maendeleo?
  3. Je ni matatizao ya kisiasa zaidi kuliko hali halisi (ya jubuni kwa ajili ya kujinufaisha kisiasa)?
  4. ni utovu wa nidhamu wa wafanyakazi wengi wa serikalini wanaosababisha serikali ionekane tofauti na matarajio?
  5. Au ni wabaya wa kundi la wanasiasa walioko madarakani wanaeneza uvumi mbaya na kumchafua kiongozi aliyeko madarakani kumfanya aonekane mbaya ikiwemo kuhakikisha maamuzi yake hayatekelezwi na kila lililopangwa haliendi?
  6. Au ni elegelege wa wananchi wenyewe kutokujua haki zao na wajibu wao mambo yanapokwenda ndivyosivyo na kubaki kulalamika tu bila kuchukua hatua zozote?
  7. Au ni upole wa raisi na wema wake wa kuruhusu uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kila mtu kutoa maoni yake ndio uliopelekea kila mtu kuweza kuongea anavyoona na kupelekea hata uvumi wa serikali kuwa hairidhishi iwe imani ya kweli kuwa serikali sio nzuri?

  Nini tatizo?
   
 5. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  hapana, hapana hivyo ndo tutaharibu kabisa, hivyo ndo tutaharibu kabisa! Kitu kingine kinachotuongeza machungu kuona hata hatua hazichukuliwi, ee mola tusaidie tupo kwenye janga utata!
   
 6. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hv chadema wapo wapi muda kama huu?me sielewi kwann hawajaanda maandamano mpk saiv,zaidi ya siku 7??au wao maandamano wanaandaa kma wakiwa wanataka madaraka tu?

  Suala la jailo wapo kimya suala la mafuta wapo kimya,jaman mananiangusha chadema,andaeni maandamano jmn tuwashinikize hawa wahuni watoke madarakani,imefika muda tuwe kama watu wa london kwa kuchoma hivi vituo vya mafuta na mali za mafisdi pai
   
 7. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Nakupinga, Uamuzi wa kuchukua hatua sisi wenyewe ndo sahihi, kama watu tuliowapa jukumu la kututetea wanatiwa kigugumizi na conflict of interest, kwanini tusichukue maamuzi sisi wenyewe, je tutaendelea kuumia hivi mpaka lini?
   
 8. k

  kokuhija Member

  #8
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha fikra potofu! then utapata hayo mafuta? yaelekea wewe na hao wauza mafuta lenu moja hamhitakii mema tz!
   
 9. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  tunapenda kutoa taarifa kwa uma kuwa kutakuwa na maandamano ya kitaifa yatakayoishia viwanja vya mnazi mmoja kesho saa 5 asubuhi kujadili mstakabala wa taifa hili.

  Upatapo taarifa hii mwaarifu na mwenzako. Tuma sms walao kwa watu kumi

  hayana uhusiano na vyama vya siasa. Hivyo watanganyika wote tutoke kama mtu mmoja.

  Huu ndio mwanza wa mapinduzi ya kizazi kipya
   
 10. h

  hittler Member

  #10
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kweli Tanzania ndiyo inafikia mwisho wa majigambo yake yaliyokuwepo tokea enzi za mababu, watu waliimba nyimbo nzuri za kuisifu Tanzania, wakazitaja rasilimali zilizopo na amani ya kudumu iliyokuwa kivutio cha mataifa mbalimbali. Leo hii rasilimali wananufaika wachache, watu walio wengi wameendelea kuwa maskin, kukandamizwa, madini yanaibiwa kila kukicha, wanyama wanataifishwa. Duh! Kikwete atajibu nini? Yeye kwake kila kitu kheri. Kweli tukae kimya na kuiacha nchi inazama? Tuamkeni jamani,
   
 11. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  binafsi inaniuma sana kuna wakati naomba nchi hii iongozwe na dikteta ili watu tuamke usingizini maana bado tuko usingizini na kila mtu anafanya anavyopenda. I think we need a DEVELOPMENTAL DICTATORSHIP SYSTEM to push the country forward. We need harsh rules and penalties for those who fail too abide to the orders of the dictator.
   
 12. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Je, wabaya wa JK ndo wanaendelea na mapambano kwa kutumia vyombo mbalimbali kumuangamiza? Au ni hali halisi ya mgogoro wa Serikali na Wafanya biashara ya Mafuta? Siamini hichi kiburi cha wafanya biashara hawa! Ingekuwa enzi za Mwalimu... Au Mzee wa Uwazi na Ukweli... hali ingekuwaje?
   
 13. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Serikali ya Tanzania imeshindwa kufikia viwango vya utoaji na usimamiaji wa huduma za kijamii nchini na hii ni kwa kila sector sio ya Nishati tu ni kuanzia afya,elimu,miundo Mbinu na usimamiaji wa rasilimali za kitaifa.
  Imeshindwa kutumiza ndoto za watanzania,ambao wengi wetu tunaamini kuwa Tanzania ni nchi ya asali na maziwa..
  sasa kama serikali imetoa "Compliance order" kwa wafanyabiashara wa mafuta na hadi hivi sasa mafuta/wese halionekani mtaani...basi sisi kama wananchi tutoe "Compliance order" kwa serikali ili iweze kufufanyia tunayo yahitaji.
   
