Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
asante kwa maneno yako matamu hahahahahahah
Ruta huyo player number yake ngapi kiwanjani au hana number?
Sio ma-player wote wenye vijisent...huwa wanatumia maneno mazuuuri kwenye ku-soundisha.
Ukimwona mitaa yenu,jua kunakiumbe kesha umia,akimaliza mi meno kenu,ujinga wake anafurahia,achagui watoto,wakezenu,popote ye upitia,mtaji dhiki zenu,malengo yake kutimia,sasa kazi kwenu,kum"bania ama kumwachia,chake c chenu,ila chenu chake ndio kanuni ana2mia,na c huko kwenu,pande nyingi wameshalia,Smile,First lady,Lizzy na wengine c wenzenu?bac waulizeni kazi yake wanaijua.Haaaaaa!player bana.Last edited by skendo; Today at 08:17.
Cha ajabu man akiwa player ndio kwanza mademu huzidi kuzimika naye...!!!
Player ni fataki na hana taswira nyingine ingawaje huificha
Wasifu wake huvuma kwani vigezo vingi huvikamilisha bayana
Mabinti humpapatikia na tamaa yao huwa ndiyo suluba yao
Player ana makorokoro kibao na vijisenti havimpigi chenga kamwe
Player hana hasira na uvumilivu bila kikomo huwa ni rungu lake
Mustakabali wa Player ni kuvuna asichopanda!
Kwa kuelewa udhaifu wa mabinti yeye huwavuna kwa rungu lake
Shida zao wakimililia yeye ni kimbelembele kuzitatua bila kalenda
Ingawaje hutuliza kero zao lakini moyo wake ni wa kwake pekee yake
Mabinti hupoteza maboya wakidhani Player anawahusudu kumbe la!.
Mwenyewe Player aelewa kawekeza mtaji wa nguvu na asubiria kivuno.
Mustakabali wa Player ni kuvuna asichopanda!
Player huficha msimamo wake ndani ya kichaka cha uanamalenga
Malenga malenga huwapumbaza nayo nao kumuwazawaza bila ukomo
Si usiku au mchana wao hujadili upendo wa Player bila ya kujua huo ni mtego
Player ajua fika tamaa ya mabinti ni kupendwa naye awahadaa kuwa anawapenda
Pia hachelei kuwakumbusha-kumbusha ya jinsi anavyoweweseka nao bila bureki!
Mustakabali wa Player ni kuvuna asichopanda!
Mtambue Player pale uonapo hataki mikwaruzano nawe unapombishia!
Mtambue Player pale ambapo penye udhia hukimbilia kuweka rupia!
Mtambue Player pale ambapo hudai malipo ya uwekezaji wake bila ya aibu!
Mtambue Player pale ambapo huhakikisha biashara yake huwa ni asubuhi tu!
Mtambue Player pale ambapo uonapo anavuma sana na kila binti anamsaka!
Mustakabali wa Player ni kuvuna asichopanda!
Rutashubanyuma mademu wengi huzimika na players coz wanadanaganyika kuwa players ni noma kitandani...mathematics.....................ni kweli kwa sababu mahesabu yake huwa ndiyo yanawazuzua ingawaje huishia kullizwa naye!
[MENTION]Rutashubanyuma mademu wengi huzimika na players coz wanadanaganyika kuwa players ni noma kitandani...
na walio wengi ni ulimbukeni tu hamna lolote
chanzo cha player kupata wanawake wengi, ni kwamba huwa wana maneno machungu ila yanakuwa yamepakazwa asali kwa juu,so ukiyasikia utahc ni matamu kumbe ni hit n run!