Musoma: Shule yanusurika kufungwa kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kishirikina

Uchawi haupo!

Kinachowasumbua ni ujinga [kwa maana halisi ya ujinga] tu.

Lakini Mungu yupo sio?

Yesu alikuja kweli au na hilo tulipigwa?

Kama unakubali alikuja je unakubali alifanya miujiza pi?

Manabii na mitume wanaotajwa na vitabu vya dini walikuwepo kweli au nayo ni ujinga ujinga tu?

Vipi kuhusu miujiza waliofanya hao manabii na mitume kama ni kweli au janja janja tu?
 
Mkuu wa wilaya ya Musoma, Vicent Naano ametoa wiki moja kwa wananchi wa kijiji Kakisheri kata ya Nyakatende wilaya ya Musoma Vijijini wanaojihusisha na matukio ya kishirikina kuacha vitendo hivyo haraka na endapo vitandelea basi atafunga shule na kuwahamisha walimu wa Shule ya Msingi Kambarage.

Shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na matukio yasiyo ya kawaida ikiwemo walimu kuingiliwa kimwili nyakati za usiku, kulazwa nje na wanafunzi kudondoka ovyo na kupiga kelele.

DC Naano ametoa maagizo hayo baada ya kutokea kwa tukio la wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo kuanguka na kupiga kelele, kukuta chakula aina ya makande kikiwa kimewekwa chooni hali iliyowalazimu walimu, wazazi na wanafunzi kupiga kura ili kubaini anayefanya matukio hayo kwa imani ya kishirikina.

IPP
Akifunga shule ndio wachawi watakuwa wamefanikiwa lengo lake. Mkuu wa wilaya tena mkristo asijifanye hajui nini cha kufanya hata kama ni shule ya serikali. Kama hajui cha kufanya basi ajue kwa Yesu Kristo ndio dawa ya yote hayo, amtafute mtumishi wa Mungu Aliye Hai amalize mambo hapo mapema asubuhi.
 
Kama sikosei kipindi hicho Kigoma huko visiwani.Mhe.Joseph Simbakalia aliwahi tatua mgogoro wa wananchi wa namna hiyo uliodumu kwa miaka 20.Huku wakikosa huduma za afya na mambo mengi sana.

Wenyewe wachawi wakaweka kamati ya ulinzi na kupambana na mambo yao.Miaka 12 iliyopita niliona habari hiyo ITV.

Mapigo kumi yale wa Misri na watu bado walikuwa wabishi,tena miaka hiyo watu kuongea na God.Ilikuwa chapchap.
Ilitumia miaka na miaka wa Misri kuelewa mambo makuu.

Wafanye maaendeleo vijijini vya jirani,wachaguliwe watu wakashuhudie maendeleo maeneo yasiyo ya kwao.

Waje mijini hao waone watu wanavyoroga kwa akili hapo Ubungo Junction..Tazara...:D:D:D:D:D

Wakae na mchina kule Baharini wanakojenga daraja..watajifunza jambo kuu juu ya uchawi wa maendeleo.
 
Hilo eneo hakuna watumishi wa Mungu?
Mbona kazi ndogo,watumishi wa Mungu ,waombaji waungane wakapige kazi kwenye hilo eneo km huo uchawi utaendelea!

JESUS IS LORD
 
Akifunga shule ndio wachawi watakuwa wamefanikiwa lengo lake. Mkuu wa wilaya tena mkristo asijifanye hajui nini cha kufanya hata kama ni shule ya serikali. Kama hajui cha kufanya basi ajue kwa Yesu Kristo ndio dawa ya yote hayo, amtafute mtumishi wa Mungu Aliye Hai amalize mambo hapo mapema asubuhi.
Eti anatishia kufunga shule,hajui kuwa ndo wanachotaka hao watu wa giza!

JESUS IS LORD
 
Back
Top Bottom