 14. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Licha ya rasilimali nying sn zilizopo Tz lkn maisha ya waTZ yanazidi kuwa magumu kila kukicha heri ya jana, viongozi wanaiba mabilion ya watanzania wanaachwa, raia wanauwawa wakidai haki zao, mfumuko wa bei za kila kitu, njaa, umeme, mafuta na matatizo mengne mengi, JE WATANZANIA TUFANYE NINI ILI KUJIKOMBOA KWENYE MATATIZO HAYA??
   
 15. M

  Mwamatandala Member

  #15
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ninasikitishwa kuona serikali iliyopewa ridhaa kwa niaba ya wananchi inayatolea maamuzi mepesi mambo ambayo yanagusa maisha ya watanzania walio wengi.
  Tulianza na uhaba wa umeme,tukapigwa danadana.Na sasa limekuja suala la mafuta,serikali inatoa kauli zisizo na mashiko.
   
 16. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,771
  Trophy Points: 280
  Kiukweli tumekuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Matatizo kama haya sio mageni hapa duniani. Kuna mwanajursiprudensia mmoja alipata kunena kwamBa " Serikali ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa" Hii inamaanisha kuwa uhusiano tulionao kati yetu na viongozi wetu ni mkataba kama mikataba mingine, Kama upande mmoja kati ya waliongia mkataba hautaridhishwa na mwenendo mbovu juu ya mkataba unaotendwa na upande wa pili wa aliyeingia mkataba, ni dhahiri kuwa upande uwo ambao hujaridhishwa na mkataba husika unaweza kuamua kuvunja mkataba uwo.

  Kwa mwenendo wa serikali hii iliyopo madarakani imefikia hatua wananchi tunapaswa kuvunja nayo mkataba. Kwa tukio hili la janga la mafuta hapa nchini lililosababishwa na serikali dhidi ya wananchi wake, sisi wananchi tulitakiwa tushike mabango tuingie barabarani tukionyesha nia yakutaka kuvunja mkataba huu na serikali iliyopo madarakani.Hili janga la mafuta ni golden chance ambayo inatuwezesha wananchi kuamasisha serikali ijiengue kwa makosa inayofanya.

  Watanzania tunahisia ya kumtoa mkoloni mweusi madarakani ila tunakuwa wanafki tunaishia kuongelea ili swala vyumbani mwetu. Swala la maandamano ya kuipinga serikali tusiwaachie vijana wetu wa sokoni na vijana wa vijiweni. Katika nchi mbalimbali ambazo wananchi wametimiza adhma yao kwa kutumia maandamano yamewajumuisha wakulima,wafanyabishara,wanavyuo,wafanya kazi ni wale wote wasio na kazi kwani wote hawa ndo waadhirika wa mfumo mbovu wa serikali. Watanzania tusiwe wanafki wala waoga na kuwaachia vijana wasio na kazi au wenye vipato vya chini pekee ndio washike mabango na kuandamana kupinga mfumo mbovu wa serikali yetu sote.

  Tuonyeshe kujitambua na kuionyesha serikali nia ya wazi ya kutokubaliana na mwenendo wake kwa kudai haki yetu ya msingi kwa njia ya maandamano kama mataifa mengine yalioonyesha utayari huu. Tunayoyasoma kwenye historia yasiishie kwenye vitabu tu, bali yatupe motisha wa kufanya yaliyofanywa na wenzetu waliotangulia kufanya. Tusione aibu kushika bango linaloonyesha haki ya msingi tunayoidai.

  Hili ni janga la taifa zima kwa ujumla hatunabudi kuweka pembeni hisia zetu za vyama kwa kuzingatia ukweli na haki. Kwa pamoja tupaze sauti na kuikemea serikali pale inapokosea, Tukubali ukweli na kupingana na uongo, tuweke misimamo yetu ya kichama pembeni ili kwa pamoja tukatae giza na kukubali mwangaza. Tusigawanywe na vyama alafu tufumbwe na tupumbazwe ili tusiseme ukweli na kudai haki.

  Tukipaza sauti kwa pamoja pasipo kupumbazwa na hisia za kivyama hakika tutasika na mkoloni mweusi atadondoka pale anapotunyima tusulubu kwa mfumo mbaya wa uongozi.

  Kenyatta mkubwa alishawai kumuambia Mwl Julius Kambarage Nyerere kuwa "Mwalimu unaongoza maiti" akiwa anamaanisha Watanzania wamepumbaa kiasi cha kupelekeshwa kwa namna yoyote viongozi wao watakavyoamua.

  Tubadilike tufanye maamuzi magumu sote kwa pamoja tuseme ndio pale tunaporidhiswa na mfumo mzuri wa serikali, pia tupaze sauti kwa pamoja tuseme hapana pale ambapo hatutaridhishwa na mfumo mbovu wa serikali. Tusikubali tena kupoteza golden chance ya kuinyooshea serikali kidole kwa kuandamana tutakayoipata pale mfumo mbovu wa serikali utakapojitokeza.

  TUAMKE USINGIZINI WATANZANIA.
   
Loading...